Buriani Mzee Ruksa: Ni Deng Xiaoping Wetu wa Mageuzi ya Kiuchumi, Demokrasia, Haki za Binadamu na Uhuru wa Habari. Asante kwa Ruksa Zako, Pumzika!

Buriani Mzee Ruksa: Ni Deng Xiaoping Wetu wa Mageuzi ya Kiuchumi, Demokrasia, Haki za Binadamu na Uhuru wa Habari. Asante kwa Ruksa Zako, Pumzika!

Aisee!

Kula ilikuwa changamto, sukari changamoto. Nguo za viraka. Haikutosha, hata sabuni na dawa ya kupigia mswaki?

Kama kitu kama sabuni na dawa ya kupigia mswaki vilionekana anasa nakosa cha kusema kiukweli! Mlipitia kipindi kigumu sana.
Kulikuwa na viatu fulani vya mbao viliitwa magongo, ukipigwa teke la ugoko lazima ukae chini. Tulikuwa choka mbaya miaka baada ya vita ya Kagera.
 
Nimeandika weeee nikafuta. Ila ubaguzi wa dini sio mzuri.
Pia sikiliza watu wanavoelezea CV ya mtu hatakama kuna mapungufu ila alikua na dhamira njema,alitumikia watu katika kipindi kigumu
Kuwa hadithi nzur Kwa watakaosimuliwa, Mwinyi amewauma roho watu Kwa sifa anazomwagiwa, huyu Baba anapendwa haswa ndo mana wazaz wengi waliwapa watoto wao jina la Mwinyi
 
sio alishindwa ku control Bunge, aliridhia Demokrasia ichukue nafasi yake

Wabunge wengi kupitia G55 walipiga kura kuridhia kurejeshwa serikali ya Tanganyika ambayo hadi leo inaliliwa, Mwinyi akajadiliana na PM wake Malecela na Katibu Mkuu wa Chama Horace Kolimba wakaona bora waridhie kilio cha wengi

kuna Machawa wakamjulisha Mwl Nyerere ndio mbio mbio akaomba iitishwe Kikao cha Wabunge cha CCM walati huo Wabunge wote ni CCM akaomba awahutubie kwa kuwa kule Bungeni hatambuliki kisheria

ndio akawaibukia akatibua mpango akawaambia mkitaka Serikali 3 kwanza mjitoe CCM kwa kuwa sio sera ya Chama , wakati huo ukijitoa CCM kama vile umejitoa uhai na mchezo ukaishia hapo wa Serikali 3


Unaemwita Kilaza hakuwa na lugha za kukera wala kufedhehesha ila naamini kama kwny familia yako wangepewa fursa ya kuchagua Baba kati yako na Yeye kwa kura za siri angepita kwa kura za ushindi wa Tsunami
Nzasa au Sihaba Kwa kweli hakuwa na lugha za kukera, 😅😅😅 eti wachague Kati ya yy au Mwinyi
 
Kwa shida nilizozipata wakati wa Nyerere hata ukiuza dawa ya mbu unaitwa mlanguzi!!!

Leo mtu anambie Nyerere alikuwa mzuri huwa nashangaa sana na ndio maana wakati mwengine nashindwa kuchangia chochote kwa kujua wengi wanaobisha ni watoto wa juzi madhila tuliopitia hawayajui
Watoto WA juzi pia hawakuhadithiwa watu walivyoteseka
 
Kuwa hadithi nzur Kwa watakaosimuliwa, Mwinyi amewauma roho watu Kwa sifa anazomwagiwa, huyu Baba anapendwa haswa ndo mana wazaz wengi waliwapa watoto wao jina la Mwinyi
Kweli mkuu hata sifa njema na nafuu kwa mtu fulani wengine vinawatesa
 
Nilikua na shaukun kufahaku juu ya vita ya member chai leo umenijubu . Shukrani sana kwa uandishi mzuri na mtirirko mzuri wa masimulizi yako. Seba akojiwe sana @pasmayala
 
Ni kipindi cha nguo kupigwa viraka,Enzi hizo watu wanavaa nguo imepigwa viraka vya rangi tofauti tofauti

Watu walivaa nguo zilizotoboka ,Ilikuwa hakuna kumshangaa mtu

Wanafunzi wanaenda shule peku peku bila viatu na unawakuta wanakimbia mchaka mchaka kwa uzalendo

Enzi hizo sherehe za Chrismass na Idi zilikuwa sherehe kweli

Watu kabla ya miezi miwili christmass au idd mnaanza kutafuta mchele na kuuhifadhi ndani kwa ajili ya maandalizi ya sherehe,Unaweza enda siku ya sherehe sokoni ukakosa vinywaji na vyakula
Kwa sisi tuliokuwepo enzi hizo, kiukweli tumetoka mbali!. Mwache Mwinyi apumzike kwa amani.
P
 
Stupid comment.

Mwinyi kakabidhiwa nchi noti kubwa ikiwa sh 100. Kashauriwa na bwana zake kuwa suluhisho ni kuchapisha manoti. Matokeo ikawa ni hordes of money chasing too few available goods.

Elimu ya madrasa haiwezi kumkomboa mwanadamu.
Mwinyi alisoma chuo england hakua kilaza
 
Wanabodi
View attachment 2923058Siku ya leo, tunampunzisha Mzee wetu, Rais Mtaafu wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi, kwa jina maarufu la Mzee Rukhsa, kwenye nyumba yake ya malalo ya makao ya milele.

Mara ya Kwanza Kulisikia Jina la Ali Hassan Mwinyi.
Kwa mara ya kwanza jina la Ali Hassan Mwinyi, nililisikia mwaka 1977 nikiwa darasa la 3 shule ya msingi, wakati huo akiwa ni Waziri wa Mambo ya Ndani wa serikali ya Nyerere, alipolazimika kujiuzulu kutokana na kashfa ya vifo vya watuhumiwa wawili wa mauaji ya vikongwe, huko Mwanza mwaka 1976.

Mwinyi hakuwa peke yake aliyejiuzulu kutokana na kashfa hiyo, bali Makamo wa pili wa rais na Waziri Mkuu, Rashidi Mfaume Kawawa, pia aliondolewa!, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, anyeshughulikia Usalama wa Taifa, Peter Siyovelwa aliondolewa!. Wakafuatiwa na watendaji wakuu wa vyombo vya usalama Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Emelio Mzena, akastaafishwa kwa manufaa ya umma!, Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Samweli Pundugu akastaafishwa kwa manufaa ya umma, na Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza pia akapumzishwa.

Mwalimu Nyerere alikuwa sio mtu wa mchezo hata kidogo!, kwani baada ya kuwafagia kule juu, fagio la chuma, likatua mjini Mwanza, likaanzia kumfagia Mkuu wa Mkoa Peter Kisumo, akaenda na maji, RPC wa Mwanza, RSO, OCD, na DSO wa Mwanza, kwanza wote wakafutwa kazi, kisha wakarejeshwa vijijini kwao, kwa kusombwa na Land rover 109 usiku usiku na kurudishwa kwenye their places of domicile na mwisho wa siku walikuwa kushitakiwa kwenye ile kesi maarufu, "Kesi ya Mauaji Mwanza" ya mwaka 1976. Mtu pekee aliyesalimika kati ya hao washtakiwa ni mtu mmoja tuu, aliyeitwa Andrew Mayalla, na salama yake, mdogo wake anayetwa Mathew Kasanga, kumuwekea wakili mahiri wa wakati huo, Wakili Murtaza Lakha, kumtetea kaka yake, lakini wengine wote, walikwenda na maji na walikula mvua za kutosha!. Ni kupitia tukio hilo ndipo nilipoanza kulisikia jina la Ali Hassan Mwinyi. Hiki kisa cha Kesi ya Mauaji Mwanza pia nilikihadithia kwenye bandiko hili TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!
Sijui uwajibikaji wa aina hii ya enzi za Nyerere, ulikuja kupotelea wapi, siku hizi watuhumiwa wanakufa mikononi mwa polisi, and no body cares!.

Tukio hilo lilileta mageuzi makubwa nchini mwetu, kwanza Idara ya Usalama wa Taifa, ilifumuliwa na kusukwa upya kwa kufanyiwa mabadiliko makubwa, ikaletwa sheria ya usalama wa Taifa, ya 1976, Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 na katiba mpya ya mwaka 1977.

Jina la Ali Hassan Mwinyi, nikaja kukutana nalo tena shule ya msingi, jijini Dar es Salaam, tukisoma na mtoto wake Hussen Mwinyi (Dr)aliyenitangulia madarasa mawili. Baada ya shule ya Msingi nikajiunga shule ya sekondari ya Tambaza, ile mwaka 1985 Rais Mwinyi anakuwa Rais wa Tanzania, yule mtoto wake Hussein Mwinyi alikuwa anasoma PCB Tambaza! alikuwa darasa moja na mtoto wa Malecela, Seche. Kitendo cha mtoto wa rais na mtoto wa Makamo wa Pili wa Rais na Waziri Mkuu John Malecela kusoma shule moja, na halikuwa jambo dogo!, sasa ndio nikazidi kumfahamu Ali Hassan Mwinyi kwa karibu, wakati huo hapo Tambaza pia tuko na mtoto wa Nyerere na Mtoto wa Mkapa, darasa moja.

Mwanzo wa Mwinyi Kutwa Mzee Ruksa.

Wakati Mwinyi anachukua urais ile 1985, hali yetu ya Uchumi ili dhollfu bin taaban, baada ya vitavya Kager ana Mwalimu Nyerere kutangaza miezi 18 ya kufunga mikanda, mambo kiukweli yalikuwa magumu, tumekula unga wa Yanga, kutoka Marekani ambao kule kwao ni chakula cha mifugo!, Watu wamevaa magunia, sandarusi hadi sisi wanafunzi nchi nzima tumevaa uniforma ya kitambaa cha madurufu, ambacho nip amba chafu ya kutupa!.

Mahitaji muhimu yote ni kwa resheni kupitia maduka ya kaya, tulikuwa tunapanga foleni siku nzima kusubiria kuuziwa kilo mbili mbili za sukari, hivyo Watoto wote mnatumwa, ili kuwahi foleni, watu walidamka asubuhi na kupanga mawe, gari linaweza kuja saa 10 jioni au siku nyingine kutoka bila bila, haliji kabisa.

Nchi za mabeberu zilimpa Mwalimu Nyerere masherti magumu ya kutupa misaada, ndipo Mwalimu akaamua kuliko kukubali misaada ya masherti na kugeuka nyuma akageuka jiwe, bora aachie ngazi, kwa mtindo wa kung’atuka na kumpisha Ali Hassan Mwinyi. Hivyo Mwinyi aliipokea nchi ikiwa kwenye dhiki kubwa!.

Baada ya ya kuingia rais Muislamu, kukaibuka vikundi vya Waislamu wenye siasa kali, kwanza waligomea Nguruwe wasichinjiwe mahali pamoja, na wanyama wengine kwasababu nguruwe ni haramu kwa Waislamu,
na isiuzwe bucha zile zile za nyama ya kawaida.

Vikundi hivyo vikaleta vurugu za kulazimisha nyama ya nguruwe ipigwe marufuku kwasababu ni haramu, na kuanzishwa mihadhara ya kashfa, kwa wanazuoni wa Kiislamu kuikosoa Biblia na kusema nguruwe hata kwenye Biblia ni Haramu. Vurugu hizo zikapelekea kuvamia mabucha ya nguruwe na kuvunja kisha kukimbilia kujificha misikitini kulikopelekea vurugu za Msikiti wa Mwembecha miaka kadhaa baadae.

Rais Mwinyi akatangaza rukhsa mtu yoyote kula kitu chochote, hakuna ruhusa ya mtu mwingine yeyote kuingilia uhuru wa mtu wa dini nyingine yoyote kula chochote, “Ruksa” na huo ukawa ndio mwanzo wa kuitwa Mzee wa Ruksa, wale wahuni kwa kisingizio cha dini walishughulikiwa kikamilifu, ikiwemo Msikiti wa Mwembechai Kuvamiwa, tena ikatokea mmoja wa wana vuguvugu hawa ni mshikaji wangu sana wa deski moja sekondari ya Tambaza, akiitwa Hassan.

Baada ya kuzifungulia hizo ruksa, alikuja kufungulia ruksa nyingine nyingi za biashara, Uchumi, akaruhusu mitumba, akaruhusu Chai Maharage, akalipindua Azimio la Arusha lililoweka miiko ya uongozi na kuleta Azimio la Zanzibar ambalo liliruhusu viongozi kufanya biashara na kumiliki mali na hapa sasa ndio viongozi wa umma wakaanza kuwa matajiri na kuupindua uchumi wetu kutoka uchumi wa kijamaa na kuingia kwenye uchumi wa kibepari wa nguvu ya soko, market economy.

Ruksa nyingine kubwa Rais Mwinyi aliyotuachia ni ruksa ya mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini Tanzania kiasi kwamba sifa ya Baba wa demokrasia Tanzania inamstahili kabisa!, Mwinyi ndie Deng Xioping wetu!.

Japo Rais Mstaafu, Ali Haasan Mwinyi, Mzee wa Rukhsa, ametutoka kwa kutangulia mbele ya haki, huku nyuma Watanzania tunaendelea kuzifaidi rukhsa zake, tutanzienzi milele, na tena sio tuu ametuachia Rukhsa, pia ametuachia na kale ka copy pale Zanzibar!, cha mtu rahimu kama yeye!.

Akina sisi, tayari tumeisha mshauri Mama, kama hoja Hivyo kama HII sauti ni sauti ya kweli, na kama vipi 2025, ataona ni parefu, hakuna ubaya, akikapisha kale ka Copy kule kaje huku kutufungulia ruksa nyingine zote zilizobakia!.

Buriani Ali Hassan Mwinyi, Mwendo Umeumaliza.

inna lillahi wa inna ilayhi rajiun
(إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّ إِلَيْهِ رَاجِعُونَ‎)

Paskali.
ALAZWE MAHALI PEMA STAN KATABALO.
 
Kuna kipindi alipwaya mpaka Nyerere aliamua kumsaidia.
No ilikuwa sio kumsaidia bali ni kumuingilia!.
Moja ya issue Nyerere aliyo iingilia ni suala la OIC lililopelekea wabunge wa G.55 kuidai serikali ya Tanganyika. Mwalimu Nyerere ilikuwa mkali kwelikweli, ila ni kumuingilia tuu OIC haina tatizo na serikali ya Tanganyika haina tatizo
P
 
Mmojawapo ni huyu Stroke ..toto la miaka ya 2000 linachojua ni ChaDema,Mbowe na kunakili ujinga na matusi ya Lema au mdude Mdude_Nyagali mtandaoni.

Hovyo sana hili toto. Hata Maghayo anakuwaga ana afadhali
Huyu member ni ccm lia lia kama ulikua humjui sio hata chadema
Ujinga wako ni kudhani kila mtu anayepinga ni chadema
 
Mimi huwa kuna mambo wanamsifia mzee Ruksa lakini mimi huwa naona ni kama kujikomba au kutofikiria kwa kina.
1. Ni kweli aliruhusu biashara huria, lakini nina uhakika ni kutokana na mabadiliko ya dunia, na hata kama Nyerere angeendelea kuongoza, angefanya hivyo hivyo. Anyways, kwa hili nampa maksi 75%.
2. Vyama vingi na demokrasia. Hili hakuwa na jinsi kwa sababu yalikuwa ni mabadiliko ya dunia nzima, na hata zile serikali za kufashisti zilijikuta zikiingia kwenye huo mfumo. Na mbaya zaidi, alileta mabadiliko ya bandia kwa sababu hakupenda kubadilisha mfumo wa utawala uendane na hali halisi. Hili nampa maksi 40%
3. Uhuru wa vyombo vya habari. Hili nalo alifeli kwa sababu aliachia uholela wa habari na siyo ubora wa habari. Matokeo yake mpaka leo hali ni mbaya sana kwa kuwa sekta ya habari imekuwa ni sekta ya kitapeli ambayo watu ''wajanja wajanja'' wanaingia ili kutafuta kula yao.
4. Na mwisho niseme kuwa mwalimu Nyerere alisaidia sana kurekebisha mambo yalipokuwa yanaenda mrama kipindi cha utawala wa Mwinyi. uzuri wa Mwinyi ni kuwa alikuwa mnyenyekevu na alikubali kusahihishwa pale alipoteleza.
Mwinyi alikua mr yes man wa nyerere
 
Hii ndio faida ya freedom of expression, uko huru kuita wenzako vichaa na nikaheshimu mchango wako na mawazo yako kuwa kumfananisha Mwinyi na Deng Xioping ni ukichaa!.
P
Ni ukichaa sababu xioping deng aliitoa china kutoka nchi maskin mpaka nchi ya pili kwa uchumi mkubwa huwezi mfananisha na mwinyi

Simpondi mwinyi hapana
Japokua mwinyi alileta mabadiliko ila still to date Tanzania ni nchi maskini
 
Ni ukichaa sababu xioping deng aliitoa china kutoka nchi maskin mpaka nchi ya pili kwa uchumi mkubwa huwezi mfananisha na mwinyi

Simpondi mwinyi hapana
Japokua mwinyi alileta mabadiliko ila still to date Tanzania ni nchi maskini
By the time Mwinyi anachukua nchi, how old were you?.
P
 
Back
Top Bottom