Buriani Rashid Mbuguni, Mzalendo aliyedhulumiwa kiwanda amekufa hajaona haki

Nilikwambia mzee wako unajua kwanini nyumba zake ziliuzwa umebaki kubwabwaja jibu hilo kwanza.
Bado hujui kuandika sentensi iliyonyooka ya Kiswahili.

Mzee wangu ana nyumba Oysterbay, Mbezi Beach anazo nyumba mbili, nyingine Kigamboni na nyingine Mwanza.

Hajawahi kuuza nyumba yake hata moja, anaongeza nyumba tu.

Nimekwambia wewe hujui kusoma kwa ufahamu.
 
Rashid Mbuguni Afariki Dunia.

Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kuondoka duniani kwa Ndugu Rashid Mbuguni.
Apumzike Kwa Amani.

Maggid

Luqman Maloto anaandika:
Luqman Maloto

“MZALENDO ALIYEDHULUMIWA KIWANDA AMEKUFA HAJAONA HAKI

NAKUMBUKA mwaka 1999. Mara ya kwanza naingia chumba cha habari. Business Times Ltd (BTL).

Newsroom yenye hadhi. Nilivutiwa na chumba kikubwa cha wachoraji. Kizuri sana, kiliundwa kwa vioo. Kila kijana mwenye kipaji cha kuchora, alipaona nyumbani.

BTL, nyumba ya magazeti ya Business Times, Majira, Spoti Starehe, Sanifu, Dar Leo na Maisha. Mamia ya Watanzaia waliajiriwa direct. Maelfu indirect.

Kila kitu kilianza na fikra zilizoishi mbele ya muda, za wazalendo Richard Nyaulawa na Rashidi Mbuguni. Hatimaye, wote sasa ni marehemu.

Nyakati sekta binafsi ikitafsiriwa kuwa mtoto wa haramu, Nyaulawa na Mbuguni walithubutu na waliibeba kwa ujasiri na mawazo yenye ujazo mkubwa.

Kampuni yao, Business Care Limited (BCS), ikazaa BTL, iliyosajili na kuchapa gazeti la kwanza binafsi Tanzania, Business Times. Mwaka 1989.

Wakati wowote, historia ya vyombo vya habari binafsi Tanzania ikiandikwa, majina ya Nyaulawa na Mbuguni, yanastahili wino wa dhahabu.

Gazeti la Business Times, lilizaa Majira mwaka 1992. Baada ya hapo, magazeti zaidi ya kampuni binafsi yalizaliwa, kisha redio na televisheni. BTL ya Nyaulawa na Mbuguni, ilifungua njia.

Nyaulawa na Mbuguni, walianzisha kampuni ya uchapaji ya Business Printers Limited (BPL). Kiwanda cha BPL kilikuza mno tasnia ya habari.

BPL, haikuchapa magazeti ya BTL pekee, bali yote ya kampuni binafsi wakati huo. Vilevile vitabu, majarida na machapisho mbalimbali. Nyaulawa na Mbuguni ni wazazi na walezi wa kila gazeti lililozaliwa miaka ya 1990.

Uchaguzi Mkuu 1995, Nyaulawa na Mbuguni, waliandaa mdahalo wa kihistoria wa wagombea urais. Tukio hilo halijawahi kujirudia nchini.

Nyaulawa na Mbuguni ni Watanzania wa kwanza kuonesha kuwa sekta binafsi inaweza kushirikiana na Serikali, kutatua changamoto za wananchi.

Kupitia BCS, walianzisha miradi ya kushughulikia kero za maji, mikoa mbalimbali nchini. Baadaye, kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Sweden (Sida), Nyaulawa na Mbuguni, waliendesha Mpango wa Afya kupitia Maji Salama (Hesawa) kwa zaidi ya miaka 10.

Kupitia Hesawa, Nyaulawa na Mbuguni, waliwezesha Watanzania zaidi ya milioni tano wa vijijini, hususan Kanda ya Ziwa, kupata maji safi na salama.

Nyaulawa na Mbuguni, walijenga hamasa ya mtaji kwa Watanzania, na wakashawishi wachache kutoka nje, wakaanzisha Benki ya Biashara ya Akiba – Akiba Commercial Bank (ACB), mwaka 1997.

Desemba 1998, Nyaulawa na Mbuguni, walifanikisha kuileta Tanzania, taasisi ya kimataifa ya Junior Achievement Worldwide, yenye makao yake makuu, Colorado, Marekani.

Junior Achievement (AJ), hufundisha vijana elimu ya biashara na uwekezaji. Tangu kuwasili Tanzania, AJ imetengeneza maelfu ya vijana kuwa wafanyabiashara stadi.

Vicoba ni maarufu hivi sasa. Asili yake ni Vibindo. Nyaulawa na Mbuguni, walianzisha Vibindo mwaka 2002, kuwezesha Watanzania kuweka, kukopa na kusaidiana katika vikundi. Vibindo ndio sasa Vicoba.

Nyaulawa na Mbuguni ni waasisi wa Taasisi ya Utafiti na Kuondoa Umaskini (Repoa), ambayo tafiti zake zimekuwa mwanga kwa Serikali, Bunge na taasisi za kimataifa, katika kukabili umaskini Tanzania.

Mwaka 1990, Nyaulawa na Mbuguni, waliratibu mafunzo ya kilimo cha mwani (seaweed) kwa mara ya kwanza, kwa akina mama wa Zanzibar. Wataalamu hao walitoka Ufilipino.

Hivi sasa, mwani inashika nafasi ya tatu Tanzania kwa usafirishwaji nje ya nchi, ni namba tatu kwa mapato Zanzibar, na inachukua hadi asilimia 90 ya huduma za usafiri wa maji Zanzibar kwenda nje.

Nyaulawa na Mbuguni ndio waasisi wa biashara za kutembeza mkononi, yaani umachinga. Waliasisi hilo kupitia kuuza magazeti mikononi. Wakawa na mtandao wa vijana waliozunguka Dar es Salaam. Mtindo huo ukaitikiwa kwa ukubwa. Hivi sasa, mtindo huo umekuwa mtandao mpana wa ajira.

Kwa tafsiri yoyote, Nyaulawa na Mbuguni ni wazalendo wa nchi. Ni nuru ya sekta binafsi. Mageuzi ya ujamaa hadi uchumi wa soko, yana kurasa nyingi za Nyaulawa na Mbuguni. Bila swali, Nyaulawa na Mbuguni ni historia ya Tanzania.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka, amewahi kunieleza kuwa partnership ya Nyaulawa na Mbuguni haina mfanowe Tanzania. Walifanya mengi kibiashara na kwa nchi, kwa upacha wa hali ya juu.

Mzalendo Nyaulawa alifariki dunia mwaka 2008, akamwacha Mzalendo Mbuguni, akiendeleza waliyoyaanzisha pamoja.

Mwaka 2016, BPL chini ya Mbuguni, ilichukua mkopo benki za NMB na ECO. Fedha hizo zilitumika kununua mitambo na kufanya uwekezaji mkubwa kwenye kiwanda chake cha uchapaji. Kiwanda kikawa kipya kabisa.

Mwaka 2017, task force ya Rais wa Tano, Dk John Magufuli, ilivamia BPL. Wamiliki waliondolewa. Kiwanda kikawa chini ya usimamizi wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Kuanzia hapo, magazeti ya CCM, Uhuru, Mzalendo na Burudani, ya Serikali, Daily News, Sunday News na Habari Leo, kwa nyakati tofauti, yalichapwa bure BPL.

Magazeti mengine, Tanzanite, Fahari Yetu, La Jiji, Tanzania Perspective, The Echo, Observer na mengine mengi, yaliyoitwa ya kimkakati, yalichapwa bure BPL.

Kura za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020, zilichapwa BPL.

Wakati yote yakifanyika, Mbuguni na familia ya Nyaulawa, walipitishwa kwenye moto unaounguza. Mali zao, ikiwemo nyumba, kupigwa minada. Presha kubwa ya mikopo ya NMB na ECO.

Haitoshi, task force ya Magufuli, ilimtishia Mbuguni kumfungulia mashitaka ya uhujumu uchumi, vinginevyo alipe mamilioni kwa kushirikiana na familia ya Nyaulawa.

Kwa hofu ya kesi ya uhujumu uchumi, walikubali kulipa kwa awamu. Ajabu, wakaelekezwa kulipa benki kwenye akaunti ya mtu binafsi. Na wakalipa.

Nilimshuhudia Mbuguni akiwa kwenye mahangaiko, akipigania kiwanda chake. Panda shuka bila mafanikio.

Jana, Julai 15, 2023, Mzalendo Mbuguni, aliitikia wa wito wa mauti. Naam, kila nafsi itaonja mauti.

Mbuguni amefariki dunia akiwa bado anasotea haki yake. Kiwanda chake ambacho hakurudishiwa tangu kilipoporwa mwaka 2017.

Mtanzania aliyetenda mengi kwa nchi. Aliyebadili maisha ya maelfu kupitia mipango na ajira za moja kwa moja, nyakati za mwisho za uhai wake, zilijaa maumivu makali kwa sababu ya dhuluma. Amekufa maskini na mufilisi.

Kesho (Julai 17, 2023), Mzalendo Mbuguni atazikwa makaburi ya Kisutu. Sala ya maiti, itafanyika Msikiti wa Maamur, Upanga, Dar es Salaam.

Sisi Sote ni wa Mwenyezi Mungu na Kwake Tutarejea.

Ndimi Luqman MALOTO”
Lile Shetani bora lilikufa; sijui yule hayawani na mkia wake aliwezaje kuvaa sura ya binadamu hata akapenya na kuwa Kiongozi wa Nchi.

Natumaini bado anaungulia makali ya moto kule kuzimu, yule ilitakiwa ahukumiwe asisubirishwe Kiama.
 
Pole kwa Familia ya Mzee Mbuguni kwa Msiba huu na Mwenyezi Mungu aiweke Roho yake mahala pema peponi.

Niliijua Familia ya Marehemu na Familia yao mzima tokea nikiwa bado mdogo miaka ya 80 kuelekea ya 90 wakiwa Kwao Oysterbay nyuma ya Mtaa wa Chole ( Chole Road ) huku Watoto wa Marehemu wakiwa ni Rafiki wakubwa wa Kaka zangu.

Pole nyingi sana pia kwa Binti yake Dada Agha ambaye anamiliki Benz Moja Kali sana ( labda kwa sasa awe ameshaiuza ) kwani alishirikiana vyema nz Marehemu Baba yake huyu Kuiendesha hiyo Kampuni.

Luqman Maloto ni kweli kuwa Marehemu alifilisiwa ila ukisema kuwa Kafa Masikini nakukatalia kwani Marehemu alikuwa ni Mambo Safi Kitambo nikiishi nae Jirani Oysterbay na aliwekeza katika Miradi mingi na Kuwasomesha vyema Watoto wake Wote huku baadhi yao wakiwa Kitengoni jirani na Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay.

Otherwise Hongera mno Luqman Maloto ( Mwanafunzi wangu katika Tasnia ) kwa Uandishi mzuri wenye Mpangilio wa Kitaaluma hasa ambao unamvutia Msomaji yoyote bila Kuchoka au Kumboa vile vile.

Katika Waandishi wa Habari wanaoujua Kuandika vyema, Kuchambua na kuweka Facts vizuri Luqman Maloto hukosi katika Tano Bora yangu na bahati nzuri GENTAMYCINE nimekufundisha Tasnia hii Chuoni ( 2011 - 2012 ) hivyo nakujua Kiuwezo, Kitasnia na Kitabia na sishangai Wewe kuwa Bora na Mahiri hivi Kiuandishi.
Sasa wewe mbona unatumia ID fake au ndo Msomi dizaini ya Propesa Kabudi🤗
 
Kabla ya kumuhukumu Magufuli ingekua vizuri Kama tungepata na story za upande wa pili,ili tujuwe Nini zilikua sababu za kutaifishwa kwa hiyo mitambo! Unaweza kuta Mshikaji nae alikuwa fisadi, na ni kawaida sana fisadi kupendwa na Watanzania masikini kisa tu kuna visenti anatoa kwa walala hoi!!
kwanini upore watu mali zao kienyeji sana badala ya angalau kuwafikisha kisutu na kupiga zile simu za maelekezo alizosema Rostam walau ionekane haki imetendeka
 
Nina uhakiaka kuna jambo lipo nyuma yake...
Kama kuna mdau mwenye taarifa za upande wa pili aziweke hapa.

Nakumbuka kuna wadau walijibinafsishia baadhi ya mali za uma.. jamaa (magu)akafanya kuzirudisha (mfano sakata la Airtel.. hisa za vodacom, kituo cha DTV)
Kulikuwa kuna mengi nyuma yake
kwanini hakutumia njia za kisheria kukamilisha hiyo mipango ?
 
Story ya upande mmoja hii, hata kama Magu alikua konyo ila lazima kuna sababu eidha za kipuuzi au za maana kufanya hivyo.
Hakuna lolote, Shetani Magufuli alifanya vile kwa kusudi la kudhibiti Uhuru wa Habari hakuna kingine; Shetani yule alikuwa mwoga kukosolewa. Ningekuwa na jina baya zaidi ya Shetani ningemwita pumbavu yule
 
Bado hujui kuandika sentensi iliyonyooka ya Kiswahili.

Mzee wangu ana nyumba Oysterbay, Mbezi Beach anazo nyumba mbili, nyingine Kigamboni na nyingine Mwanza.

Hajawahi kuuza nyumba yake hata moja, anaongeza nyumba tu.

Nimekwambia wewe hujui kusoma kwa ufahamu.
Bado unatapatapa
 
He hivi walikua wanajielewa?!
Yaani wao walikua wanamvamia kila mtu sasa wapo wanaokufahamu hawawezi kusema kitu wakiamini wale wametoka daslm kwa hiyo ilikua pia sio salama kwa kazi zao yule dogo nilikua namkubuka nilipopita baadae nikaja kuuliza nikaamniwa alitolewa pale KIA alikua kavu sana..
 
Huna tofauti na wale wafuasi wa Pastor Mackenzie. Sasa hadi umefunga biashara yako na unaona ni sawa tu una tofauti gani na walioambiwa washinde njaa hadi mauti? Wewe hata haki zako huzipendi.

Hata hao machinga saivi wamefunga biashara zao sema kwakua haikuhusu huwezi kuona pain walopitia pia baada ya kupata hope ya muda mfupi, inshot nilifunga biashara nikaanza kuuzia vyombo machinga kwa jumla na nilipata pesa japo sio sana ila maisha yalisonga na nilifix hasara, sina ushabiki na hua napenda kutambua ukweli ilikua wao pia wapate kwa wakati ule huwezi kuforce maisha yawe upande wako tuu kilasiku!! na maisha hayana formla kila wakati na namna yake hupaswi kua solid zaidi unapaswa kua smart tu inatosha
, kuanguka au kuangushw kupo tuu ni swala la kua frex na maisha.

Kwaiyo maisha yako yote utaishi kumtukana mfu kisa kakufirisi!!! Pesa bado ipo kama unamaarifa utaipata tuu bilatabu ila kama ulikua mwizi au ulibahatisha na ukashidwa kujiongeza kweli itakupa shida.
 
Bado unatapatapa
Wewe bado hujui kusoma, umechanganya madesa.

A wise man once told me, don't argue with fools.

Cause people from a distance, can't tell who is who.

I am sending you straight to my ignore list.

I haven't sent someone there in a few weeks now.

From here I will no longer see your posts.
 
Hata hao machinga saivi wamefunga biashara zao sema kwakua haikuhusu huwezi kuona pain walopitia pia baada ya kupata hope ya muda mfupi, inshot nilifunga biashara nikaanza kuuzia vyombo machinga kwa jumla na nilipata pesa japo sio sana ila maisha yalisonga na nilifix hasara, sina ushabiki na hua napenda kutambua ukweli ilikua wao pia wapate kwa wakati ule huwezi kuforce maisha yawe upande wako tuu kilasiku!! na maisha hayana formla kila wakati na namna yake hupaswi kua solid zaidi unapaswa kua smart tu inatosha
, kuanguka au kuangushw kupo tuu ni swala la kua frex na maisha.

Kwaiyo maisha yako yote utaishi kumtukana mfu kisa kakufirisi!!! Pesa bado ipo kama unamaarifa utaipata tuu bilatabu ila kama ulikua mwizi au ulibahatisha na ukashidwa kujiongeza kweli itakupa shida.
Frex = flexible, kakufirisi = kakufilisi. Wewe unaongea uharo mtupu. Mtu aliyekufilisi ukimtukana ni umemsamehe sana. Unaona kufilisiwa ni jambo dogo? Wewe ni mpumbavu wa mwisho.
 
Kabla ya kumuhukumu Magufuli ingekua vizuri Kama tungepata na story za upande wa pili,ili tujuwe Nini zilikua sababu za kutaifishwa kwa hiyo mitambo! Unaweza kuta Mshikaji nae alikuwa fisadi, na ni kawaida sana fisadi kupendwa na Watanzania masikini kisa tu kuna visenti anatoa kwa walala hoi!!
Mzee Mbuguni apumzike kwa amani,Mojawapo ya watu wenye upendo na watenda haki.Mimi binafsi amewahi kuyagusa maisha yangu kwa namna ya pekee.Pole kwa Imma na Agha.
 
Rashid Mbuguni Afariki Dunia.

Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kuondoka duniani kwa Ndugu Rashid Mbuguni.
Apumzike Kwa Amani.

Maggid

Luqman Maloto anaandika:
Luqman Maloto

“MZALENDO ALIYEDHULUMIWA KIWANDA AMEKUFA HAJAONA HAKI

NAKUMBUKA mwaka 1999. Mara ya kwanza naingia chumba cha habari. Business Times Ltd (BTL).

Newsroom yenye hadhi. Nilivutiwa na chumba kikubwa cha wachoraji. Kizuri sana, kiliundwa kwa vioo. Kila kijana mwenye kipaji cha kuchora, alipaona nyumbani.

BTL, nyumba ya magazeti ya Business Times, Majira, Spoti Starehe, Sanifu, Dar Leo na Maisha. Mamia ya Watanzaia waliajiriwa direct. Maelfu indirect.

Kila kitu kilianza na fikra zilizoishi mbele ya muda, za wazalendo Richard Nyaulawa na Rashidi Mbuguni. Hatimaye, wote sasa ni marehemu.

Nyakati sekta binafsi ikitafsiriwa kuwa mtoto wa haramu, Nyaulawa na Mbuguni walithubutu na waliibeba kwa ujasiri na mawazo yenye ujazo mkubwa.

Kampuni yao, Business Care Limited (BCS), ikazaa BTL, iliyosajili na kuchapa gazeti la kwanza binafsi Tanzania, Business Times. Mwaka 1989.

Wakati wowote, historia ya vyombo vya habari binafsi Tanzania ikiandikwa, majina ya Nyaulawa na Mbuguni, yanastahili wino wa dhahabu.

Gazeti la Business Times, lilizaa Majira mwaka 1992. Baada ya hapo, magazeti zaidi ya kampuni binafsi yalizaliwa, kisha redio na televisheni. BTL ya Nyaulawa na Mbuguni, ilifungua njia.

Nyaulawa na Mbuguni, walianzisha kampuni ya uchapaji ya Business Printers Limited (BPL). Kiwanda cha BPL kilikuza mno tasnia ya habari.

BPL, haikuchapa magazeti ya BTL pekee, bali yote ya kampuni binafsi wakati huo. Vilevile vitabu, majarida na machapisho mbalimbali. Nyaulawa na Mbuguni ni wazazi na walezi wa kila gazeti lililozaliwa miaka ya 1990.

Uchaguzi Mkuu 1995, Nyaulawa na Mbuguni, waliandaa mdahalo wa kihistoria wa wagombea urais. Tukio hilo halijawahi kujirudia nchini.

Nyaulawa na Mbuguni ni Watanzania wa kwanza kuonesha kuwa sekta binafsi inaweza kushirikiana na Serikali, kutatua changamoto za wananchi.

Kupitia BCS, walianzisha miradi ya kushughulikia kero za maji, mikoa mbalimbali nchini. Baadaye, kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Sweden (Sida), Nyaulawa na Mbuguni, waliendesha Mpango wa Afya kupitia Maji Salama (Hesawa) kwa zaidi ya miaka 10.

Kupitia Hesawa, Nyaulawa na Mbuguni, waliwezesha Watanzania zaidi ya milioni tano wa vijijini, hususan Kanda ya Ziwa, kupata maji safi na salama.

Nyaulawa na Mbuguni, walijenga hamasa ya mtaji kwa Watanzania, na wakashawishi wachache kutoka nje, wakaanzisha Benki ya Biashara ya Akiba – Akiba Commercial Bank (ACB), mwaka 1997.

Desemba 1998, Nyaulawa na Mbuguni, walifanikisha kuileta Tanzania, taasisi ya kimataifa ya Junior Achievement Worldwide, yenye makao yake makuu, Colorado, Marekani.

Junior Achievement (AJ), hufundisha vijana elimu ya biashara na uwekezaji. Tangu kuwasili Tanzania, AJ imetengeneza maelfu ya vijana kuwa wafanyabiashara stadi.

Vicoba ni maarufu hivi sasa. Asili yake ni Vibindo. Nyaulawa na Mbuguni, walianzisha Vibindo mwaka 2002, kuwezesha Watanzania kuweka, kukopa na kusaidiana katika vikundi. Vibindo ndio sasa Vicoba.

Nyaulawa na Mbuguni ni waasisi wa Taasisi ya Utafiti na Kuondoa Umaskini (Repoa), ambayo tafiti zake zimekuwa mwanga kwa Serikali, Bunge na taasisi za kimataifa, katika kukabili umaskini Tanzania.

Mwaka 1990, Nyaulawa na Mbuguni, waliratibu mafunzo ya kilimo cha mwani (seaweed) kwa mara ya kwanza, kwa akina mama wa Zanzibar. Wataalamu hao walitoka Ufilipino.

Hivi sasa, mwani inashika nafasi ya tatu Tanzania kwa usafirishwaji nje ya nchi, ni namba tatu kwa mapato Zanzibar, na inachukua hadi asilimia 90 ya huduma za usafiri wa maji Zanzibar kwenda nje.

Nyaulawa na Mbuguni ndio waasisi wa biashara za kutembeza mkononi, yaani umachinga. Waliasisi hilo kupitia kuuza magazeti mikononi. Wakawa na mtandao wa vijana waliozunguka Dar es Salaam. Mtindo huo ukaitikiwa kwa ukubwa. Hivi sasa, mtindo huo umekuwa mtandao mpana wa ajira.

Kwa tafsiri yoyote, Nyaulawa na Mbuguni ni wazalendo wa nchi. Ni nuru ya sekta binafsi. Mageuzi ya ujamaa hadi uchumi wa soko, yana kurasa nyingi za Nyaulawa na Mbuguni. Bila swali, Nyaulawa na Mbuguni ni historia ya Tanzania.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka, amewahi kunieleza kuwa partnership ya Nyaulawa na Mbuguni haina mfanowe Tanzania. Walifanya mengi kibiashara na kwa nchi, kwa upacha wa hali ya juu.

Mzalendo Nyaulawa alifariki dunia mwaka 2008, akamwacha Mzalendo Mbuguni, akiendeleza waliyoyaanzisha pamoja.

Mwaka 2016, BPL chini ya Mbuguni, ilichukua mkopo benki za NMB na ECO. Fedha hizo zilitumika kununua mitambo na kufanya uwekezaji mkubwa kwenye kiwanda chake cha uchapaji. Kiwanda kikawa kipya kabisa.

Mwaka 2017, task force ya Rais wa Tano, Dk John Magufuli, ilivamia BPL. Wamiliki waliondolewa. Kiwanda kikawa chini ya usimamizi wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Kuanzia hapo, magazeti ya CCM, Uhuru, Mzalendo na Burudani, ya Serikali, Daily News, Sunday News na Habari Leo, kwa nyakati tofauti, yalichapwa bure BPL.

Magazeti mengine, Tanzanite, Fahari Yetu, La Jiji, Tanzania Perspective, The Echo, Observer na mengine mengi, yaliyoitwa ya kimkakati, yalichapwa bure BPL.

Kura za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020, zilichapwa BPL.

Wakati yote yakifanyika, Mbuguni na familia ya Nyaulawa, walipitishwa kwenye moto unaounguza. Mali zao, ikiwemo nyumba, kupigwa minada. Presha kubwa ya mikopo ya NMB na ECO.

Haitoshi, task force ya Magufuli, ilimtishia Mbuguni kumfungulia mashitaka ya uhujumu uchumi, vinginevyo alipe mamilioni kwa kushirikiana na familia ya Nyaulawa.

Kwa hofu ya kesi ya uhujumu uchumi, walikubali kulipa kwa awamu. Ajabu, wakaelekezwa kulipa benki kwenye akaunti ya mtu binafsi. Na wakalipa.

Nilimshuhudia Mbuguni akiwa kwenye mahangaiko, akipigania kiwanda chake. Panda shuka bila mafanikio.

Jana, Julai 15, 2023, Mzalendo Mbuguni, aliitikia wa wito wa mauti. Naam, kila nafsi itaonja mauti.

Mbuguni amefariki dunia akiwa bado anasotea haki yake. Kiwanda chake ambacho hakurudishiwa tangu kilipoporwa mwaka 2017.

Mtanzania aliyetenda mengi kwa nchi. Aliyebadili maisha ya maelfu kupitia mipango na ajira za moja kwa moja, nyakati za mwisho za uhai wake, zilijaa maumivu makali kwa sababu ya dhuluma. Amekufa maskini na mufilisi.

Kesho (Julai 17, 2023), Mzalendo Mbuguni atazikwa makaburi ya Kisutu. Sala ya maiti, itafanyika Msikiti wa Maamur, Upanga, Dar es Salaam.

Sisi Sote ni wa Mwenyezi Mungu na Kwake Tutarejea.

Ndimi Luqman MALOTO”
Magufuli alikuwa mnyama sana
 
Back
Top Bottom