Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
BURIANI RAFIKI YANGU WAZIRI ''MAESTRO'' ALLY
Hakika sisi ni wa Allah na kwake ni marejeo yetu.
Kifo hakizoeleki hata kidogo.
Nimepokea taarifa ya kifo cha rafiki yangu Waziri kwa mshtuko mkubwa.
Nimejuana na Waziri mwaka wa 1979 wakati huo mimi mwanafunzi Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
Waziri, Mohamed Mrisho, Mabruk, Hemed Chuki, Said Lunje walikuwa na bendi yao, ''The Revolution,'' walikuwa wamekuja Dar es Salaam na wakipiga Kilimanjaro, Simba Grill.
Vijana wengi kutoka Tanga tuliokuwa sote pale chuoni walikuwa hawakosi Simba Grill siku za Jumamosi.
Nikipenda muziki toka utoto wangu na nilijifunza kupiga guitar mapema sana na hapo chuoni nilikuwa na ''stereo system'' chumbani kwangu na ''collection,'' kubwa ya muziki wa jazz.
Nadhani ni hawa vijana kutoka Tanga ndiyo waliniunganisha na Waziri na akawa ananitembelea chumbani kwangu kusikiliza muziki niliokuwanao.
Vijana wengi niliokuwanao pale chuoni walikuwa hawaelewi ule mziki kwao kilikuwa kitu kigeni sana.
Wapigaji wa jazz kama George Benson, Earl Klugh, Bob James, Groover Washington, Jimmy Smith, Wes Montgomery yalikuwa majina hawakupata kuyasikia hata siku moja maishani mwao.
Waziri na Mohamed wao walishangazwa na ule mkusanyiko wa muziki ule niliokuwanao katika maktaba yangu.
Ikawa kila wakipata nafasi watapita kunijulia hali na tutasikiliza jazz pamoja na kuzungumza.
Sikupata kufika Simba Grill ila siku moja walipiga Dar es Salaam Institute nikaenda kuwasikiliza.
Hakika upigaji wao ulinichukua sana hasa walipokuwa wanapiga jazz.
Nilikuwa nasikiliza Waziri alivyokuwa akipiga ''keybaord,'' akimuiga Bob James na Mohamed akipiga guitar lake kama Earle Klugg mwenyewe.
Hivi ndivyo nilivyojuana na Waziri Ally na nikawa nampa kila jina la wapiga ''keyboard'' maarufu katika ulimwengu wa jazz lakini kila nilipomwandika niliweka ''Mestro,'' katikati ya majina yake mawili nikimaananisha, ''Bingwa wa Mabingwa.''
Kuna picha nilimpiga Waziri na Mohamed Tanga kwenye sherehe Yanga Bwanga mchezaji mpira maarufu wa Coastal Union na Yanga alipokuwa anamuozesha bint yake miaka 10 iliyopita.
Hii ni moja ya picha zangu ninazozipenda sana.
Siku ile tulipokutana ilikuwa mi miaka mingi sijatiana machoni na hawa marafiki zangu kwani nilikuwa nimehama
Dar es Salaam niko Tanga kwa miaka mingi.
Ilikuwa furaha kubwa sana kwetu sote.
Ndipo nikawaomba niwapige picha hiyo.
Mwaka wa 1984 nilikuwa nakaa Hotel 77 na The Kilimanjaro walikuwa ''Resident Band,'' pale hotelini wakipiga
wakati wa chakula cha jioni.
Huu mwaka naukumbuka kwani wakati Aboud Jumbe anajiuzulu nafasi zake zote katika CCM taarifa hizi nilizipata pale Hotel 77 asubuhi kwenye Daily News.
Ukurasa wa mbele kulikuwa na picha inamuonyesha Waziri Mkuu Edward Sokoine akimsindikiza Aboud Jumbe kuingia ndani ya Mercedes Benz.
Picha hii imenikaa sana katika kichwa changu hadi leo ingawa sijapata kuiona tena popote pale.
Watu wengi walikuwa wanakuja pale hotelini jioni kula ''diner,'' na kusikiliza muziki wao.
Nilikuwa sikosekani hapo.
The Revolutions walikuwa wakikaa hapo hoteni pia basi mimi nilipata fursa kubwa sana ya kujuananao kwa karibu.
Nakumbuka walikuwa ''weekend,'' moja wanakwenda Ngorongoro Lodge kufanya onyesho na wakanikaribisha tufuatane.
Hivi ndivyo nikaweza kujenga usuhuba mkubwa baina yangu na Waziri, Mohamed, Said, Hemed Chuki na Mabruki ambao hawa wawili walishatangulia mbele ya haki.
Walikuwa wakifanya mazoezi pale hotelini mimi nitatoka chumbani kwangu kwenda kuwasikiliza na walifurahi kwa kuona, ''how I was into their music.''
Siku moja walikuwa wamemaliza ''rehersals,'' Mohamed akaweka guitar lake chini.
Mimi nikalinyanyua bila ya hata kuomba nikavaa mkanda wa guitar.
Wote wakawa wananiangalia kwa mshangao.
Huyu anataka kufanya nini?
Kweli nilikuwa napenda muziki lakini kupiga ala...
Vidole vyangu moja kwa moja vikaenda kwenye E Minor, C Major...
Napiga ''Summer Time,'' version ya Sam Cooke.
Wote walikuwa kimya wakisikiliza.
Sikwenda mbali sana.
Nililivua guitar nikaliweka chini.
Mohamed kwa mshangao akaniuliza, ''Mohamed wewe unajua kupiga guitar!''
Nilirudi kutoka Uingereza na keyboard sasa siku hiyo nikakutana na Waziri Mtaa wa Jamhuri na Mosque hii ni sehemu vijana wa Tanga wakipenda sana kukutana kwa ndugu yao Seif Fundi.
Baada ya kuulizana habari za kupoteana nikamwambia Waziri kuwa nilikuwa Uingereza na nimerudi na keyboard.
Waziri kama ''professional musician,'' akataka kujua nimenunua aina gani ya keyboard.
''Casio,''nikamjibu.
Waziri alikunja uso kisha akacheka.
''Sidney, hiyo ni keybord ya watoto wadogo.
Ungenunua Fender, Yamaha au Korg.''
Nilijiona kichekesho mbele ya Maestro.
Nilikuwa sishi kumchokoza Waziri nikimwimbia, ''A Whiter Shade of Pale,'' ya Procol Harum nyimbo ambayo ina ''keyboard'' kali sana nikimwambia nataka siku moja niimbe na yeye anipigie keyboard.
Siku zote akiishia kucheka tu.
Waziri na Mohamed nilikuwa najua kwa kukaa nao walikuwa wanaipenda sana ''Autumn Leaves,'' ya Nat King Cole kwani walikuwa wakiipiga vizuri sana na nikawa naiimba mbele yao kuwachokoza.
Wataishia kutingisha kichwa na kucheka kwani walikuwa wanajua wazi kuwa ujasiri wa kupanda kwenye jukwaa sikuwanao.
Mwaka jana Vuli Yeni alikuja Dar es Salaam akitokea Johannesubrg kwao baada ya miaka 40.
Vuli tumekuwa sote Dar es Salaam ya 1960 wakati wazazi wake wako Tanzania wakati wa kupigania uhuru wa Afrika ya Kusini.
Naamini si wengi wanaonisoma hapa wanamfahamu lakini waingie YouTube watamuona.
Naweka hapa picha tulizopiga Waziri, Vuli na mimi tukiwa Chef Pride, Chagga Street jioni moja mwaka wa 2020.
Ni kama jana tu.
Ilikuwa tarehe 12 December.
Buriani rafiki yangu Waziri ''Maestro'' Ally.
Allah amsamehe madhambi mja wake huyu na amuweke mahali pema peponi.
Amin.