Buriani Mzee Ruksa: Ni Deng Xiaoping Wetu wa Mageuzi ya Kiuchumi, Demokrasia, Haki za Binadamu na Uhuru wa Habari. Asante kwa Ruksa Zako, Pumzika!

Buriani Mzee Ruksa: Ni Deng Xiaoping Wetu wa Mageuzi ya Kiuchumi, Demokrasia, Haki za Binadamu na Uhuru wa Habari. Asante kwa Ruksa Zako, Pumzika!

Ni kipindi cha nguo kupigwa viraka,Enzi hizo watu wanavaa nguo imepigwa viraka vya rangi tofauti tofauti

Watu walivaa nguo zilizotoboka ,Ilikuwa hakuna kumshangaa mtu

Wanafunzi wanaenda shule peku peku bila viatu na unawakuta wanakimbia mchaka mchaka kwa uzalendo

Enzi hizo sherehe za Chrismass na Idi zilikuwa sherehe kweli

Watu kabla ya miezi miwili christmass au idd mnaanza kutafuta mchele na kuuhifadhi ndani kwa ajili ya maandalizi ya sherehe,Unaweza enda siku ya sherehe sokoni ukakosa vinywaji na vyakula
Sherehe zikiangukia weekend zinalipiwa siku za kazi. Nchi ilikua ya wote
 
Hakupwaya,
Ni Nyerere ndio alikuwa na wivu, na hakuwa anataka Mwingi afanye vitu bila kumshirikisha, eg Mwinyi alipoamua kukubali mashart ya IMF ikiwemo kudevalue currency hio ilimuuma sana Nyerere, and btw, Nyerere bado alikuwa na wafuasi wengi sanaaaa, so kitendo cha Mwinyi kwenda against sera za Nyerere kilileta maneno mengi sanaaaaa
Stupid comment.

Mwinyi kakabidhiwa nchi noti kubwa ikiwa sh 100. Kashauriwa na bwana zake kuwa suluhisho ni kuchapisha manoti. Matokeo ikawa ni hordes of money chasing too few available goods.

Elimu ya madrasa haiwezi kumkomboa mwanadamu.
 
Stupid comment.

Mwinyi kakabidhiwa nchi noti kubwa ikiwa sh 100. Kashauriwa na bwana zake kuwa suluhisho ni kuchapisha manoti. Matokeo ikawa ni hordes of money chasing too few available goods.

Elimu ya mafrasa haiwezi kumkomboa mwanadamu.
Wew ndo hujui uchumi, unadhani Nyerere alikuwa lofa kuamua kukimbia ? Nyerere alidhibit biashara ya fedha ndio mana thamani ya pesa yetu ikaonekana ipo vema, ila Mwiny akaruhusi iamuliwe na soko huru ndo mana ikashuka sana,

Halafu thamani ya pesa sip big deal kiviiile, sh 1 ya kenya ni sawa na 10 south korean won,
Ila unajua nani ana uchumi mkubwa,
South Africa ana pesa yenye thamani kubwa sana kuliko Japan, ila wote tunajua nani tajiri,
 
Stupid comment.

Mwinyi kakabidhiwa nchi noti kubwa ikiwa sh 100. Kashauriwa na bwana zake kuwa suluhisho ni kuchapisha manoti. Matokeo ikawa ni hordes of money chasing too few available goods.

Elimu ya madrasa haiwezi kumkomboa mwanadamu.
Nimeandika weeee nikafuta. Ila ubaguzi wa dini sio mzuri.
Pia sikiliza watu wanavoelezea CV ya mtu hatakama kuna mapungufu ila alikua na dhamira njema,alitumikia watu katika kipindi kigumu
 
Wew ndo hujui uchumi, unadhani Nyerere alikuwa lofa kuamua kukimbia ? Nyerere alidhibit biashara ya fedha ndio mana thamani ya pesa yetu ikaonekana ipo vema, ila Mwiny akaruhusi iamuliwe na soko huru ndo mana ikashuka sana,

Halafu thamani ya pesa sip big deal kiviiile, sh 1 ya kenya ni sawa na 10 south korean won,
Ila unajua nani ana uchumi mkubwa,
South Africa ana pesa yenye thamani kubwa sana kuliko Japan, ila wote tunajua nani tajiri,
What's your level of education!
 
Siku ya leo, tunampunzisha Mzee wetu, Rais Mtaafu wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi, kwa jina maarufu la Mzee Rukhsa, kwenye nyumba yake ya milele.

Kwa mara ya kwanza Jina la Ali Hassan Mwinyi, nililisikia mwaka 1977, wakati huo akiwa ni Waziri wa Mambo ya Ndani wa serikali ya Nyerere, alipolazimika kujiuzulu kutoka na kashfa ya vifo vya watuhumiwa wawili wa mauaji ya vikongwe, huko Mwanza mwaka 1976.

Mwinyi hakuwa peke yake, bali Makamo wa pili wa Rais na Waziri Mkuu, Rashidi Mfaume Kawawa, pia aliondolewa, Waziri wa Ofisi ya Rais, anyeshughulikia Usalama wa Taifa, Peter Siyovelwa aliondolewa, wakafutiwa na watendaji wakuu wa vyombo vya usalama Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Emelio Mzena, akastaafishwa kwa manufaa ya umma, Mkuu wa Polisi, IGP Swamweli Pundugu akastaafishwa kwa manufaa ya umma.

Baada ya Baba wa Taifa kuwafagia kule juu, fagio la chuma, likatua Mwanza, Mkuu wa Mkoa Peter Kisumo, akaenda na maji, RPC wa Mwanza, RSO, OCD, na DSO wa Mwanza, wakafutwa kazi na kushitakiwa kwenye kesi maarufu ya Mauaji Mwanza yam waka 1976. Mtu pekee aliyesalimika kati ya hao washtakiwa ni mtu mmoja tuu, aliyeitwa Andrew Mayalla, na salama yake, mdogo wake anayetwa Mathew Kasanga, kumuwekea wakili mahiri Murtaza Lakha, kumtetea kaka yake, lakini wengine wote walikula mvua za kutosha!.

Tukio hilo lilileta mageuzi makubwa nchini mwetu, kwanza Idara ya Usalama wa Taifa, ilifumuliwa na kusukwa upya kwa kufanyiwa mabadiliko makubwa, ikaletwa sheria ya usalama wa Taifa, ya 1976, Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 na katiba mpya ya mwaka 1977.

Jina la Ali Hassan Mwinyi, nikaja kukutana nalo tena shule ya msingi, tukisoma na mtoto wake Hussen Mwinyi (Dr)aliyenitangulia madarasa mawili. Baada ya ya shule ya Msingi nikajiunga shule ya sekondari ya Tambaza, ile mwaka 1985 Rais Mwinyi anakuwa Rais wa Tanzania, yule mtoto wake Hussein Mwinyi alikuwa anasoma PCB Tambaza!, kitendo cha mtoto wa rais kusoma shule moja, halikuwa jambo dogo, sasa ndio nikazidi kumfahamu Ali Hassan Mwinyi kwa karibu, wakati hapo Tambaza pia tuko na mtoto wa Nyerere na Mtoto wa Mkapa, darasa moja.

Mwanzo wa Mwinyi Kutwa Mzee Ruksa.

Wakati Mwinyi anachukua urais ile 1985, hali yetu ya Uchumi ili dhollfu bin taaban, baada ya vitavya Kager ana Mwalimu Nyerere kutangaza miezi 18 ya kufunga mikanda, mambo kiukweli yalikuwa magumu, tumekula unga wa Yanga, kutoka Marekani ambao kule kwao ni chakula cha mifugo!, Watu wamevaa magunia, sandarusi hadi sisi wanafunzi nchi nzima tumevaa uniforma ya kitambaa cha madurufu, ambacho nip amba chafu ya kutupa!.

Mahitaji muhimu yote ni kwa resheni kupitia maduka ya kaya, tulikuwa tunapanga foleni siku nzima kusubiria kuuziwa kilo mbili mbili za sukari, hivyo Watoto wote mnatumwa, ili kuwahi foleni, watu walidamka asubuhi na kupanga mawe, gari linaweza kuja saa 10 jioni au siku nyingine kutoka bila bila, haliji kabisa.

Nchi za mabeberu zilimpa Mwalimu Nyerere masherti magumu ya kutupa misaada, ndipo Mwalimu akaamua kuliko kugeuka nyuma akageuka jiwe la chumvi, bora aachie ngazi, kwa mtindo wa kung’atuka na kumpisha Mwinyi. Hivyo Mwinyi aliipokea nchi ikiwa kwenye dhiki kubwa.

Baada ya ya kuingia rais Muislamu, kukaibuka vikundi vya Waislamu wa siasa kali, kwanza waligomea Nguruwe wasichinjiwe mahali panoja, na nyama ya nguruwe isiuzwe bucha zile zile za nyama ya kawaida.

Vikundi hivyo vikaleta vurugu za kulazimisha nyama ya nguruwe ipigwe marufuku kwasababu ni harafu, na kuanzishwa mihadhara ya kashfa, kwa wanazuoni wa Kiislamu kuikosoa Biblia na kusema nguruwe hata kwenye Biblia ni Haramu. Vurugu hizo zikapelekea kuvamia mabucha ya nguruwe na kuvunja kisha kukimbilia kujificha misikitini kulikopelekea vurugu za Msikiti wa Mwembechai. Rais Mwinyi akatangaza rukhsa mtu yoyote kula kitu chochote, hakuna ruhusa ya mtu mwingine yeyote kuingilia uhuru wa mtu wa dini nyingine yoyote kula chochote, “Ruksa” na huo ukawa ndio mwanzo wa kuitwa Mzee wa Ruksa, wale wahuni kwa kisingizio cha dini walishughulikiwa kikamilifu, ikiwemo Msikiti wa Mwembechai Kuvamiwa, tena ikatokea mmoja waw ana vuguvugu haw ani mshikaji wangu sana wa sekondari ya Tambaza, Hassan Mkokola.

Baada ya kuzifungulia hizo ruksa, alikuja kufungulia ruksa nyingine nyingi za biashara, Uchumi, akalipindua Azimio la Arusha lililoweka miiko ya uongozi na kuleta Azimio la Zanzibar ambalo liliruhusu viongozi kufanya biashara na kumiliki mali na hapa sasa ndio viongozi wa umma wakaanza kuwa matajiri na kuupindua uchumi wetu kutoka uchumi wa kijamaa na kuingia kwenye uchumi wa kibepari wa nguvu ya soko,

Ruksa nyingine kubwa Rais Mwinyi aliyotuachia ni ruksa ya mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini Tanzia kiasi kwamba sifa ya Baba wa demokrasia Tanzania inamstahili kabisa!, Mwinyi ndie Deng Xioping wetu!.

Japo Rais Mstaafu, Ali Haasan Mwinyi, Mzee wa Rukhsa, ametutoka kwa kutangulia mbele ya haki, huku nyuma rukhsa zake, tutanzienzi milele, na tena sio tuu ametuachia Rukhsa, pia ametuachia na copy pale Zanzibar, cha mtu rahimu kama yeye!, kama vipi 2025, kama Mama ataona ni parefu, hakuna ubaya, akimpisha kale ka Copy kaje huku kutufungulia ruksa nyingine zote zilizobakia!.

Buriani Ali Hassan Mwinyi, Mwendo Umeumaliza.

inna lillahi wa inna ilayhi rajiun (in arabic إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّ إِلَيْهِ رَاجِعُونَ‎)

Paskali.
Naunga mkono joja zote 2025 pia naunga mkono sana nimeongea sana juu hili...muda tu utaamua saa 100 ampishe copy apige yetu 10 saafii...tugange yajayo
 
Stupid comment.

Mwinyi kakabidhiwa nchi noti kubwa ikiwa sh 100. Kashauriwa na bwana zake kuwa suluhisho ni kuchapisha manoti. Matokeo ikawa ni hordes of money chasing too few available goods.

Elimu ya madrasa haiwezi kumkomboa mwanadamu.
Huna akili kwa hiyo ww kwako ufahari wako ni kuwa na noti ya sh 100 na 50 na sio ubora wa maisha ya watu?
Yaani Nyerere aliye wafanya watu wavae uchi ,wakose mpaka mahitaji muhimu kama sabuni,haka kumiliki redio ilikuwa ni anasa ndo bora ,kuliko mwinyi aliye kuja kufuta huo upuuzi?

Sasa kati ya ww unaye amini ya kuwa nchi ikiwa na noti yenye 0 chache ndo maendeleo na Mwinyi ni nani kilaza?

Pesa ya Kuwait na Oman ina thamani zaidi ya mara 3 ya $ya kimarekani ,sasa hivi ukiwekewa $ na pesa ya hizo nchi utachagua kipi?

Pesa ya Kenya ina thamani kuliko pesa ya Korea na Japan ,haya tuambie maendeleo ya Kenya na hizo nchi yakoje?
Pesa ya Tz ina thamani zaidi ya mara 4 ya pesa ya Iran vipi kuhusu maendeleo kati ya nchi hizo mbili?

Zambia hapo si wana noti ya 100 wana nn cha maana zaidi ya njaa?
 
Pesa ya Kenya ina thamani kuliko pesa ya Korea na Japan ,haya tuambie maendeleo ya Kenya na hizo nchi yakoje?
Pesa ya Tz ina thamani zaidi ya mara 4 ya pesa ya Iran vipi kuhusu maendeleo kati ya nchi hizo mbili?
Pesa as you know it, is just a means of storing and measurung the value of wealth. If you have no wealth, printed money will have no value to you.

Elimu ya madrasa haiwezi kukusaidia kulifahamu hili.
 
Kwenye ishu ya kuvamia msikiti wa Mwembechai umechanganya madafu. Ishu ya msikiti wa Mwembechai ilikuwa ni mwaka 1998 wakati wa utawala wa Mkapa na mkuu wa mkoa akiwa ni Yusufu Makamba.

Mihadhara ya Biblia na Qur'an siyo kashfa bali wakati huo wakati inaanza kwa sababu ilikuwa ni kitu kipya ilidhaniwa hivyo. Lakini siku hizi inafanyika sana tu na inapata vibali vyote vya serikali.

Mtu wa kwanza kufanya mhadhara wa kuchambua biblia na Qur'an hapa Tanzania ni Sheikh Ahmed Deedat kutoka South Africa, aliyekuja nchini na akafanya mdahalo mkubwa hapo Diamond Jubilee mwaka 1980, Rais wa wakati huo akiwa ni Nyerere.

By the way, Katiba inaruhusu mtu kuchambua kitabu chochote kile iwe ni kwa siri au dhahiri ilimradi usivunje sheria!. Hakuna sheria nchini inayokataza Qur'an au biblia kuchambuliwa na yeyote yule ndiyo maana Dibagula alishinda kesi aliposhitakiwa kwa kusema kuwa Yesu siyo Mungu.

Get your facts correct bro.
 
Pesa as you know it, is just a means of storing and measurung the value of wealth. If you have no wealth, printed money will have no value to you.

Elimu ya madrasa haiwezi kukusaidia kulifahamu hili.
Hiyo elimu ya madrasa ndo ilikuja kuwafanya watz akiwemo ww na ukoo wako mzima waache kuvaa viraka,kuogea majani ya mapapai baada ya sabuni, na kupanga misitari kununua sukari na chumvi.

Na ndo iliyo kufanya mpaka sasa una uhuru wa mali yako unayo imiliki.
Kitu ambacho elimu ya kanisa ilishindwa kukifanya kwa miaka 25 hivyo punguza undina na kuwashwa.
Ujamaa ni mfumo wa kipumbavu.
 
Back
Top Bottom