Siku ya leo, tunampunzisha Mzee wetu, Rais Mtaafu wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi, kwa jina maarufu la Mzee Rukhsa, kwenye nyumba yake ya milele.
Kwa mara ya kwanza Jina la Ali Hassan Mwinyi, nililisikia mwaka 1977, wakati huo akiwa ni Waziri wa Mambo ya Ndani wa serikali ya Nyerere, alipolazimika kujiuzulu kutoka na kashfa ya vifo vya watuhumiwa wawili wa mauaji ya vikongwe, huko Mwanza mwaka 1976.
Mwinyi hakuwa peke yake, bali Makamo wa pili wa Rais na Waziri Mkuu, Rashidi Mfaume Kawawa, pia aliondolewa, Waziri wa Ofisi ya Rais, anyeshughulikia Usalama wa Taifa, Peter Siyovelwa aliondolewa, wakafutiwa na watendaji wakuu wa vyombo vya usalama Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Emelio Mzena, akastaafishwa kwa manufaa ya umma, Mkuu wa Polisi, IGP Swamweli Pundugu akastaafishwa kwa manufaa ya umma.
Baada ya Baba wa Taifa kuwafagia kule juu, fagio la chuma, likatua Mwanza, Mkuu wa Mkoa Peter Kisumo, akaenda na maji, RPC wa Mwanza, RSO, OCD, na DSO wa Mwanza, wakafutwa kazi na kushitakiwa kwenye kesi maarufu ya Mauaji Mwanza yam waka 1976. Mtu pekee aliyesalimika kati ya hao washtakiwa ni mtu mmoja tuu, aliyeitwa Andrew Mayalla, na salama yake, mdogo wake anayetwa Mathew Kasanga, kumuwekea wakili mahiri Murtaza Lakha, kumtetea kaka yake, lakini wengine wote walikula mvua za kutosha!.
Tukio hilo lilileta mageuzi makubwa nchini mwetu, kwanza Idara ya Usalama wa Taifa, ilifumuliwa na kusukwa upya kwa kufanyiwa mabadiliko makubwa, ikaletwa sheria ya usalama wa Taifa, ya 1976, Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 na katiba mpya ya mwaka 1977.
Jina la Ali Hassan Mwinyi, nikaja kukutana nalo tena shule ya msingi, tukisoma na mtoto wake Hussen Mwinyi (Dr)aliyenitangulia madarasa mawili. Baada ya ya shule ya Msingi nikajiunga shule ya sekondari ya Tambaza, ile mwaka 1985 Rais Mwinyi anakuwa Rais wa Tanzania, yule mtoto wake Hussein Mwinyi alikuwa anasoma PCB Tambaza!, kitendo cha mtoto wa rais kusoma shule moja, halikuwa jambo dogo, sasa ndio nikazidi kumfahamu Ali Hassan Mwinyi kwa karibu, wakati hapo Tambaza pia tuko na mtoto wa Nyerere na Mtoto wa Mkapa, darasa moja.
Mwanzo wa Mwinyi Kutwa Mzee Ruksa.
Wakati Mwinyi anachukua urais ile 1985, hali yetu ya Uchumi ili dhollfu bin taaban, baada ya vitavya Kager ana Mwalimu Nyerere kutangaza miezi 18 ya kufunga mikanda, mambo kiukweli yalikuwa magumu, tumekula unga wa Yanga, kutoka Marekani ambao kule kwao ni chakula cha mifugo!, Watu wamevaa magunia, sandarusi hadi sisi wanafunzi nchi nzima tumevaa uniforma ya kitambaa cha madurufu, ambacho nip amba chafu ya kutupa!.
Mahitaji muhimu yote ni kwa resheni kupitia maduka ya kaya, tulikuwa tunapanga foleni siku nzima kusubiria kuuziwa kilo mbili mbili za sukari, hivyo Watoto wote mnatumwa, ili kuwahi foleni, watu walidamka asubuhi na kupanga mawe, gari linaweza kuja saa 10 jioni au siku nyingine kutoka bila bila, haliji kabisa.
Nchi za mabeberu zilimpa Mwalimu Nyerere masherti magumu ya kutupa misaada, ndipo Mwalimu akaamua kuliko kugeuka nyuma akageuka jiwe la chumvi, bora aachie ngazi, kwa mtindo wa kung’atuka na kumpisha Mwinyi. Hivyo Mwinyi aliipokea nchi ikiwa kwenye dhiki kubwa.
Baada ya ya kuingia rais Muislamu, kukaibuka vikundi vya Waislamu wa siasa kali, kwanza waligomea Nguruwe wasichinjiwe mahali panoja, na nyama ya nguruwe isiuzwe bucha zile zile za nyama ya kawaida.
Vikundi hivyo vikaleta vurugu za kulazimisha nyama ya nguruwe ipigwe marufuku kwasababu ni harafu, na kuanzishwa mihadhara ya kashfa, kwa wanazuoni wa Kiislamu kuikosoa Biblia na kusema nguruwe hata kwenye Biblia ni Haramu. Vurugu hizo zikapelekea kuvamia mabucha ya nguruwe na kuvunja kisha kukimbilia kujificha misikitini kulikopelekea vurugu za Msikiti wa Mwembechai. Rais Mwinyi akatangaza rukhsa mtu yoyote kula kitu chochote, hakuna ruhusa ya mtu mwingine yeyote kuingilia uhuru wa mtu wa dini nyingine yoyote kula chochote, “Ruksa” na huo ukawa ndio mwanzo wa kuitwa Mzee wa Ruksa, wale wahuni kwa kisingizio cha dini walishughulikiwa kikamilifu, ikiwemo Msikiti wa Mwembechai Kuvamiwa, tena ikatokea mmoja waw ana vuguvugu haw ani mshikaji wangu sana wa sekondari ya Tambaza, Hassan Mkokola.
Baada ya kuzifungulia hizo ruksa, alikuja kufungulia ruksa nyingine nyingi za biashara, Uchumi, akalipindua Azimio la Arusha lililoweka miiko ya uongozi na kuleta Azimio la Zanzibar ambalo liliruhusu viongozi kufanya biashara na kumiliki mali na hapa sasa ndio viongozi wa umma wakaanza kuwa matajiri na kuupindua uchumi wetu kutoka uchumi wa kijamaa na kuingia kwenye uchumi wa kibepari wa nguvu ya soko,
Ruksa nyingine kubwa Rais Mwinyi aliyotuachia ni ruksa ya mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini Tanzia kiasi kwamba sifa ya Baba wa demokrasia Tanzania inamstahili kabisa!, Mwinyi ndie Deng Xioping wetu!.
Japo Rais Mstaafu, Ali Haasan Mwinyi, Mzee wa Rukhsa, ametutoka kwa kutangulia mbele ya haki, huku nyuma rukhsa zake, tutanzienzi milele, na tena sio tuu ametuachia Rukhsa, pia ametuachia na copy pale Zanzibar, cha mtu rahimu kama yeye!, kama vipi 2025, kama Mama ataona ni parefu, hakuna ubaya, akimpisha kale ka Copy kaje huku kutufungulia ruksa nyingine zote zilizobakia!.
Buriani Ali Hassan Mwinyi, Mwendo Umeumaliza.
inna lillahi wa inna ilayhi rajiun (in arabic إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّ إِلَيْهِ رَاجِعُونَ)
Paskali.