Buriani Rashid Mbuguni, Mzalendo aliyedhulumiwa kiwanda amekufa hajaona haki

Mtetee, na hizo hela kuziweka ktk account binafsi je, inamaanisha nini?

Hahah mbona unanichekesha!! Kwaiyo nani kaziweka!! Na kwanini!!yani ilo ni swali la kuniuliza mimi!! Mnachezewa akili na nyinyi mnajaa tuu kwa chuki binafsi.

*kuhusu izo pesa na upotevu wa mali yapaswa mumulize raisi aliyepo madarakani ndo atumbie zilikwenda wapi sababu aliyekufa ni mtu na sio office, wahusika wote wapo sa kwanini wajifanye hawajui kitu then dhambi wamtupie hayati je angekuepo wangehoji!?, au wangesifia kila kitu[emoji16]. #usiaminisiasa
 
Mama mpenda haki alikuwa wapi kumrudishia kiwanda mpaka anakufa? Magufuli toka kufariki kwake mpaka leo hii aliondoka na mafaili ya kiwanda.. huu ujinga acheni....wao walikopa wakashindwa kurudisha fedha za ECO na NMB, Bank zikashika mali zao leo hii mnamsingizia JPM. Naawambia hata yule mjinga mwingine alidai Mbowe alikamatwa wakati wa JPM (uchawa ni laani mpya)... hata hili la DPW watasema JPM ndio aliwaleta.. takataka wahed.
Pengine hajapelekewa malalamiko, unafikiri huwa anaota usiku kuwa kuna malalamiko?
 
Kwa ufupi, Mengi, E. Massawe, Mbuguni na Nyaulawa walikua National Auditing kwa wakat mmoja na inasemekana utajiri wao waliutoa huko haswa kipindi cha maandalizi ya zoezi la ubinafsishaji.
Hata kama walikwapua mahela ya Taifa ni Bora sababu kwa kiasi kikunwa sana walizirudisha kwa jamii.. Mengi na Hawa kina Nyaulawa wamewezesha vijana wengi, walemavu na wamama.. marakumi Yao kuliko hao wanaokwapua hela na kuzipeleka huko ughaibuni kuzificha.,. Yani hao ni malaika Mungu aliwatuma wake wakomboe taifa

Sent from my TECNO CI6 using JamiiForums mobile app
 
Rashid Mbuguni Afariki Dunia.

Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kuondoka duniani kwa Ndugu Rashid Mbuguni.
Apumzike Kwa Amani.

Maggid

Luqman Maloto anaandika:
Luqman Maloto

“MZALENDO ALIYEDHULUMIWA KIWANDA AMEKUFA HAJAONA HAKI

NAKUMBUKA mwaka 1999. Mara ya kwanza naingia chumba cha habari. Business Times Ltd (BTL).

Newsroom yenye hadhi. Nilivutiwa na chumba kikubwa cha wachoraji. Kizuri sana, kiliundwa kwa vioo. Kila kijana mwenye kipaji cha kuchora, alipaona nyumbani.

BTL, nyumba ya magazeti ya Business Times, Majira, Spoti Starehe, Sanifu, Dar Leo na Maisha. Mamia ya Watanzaia waliajiriwa direct. Maelfu indirect.

Kila kitu kilianza na fikra zilizoishi mbele ya muda, za wazalendo Richard Nyaulawa na Rashidi Mbuguni. Hatimaye, wote sasa ni marehemu.

Nyakati sekta binafsi ikitafsiriwa kuwa mtoto wa haramu, Nyaulawa na Mbuguni walithubutu na waliibeba kwa ujasiri na mawazo yenye ujazo mkubwa.

Kampuni yao, Business Care Limited (BCS), ikazaa BTL, iliyosajili na kuchapa gazeti la kwanza binafsi Tanzania, Business Times. Mwaka 1989.

Wakati wowote, historia ya vyombo vya habari binafsi Tanzania ikiandikwa, majina ya Nyaulawa na Mbuguni, yanastahili wino wa dhahabu.

Gazeti la Business Times, lilizaa Majira mwaka 1992. Baada ya hapo, magazeti zaidi ya kampuni binafsi yalizaliwa, kisha redio na televisheni. BTL ya Nyaulawa na Mbuguni, ilifungua njia.

Nyaulawa na Mbuguni, walianzisha kampuni ya uchapaji ya Business Printers Limited (BPL). Kiwanda cha BPL kilikuza mno tasnia ya habari.

BPL, haikuchapa magazeti ya BTL pekee, bali yote ya kampuni binafsi wakati huo. Vilevile vitabu, majarida na machapisho mbalimbali. Nyaulawa na Mbuguni ni wazazi na walezi wa kila gazeti lililozaliwa miaka ya 1990.

Uchaguzi Mkuu 1995, Nyaulawa na Mbuguni, waliandaa mdahalo wa kihistoria wa wagombea urais. Tukio hilo halijawahi kujirudia nchini.

Nyaulawa na Mbuguni ni Watanzania wa kwanza kuonesha kuwa sekta binafsi inaweza kushirikiana na Serikali, kutatua changamoto za wananchi.

Kupitia BCS, walianzisha miradi ya kushughulikia kero za maji, mikoa mbalimbali nchini. Baadaye, kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Sweden (Sida), Nyaulawa na Mbuguni, waliendesha Mpango wa Afya kupitia Maji Salama (Hesawa) kwa zaidi ya miaka 10.

Kupitia Hesawa, Nyaulawa na Mbuguni, waliwezesha Watanzania zaidi ya milioni tano wa vijijini, hususan Kanda ya Ziwa, kupata maji safi na salama.

Nyaulawa na Mbuguni, walijenga hamasa ya mtaji kwa Watanzania, na wakashawishi wachache kutoka nje, wakaanzisha Benki ya Biashara ya Akiba – Akiba Commercial Bank (ACB), mwaka 1997.

Desemba 1998, Nyaulawa na Mbuguni, walifanikisha kuileta Tanzania, taasisi ya kimataifa ya Junior Achievement Worldwide, yenye makao yake makuu, Colorado, Marekani.

Junior Achievement (AJ), hufundisha vijana elimu ya biashara na uwekezaji. Tangu kuwasili Tanzania, AJ imetengeneza maelfu ya vijana kuwa wafanyabiashara stadi.

Vicoba ni maarufu hivi sasa. Asili yake ni Vibindo. Nyaulawa na Mbuguni, walianzisha Vibindo mwaka 2002, kuwezesha Watanzania kuweka, kukopa na kusaidiana katika vikundi. Vibindo ndio sasa Vicoba.

Nyaulawa na Mbuguni ni waasisi wa Taasisi ya Utafiti na Kuondoa Umaskini (Repoa), ambayo tafiti zake zimekuwa mwanga kwa Serikali, Bunge na taasisi za kimataifa, katika kukabili umaskini Tanzania.

Mwaka 1990, Nyaulawa na Mbuguni, waliratibu mafunzo ya kilimo cha mwani (seaweed) kwa mara ya kwanza, kwa akina mama wa Zanzibar. Wataalamu hao walitoka Ufilipino.

Hivi sasa, mwani inashika nafasi ya tatu Tanzania kwa usafirishwaji nje ya nchi, ni namba tatu kwa mapato Zanzibar, na inachukua hadi asilimia 90 ya huduma za usafiri wa maji Zanzibar kwenda nje.

Nyaulawa na Mbuguni ndio waasisi wa biashara za kutembeza mkononi, yaani umachinga. Waliasisi hilo kupitia kuuza magazeti mikononi. Wakawa na mtandao wa vijana waliozunguka Dar es Salaam. Mtindo huo ukaitikiwa kwa ukubwa. Hivi sasa, mtindo huo umekuwa mtandao mpana wa ajira.

Kwa tafsiri yoyote, Nyaulawa na Mbuguni ni wazalendo wa nchi. Ni nuru ya sekta binafsi. Mageuzi ya ujamaa hadi uchumi wa soko, yana kurasa nyingi za Nyaulawa na Mbuguni. Bila swali, Nyaulawa na Mbuguni ni historia ya Tanzania.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka, amewahi kunieleza kuwa partnership ya Nyaulawa na Mbuguni haina mfanowe Tanzania. Walifanya mengi kibiashara na kwa nchi, kwa upacha wa hali ya juu.

Mzalendo Nyaulawa alifariki dunia mwaka 2008, akamwacha Mzalendo Mbuguni, akiendeleza waliyoyaanzisha pamoja.

Mwaka 2016, BPL chini ya Mbuguni, ilichukua mkopo benki za NMB na ECO. Fedha hizo zilitumika kununua mitambo na kufanya uwekezaji mkubwa kwenye kiwanda chake cha uchapaji. Kiwanda kikawa kipya kabisa.

Mwaka 2017, task force ya Rais wa Tano, Dk John Magufuli, ilivamia BPL. Wamiliki waliondolewa. Kiwanda kikawa chini ya usimamizi wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Kuanzia hapo, magazeti ya CCM, Uhuru, Mzalendo na Burudani, ya Serikali, Daily News, Sunday News na Habari Leo, kwa nyakati tofauti, yalichapwa bure BPL.

Magazeti mengine, Tanzanite, Fahari Yetu, La Jiji, Tanzania Perspective, The Echo, Observer na mengine mengi, yaliyoitwa ya kimkakati, yalichapwa bure BPL.

Kura za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020, zilichapwa BPL.

Wakati yote yakifanyika, Mbuguni na familia ya Nyaulawa, walipitishwa kwenye moto unaounguza. Mali zao, ikiwemo nyumba, kupigwa minada. Presha kubwa ya mikopo ya NMB na ECO.

Haitoshi, task force ya Magufuli, ilimtishia Mbuguni kumfungulia mashitaka ya uhujumu uchumi, vinginevyo alipe mamilioni kwa kushirikiana na familia ya Nyaulawa.

Kwa hofu ya kesi ya uhujumu uchumi, walikubali kulipa kwa awamu. Ajabu, wakaelekezwa kulipa benki kwenye akaunti ya mtu binafsi. Na wakalipa.

Nilimshuhudia Mbuguni akiwa kwenye mahangaiko, akipigania kiwanda chake. Panda shuka bila mafanikio.

Jana, Julai 15, 2023, Mzalendo Mbuguni, aliitikia wa wito wa mauti. Naam, kila nafsi itaonja mauti.

Mbuguni amefariki dunia akiwa bado anasotea haki yake. Kiwanda chake ambacho hakurudishiwa tangu kilipoporwa mwaka 2017.

Mtanzania aliyetenda mengi kwa nchi. Aliyebadili maisha ya maelfu kupitia mipango na ajira za moja kwa moja, nyakati za mwisho za uhai wake, zilijaa maumivu makali kwa sababu ya dhuluma. Amekufa maskini na mufilisi.

Kesho (Julai 17, 2023), Mzalendo Mbuguni atazikwa makaburi ya Kisutu. Sala ya maiti, itafanyika Msikiti wa Maamur, Upanga, Dar es Salaam.

Sisi Sote ni wa Mwenyezi Mungu na Kwake Tutarejea.

Ndimi Luqman MALOTO”
Bado Mtu anasimama kusema Magufuli alikuwa nyenyenye!!
 
Magufuli uendelee kulaanika wewe binafsi watoto wako na mama Janeth hawana hatia ila wewe magufuli KWA uliyoyafanya duniani ulaaniwe milele.
Yaani kati ya mambo yaliyomchafua Magufuli ni pamoja na hiyo yak force yake! Alidhulumu sana watu, inakuwaje unachukua hela za watu unaweka kwenye akaunti binafsi? Hovyo kabisa! Ila nilisikiasikia eti hiyo mitambo ya BTL ilikuwa ya CCM walikodisha hao wamiliki wakawa wamejimilikisha jumla na hawakuwahi kuilipia ndiyo kisa cha kukamatwa!
 
Watu kama mzee Rashid Mbuguni ni hazina ya Taifa, hata kama kafariki ila mchango wake utaendelea kuishi. Kagusa maisha ya watu ambao hata hawamjui na ukute hawatokaa kumjua wala kujua jina lake, a true definition of a Legend
 
Mwendawazimu Jiwe na genge lake walipora na kutumia mitambo ya kampuni yake ya uchapaji
bure kuchapa magazeti yaliyojaa propaganda tu
zile toilet paper za kuchambia za yule taahira Musiba yaani Fahari yetu na Tanzanite zilikua project bubu za jiwe kujipa maujiko!

R.I.P Mbuguni

Root in hell jiwe!
 
Mkuu mimi pana mtoto mdogo nashuka Kilimanjaro Airport alitaka kunisumbua eti anauliza mbona nasafiri mara kwa mara alikua uhamiaji nilimuuliza hizi passport mnatoa za nini na pia hayo maswali huwezi kuniuliza wewe mtoto mdogo miaka naanza kusafiri hata shule haujaanza alikua na vinyotanyota vyake eti atanionyesha nilimwambia na wiki ijayo nasafiri njoo unizuie kila mjinga alijifanya anaweza kufanya kitu chochote kwa cheo chake nilimkariri yule dogo baadae kidogo mzee alivyofariki sikumuona pale nilisikia alikua ndio risasi kidole wao ili mambo ya Bank yanaanzia kwake kwa wasafiri niliumia sana aisee ila sijakaona tena kale kapuuzi nikikaulizia sipati majibu kapo wapi?..
Ungemuuliza tu, kwani kusafiri mara kwa mara ni kosa?
 
Logical non sequitur it doesn’t work here,
Siwezi kujibu vile unavyotaka kama hatujameet kwenye point ya makubaliano ya kuweka kosa la uyo hayati bayana.

Sijatetea nimejaribu kuelabolate tukio na chanzo chake openly kwa mfano hai ili na wewe unipe deep data za chanzo cha hayati kufanya ivo.

Unaweza kuta hayati na uyo mzee walikua wanapersonal issues, hayati alipopata nasafi akaamua kumkomesha kitu ambacho sio sawa kutumia power ulonayo kwa mambo binafsi, huo ni mfano so wewe inatakiwa ulete chanzo sio unatuonesha tukio af unasema aliamka tuu hasbui kama mtu mwenye majini akafika aka chukua vifaa!!! Hell no,

Lastly, kuhusu kukandamiza vyombo vya habari unahisi ni kosa la hayati!? No, since vyombo vya habari vinaendeshwa kwa sheria na kanuni za nchi that means havipo huru, na ninachojua mimi hakuna uhuru usiokua na mipaka kwaiyo ukinimbia amekandamiza uhuru bado haingii akilini wakati kimsingi huo uhuru wenyewe haupo.

so badala ya kumlaumu mtu ungejikita kuelezea jinsi katiba yetu ilivyombovu hapo ningekuelewa maana yawezekana soon akazaliwa mwingine kama uyo alieondoka na akaja tena kufanya yaleyale alio yafanya mwendazake maana kikatiba anayo mamlaka ya kuamua ivo,

Inshot raisi anauhuru wakukupiga unapomkosea au kusamehe na anaweza tumia kisu,rungu au fimbo so ni mood yake na hekima ndo vitamwongoza akubamize na nini ama akusamehe, kwaiyo mkuu leta chanzo tuongee kama watu wazima.
Una argue kwa "unaweza kuta".

That is uharo. Pure uharo.

Not even solid shit.
 
Mpaka umenichekesha, kwanza jua sina hasira na mtu, na hasa akinizidi nguvu au maarifa hua natuliza akili alafu nangalia jinsi yakucheza nae.

Binafsi yalinikumba mengi tuu hasa swala la machinga walipokua huru lilifanya nkafunga hadi duka maana kodi zilikua juu hasa vitu vya electronics na wakati chinga hawaachi ela tofauti na sisi tulio kwenye mfumo maalum na tunalipa kodi nyingi tuu.

*Ok naomba uniambie kama unadaiwa kod ulitaka na hujaenda kuclear installment zako ulitaka wakuchum ili ukatoe pesa yao!? Na je ushawahi kukaa ukasoma policy za benk unayotunzia pesa ziko?

Mi mpaka sasa nimkwepaji mzuri wa kodi ila nikikamatwa siwezi kulaumu serikali/kiongozi nitajilaumu mwenyewe kwa kushidwa kua smart mpaka nimekamatwa, na huo ndo ukweli mkuu, don’t hate the game hate how you play it.
Huna tofauti na wale wafuasi wa Pastor Mackenzie. Sasa hadi umefunga biashara yako na unaona ni sawa tu una tofauti gani na walioambiwa washinde njaa hadi mauti? Wewe hata haki zako huzipendi.
 
Kimsingi huyo mzee alikuwa Don, kweli Jiwe alikuwa mwehu kabisaaaa, yaani watu wenye akili alikua hataki kabisa kuwasikia na kuwaona, Majira ni moja ya Brand za gazeti ambazo hazitafutika kamwe kwenye tasnia ya Habari, Business Times pia lilikua gazeti mwanana sana kabla hata ya wakina The Guardian na hawa wa agakhan wanaojimwambafai sasahivi. Mwishoni walijaribu pia kuanzisha gazeti la kila siku la Daily Times ikiwa ni mtoto wa business times lakini hawakutoboa, majira likahangaikaaaaa nalo halikutoboa, maisha haya ni magumu sana , media hizo ziliweza kuwapika ma giant wengi sana kwenye tasnia , hata Kipanya masudi alianzia majira na katuni zake, kuna wakongwe kina Karl Lymo, kuna kina Mngazija, kina Maugo etc wote ni product za Business times. Itoshe kusema Bongo Bahati mbaya ndiomaana wengine tukaamua kuwa wabeba boksi tu potelea mbali. R.I.P Mzee Mbuguni.
 
Kabla ya kumuhukumu Magufuli ingekua vizuri Kama tungepata na story za upande wa pili,ili tujuwe Nini zilikua sababu za kutaifishwa kwa hiyo mitambo! Unaweza kuta Mshikaji nae alikuwa fisadi, na ni kawaida sana fisadi kupendwa na Watanzania masikini kisa tu kuna visenti anatoa kwa walala hoi!!
KWA hiyo KWA akili yako unahisi hao waliotaifisha hizo Mali NI Malaika?na pesa wakaagiza zilipwe KWENYE acc binafsi,serikali haikuwa na acc za kuweka pesa za wahujumu uchumi?ikulu NI Mahala patakatifu hatupaswi kupeleka pale MTU tunaemtilia shaka.tuwe Makini sn KWENYE chaguzi zetu
 
Hata kama walikwapua mahela ya Taifa ni Bora sababu kwa kiasi kikunwa sana walizirudisha kwa jamii.. Mengi na Hawa kina Nyaulawa wamewezesha vijana wengi, walemavu na wamama.. marakumi Yao kuliko hao wanaokwapua hela na kuzipeleka huko ughaibuni kuzificha.,. Yani hao ni malaika Mungu aliwatuma wake wakomboe taifa

Sent from my TECNO CI6 using JamiiForums mobile app
Personal nimefanya kazi kwa karibu na Rashid wakat nipo kitengo cha sheria ACB na yeye akiwa director anaewakilisha minority shareholders. Alikua ni mtu mwema sana na alikua ana proffers rastafarian believes japo hakua na rasta
 
Mkuu mimi pana mtoto mdogo nashuka Kilimanjaro Airport alitaka kunisumbua eti anauliza mbona nasafiri mara kwa mara alikua uhamiaji nilimuuliza hizi passport mnatoa za nini na pia hayo maswali huwezi kuniuliza wewe mtoto mdogo miaka naanza kusafiri hata shule haujaanza alikua na vinyotanyota vyake eti atanionyesha nilimwambia na wiki ijayo nasafiri njoo unizuie kila mjinga alijifanya anaweza kufanya kitu chochote kwa cheo chake nilimkariri yule dogo baadae kidogo mzee alivyofariki sikumuona pale nilisikia alikua ndio risasi kidole wao ili mambo ya Bank yanaanzia kwake kwa wasafiri niliumia sana aisee ila sijakaona tena kale kapuuzi nikikaulizia sipati majibu kapo wapi?..
He hivi walikua wanajielewa?!
 
Back
Top Bottom