Burundi yaongeza wanajeshi Kivu Kusini

Burundi yaongeza wanajeshi Kivu Kusini

Nchi ya Burundi, inayohusika na vita vinavyoendelea mashariki mwa Congo, kupitia makubaliano ya ushirikiano kwa mambo ya kisalama, kuanzia Septemba 2023, na hili jambo liliifanya Burundi kuwa mshirika mzuri kikanda. Burundi imeweza kupeleka nchini Congo wanajeshi wapatao elfu 10 kulisaidia jeshi la FARDC kukabiliana na M23, waasi wanaoungwa mkono na Rwanda.

Kwa siku mbili sasa, kikosi cha 22, kinakusanyika mpakani Gatumba, kwa maandalizi ya kuingia Kivu kusini. Hili litafanya vikosi 16 vya jeshi la Burundi kuwa nchini DRC,ambapo inakadiliwa watakuwa kati ya elfu 8 na elfu 10. Wanajeshi hao watakuwa na kazi ya kulinda barabara zinazoingia Bukavu mjini, lengo likiwa kuzuia M23 kuingia mjini humo.

Source RFI/Afrique

Hili linafanyika wakati nchi za SADC zinajiandaa kuondoa wanajeshi wake nchini humo, kuanzia Malawi iliokwishatoa Tangazo, Afrika kusini na yenyewe ilionesha nia ya kuwaondoa wanajeshi wake.
Yaani mpaka madini yaliyoko Congo yatakapokwisha kuchimbwa ndo Banyamulenge na Intarahamwe wataondoka pale Kivu, Goma na Masisi
 
Nchi ya Burundi, inayohusika na vita vinavyoendelea mashariki mwa Congo, kupitia makubaliano ya ushirikiano kwa mambo ya kisalama, kuanzia Septemba 2023, na hili jambo liliifanya Burundi kuwa mshirika mzuri kikanda. Burundi imeweza kupeleka nchini Congo wanajeshi wapatao elfu 10 kulisaidia jeshi la FARDC kukabiliana na M23, waasi wanaoungwa mkono na Rwanda.

Kwa siku mbili sasa, kikosi cha 22, kinakusanyika mpakani Gatumba, kwa maandalizi ya kuingia Kivu kusini. Hili litafanya vikosi 16 vya jeshi la Burundi kuwa nchini DRC,ambapo inakadiliwa watakuwa kati ya elfu 8 na elfu 10. Wanajeshi hao watakuwa na kazi ya kulinda barabara zinazoingia Bukavu mjini, lengo likiwa kuzuia M23 kuingia mjini humo.

Source RFI/Afrique

Hili linafanyika wakati nchi za SADC zinajiandaa kuondoa wanajeshi wake nchini humo, kuanzia Malawi iliokwishatoa Tangazo, Afrika kusini na yenyewe ilionesha nia ya kuwaondoa wanajeshi wake.
Screenshot_20250207-112758.jpg

Hao wanajeshi wa Burundi wapo huko kitambo ila DRC haisemi kwa kuwa wanapigania interests za Wahutu pamoja na waasi wa wa Rwanda waliojificha DRC.
 
Rais wa congo ni kama kiongozi asiyejiamini na jeshi lake,asingeweza kusumbiliwa na kanchi kadogo kama Rwanda,imagine sasa tanzania tunataka eneo congo SI tunalichukua mapema sana kwa udhaifu WA kiongozi wao MPENDWA kuongea bila action
 
Burundi asipoacha kiherehere PK ataipa kichapo direct kutokea Kigali tena mchana kweupe.

30 January 2025​

Giteranyi: Mamlaka za Tanzania ziliharibu madaraja yanayoelekea Burundi kwa ajili ya Usalama​

Mamlaka ya Tanzania iliharibu madaraja yanayotenganisha Tanzania na Burundi siku ya Jumanne. Wakazi wa eneo hilo katika tarafa ya Giteranyi, mkoa wa Muyinga (kaskazini-mashariki mwa Burundi) wanazungumza kuhusu operesheni ambapo watu wenye silaha waliovalia sare za jeshi la Tanzania walishiriki.

HABARI SOS Médias Burundi

Madaraja ambayo yalibomolewa yanaelekea maeneo ya Kabogo na Shoza katika wilaya ya Giteranyi, kwanza.

“Kabla ya kuharibiwa kwa madaraja haya, tuliona mkusanyiko wa vikundi vidogo miongoni mwa watu tuliowaona, kulikuwa na wengi waliokuwa wamevalia sare za jeshi la Tanzania, wakiwa na bunduki,” Burundi iliiambia SOS Médias mkazi wa Kabogo hill. Kulingana naye, shughuli hiyo ilianza mwendo wa saa nane asubuhi.

Kwa upande huu, hakuna kizuizi cha asili kinachotumika kama mpaka kati ya Burundi na Tanzania.

“Hatukuarifiwa kuhusu ubomoaji huu kwa sababu hakuna mtu aliyeidhinishwa kwenda upande wa Tanzania,” alisema afisa mmoja wa eneo hilo aliyechaguliwa huko Shoza.

Utawala wa manispaa unasema umegundua kuwa operesheni hiyo ilichochewa na sababu za kiusalama.

“Mamlaka za Tanzania zinasema kwamba kuja na kuondoka kwa Warundi, hasa wakati wa usiku, kunawatia wasiwasi,” Florida Nduwayezu, msimamizi wa jumuiya ya Giteranyi.

Vyanzo vingine vya ndani vilifichua kuwa hatua hiyo ni matokeo ya ushirikiano fulani kati ya wahalifu wa Burundi na Tanzania.

Kwa mujibu wa vyanzo vilivyo karibu na mamlaka ya Tanzania, operesheni hiyo inapaswa kuendelea hadi maeneo ya Murama na Kobero, mtawalia katika tarafa za Muyinga na Butihinda
1738921085491.png
 
Februari 7, 2025Jean Ntumwa

Rumonge: Mahakama ya (kijeshi military court) imetoa adhabu kali kwa askari waliokataa kwenda kupigana pamoja na FARDC dhidi ya M23.​

Alhamisi hii, wanajeshi 272 wa Burundi waliokataa kwenda kupigana pamoja na FARDC (Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo) dhidi ya M23 waliarifiwa kuhusu hukumu yao. Baadhi walihukumiwa kifungo cha maisha. Wana miezi miwili kukata rufaa dhidi ya uamuzi huu. (SOS Media Burundi)
1738921625546.jpeg

Vipengele hivi vya FDNB (Jeshi la Ulinzi la Taifa la Burundi) viliwekwa katika makundi manne. Kundi la kwanza linajumuisha wanajeshi private na makoplo waliorejea Burundi kwa ndege. Walihukumiwa kifungo cha miaka minne jela.

Kundi la pili linaundwa na makoplo na maafisa wasio na kamisheni NCOs ambao pia walisafirishwa hadi Burundi. Watalazimika kutumikia kifungo cha miaka mitano.

Tatu, kuna wanajeshi vyeo private na koplo waliorudishwa nyumbani kwa boti. Walihukumiwa kifungo cha miaka kumi jela.

Kundi la nne na la mwisho linaundwa na makoplo na maafisa wasio na kamisheni ambao pia walifika Burundi kwa boti. Walihukumiwa kifungo cha maisha.

Ni askari mmoja tu aliyehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela.
Wale wanaohusika wana miezi miwili, kuanzia Februari 6, 2025, kukata rufaa dhidi ya uamuzi huu.

SOS Médias Burundi ilikuwa bado haijawa na idadi ya wanajeshi wanaounda kila kategoria. Wakiwa wamezuiliwa katika magereza matatu, ambayo ni Ruyigi (mashariki), Bururi na Rumonge (kusini-magharibi), wanajeshi 272 wa jeshi la Burundi kwa sasa wamekusanyika katika gereza kuu la Murembwe huko Rumonge ambapo kesi ya rufaa ilifanyika Desemba 2024.

Jeshi la Burundi linashiriki katika vita dhidi ya M23 katika jimbo la Kivu Kaskazini (mashariki mwa Kongo) pamoja na FARDC (Vikosi vya Wanajeshi vya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo) na wanamgambo wa ndani wanaodumishwa na mamlaka ya Kongo, ndani ya mfumo wa ushirikiano wa nchi mbili kati ya serikali ya Burundi na Kongo.

Wanaharakati kadhaa wa Burundi mara nyingi wameshutumu "kujihusisha bila manufaa na hatari kwa wanajeshi wetu katika vita ambavyo havituhusu".

Lakini Rais Evariste Ndayishimiye, kamanda mkuu, amekuwa akihalalisha "ujumbe wa kuokoa", akithibitisha kuwa ni kawaida kwamba wanajeshi wa Burundi wanauawa DRC (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo) "kwa sababu walijiandikisha kwa hilo".
Kundi la M23 ni waasi wa zamani wa Watutsi ambao walichukua silaha tena mwishoni mwa 2021, wakishutumu mamlaka ya Kongo kwa kutoheshimu ahadi zao za kuwajumuisha tena wapiganaji wake. Mamlaka ya Kongo inasalia kushawishika kwamba anafaidika na msaada kutoka Rwanda, jambo ambalo serikali ya Rwanda inaendelea kulipuuza.
________________________________________________
 
Wakiwa wamezuiliwa katika magereza matatu, ambayo ni Ruyigi (mashariki), Bururi na Rumonge (kusini-magharibi), wanajeshi 272 wa jeshi la Burundi kwa sasa wamekusanyika katika gereza kuu la Murembwe huko Rumonge ambapo kesi ya rufaa ilifanyika Desemba 2024.

Intelejensia kali ya TPDF ndiyo maana Tanzania inaangalia mpaka na Burundi kwa macho usiku na mchana, ikiwemo kuvunja vivuko na madaraja ili askari kutoka Burundi wasiingie kwa utoro au operesheni maalum
 
Kwa mujibu wa akili mnemba

Mashambulizi ya waasi wa M23 (Mouvement du 23 Mars) katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) yanachangiwa na sababu kadhaa za kisiasa, kijamii, na kiuchumi. Hapa kuna baadhi ya sababu kuu:

1. Mgogoro wa Kisiasa na Mkataba wa 2009

M23 inadai kuwa serikali ya DRC imeshindwa kutekeleza kikamilifu mkataba wa amani wa 2009, ambao uliahidi kuingiza wapiganaji wa kundi la CNDP (chama kilichotangulia M23) katika jeshi la serikali na kuwapatia nyadhifa serikalini.

2. Mgogoro wa Kabila na Ushawishi wa Rwanda na Uganda

M23 inaundwa hasa na waasi wa kabila la Watutsi, na kuna madai kwamba wanapata msaada kutoka kwa Rwanda na Uganda. Rwanda imekuwa ikituhumiwa kuwaunga mkono waasi ili kulinda maslahi yake, hasa kuzuia mashambulizi ya FDLR (kundi la waasi wa Kihutu) kutoka DRC.

3. Utajiri wa Madini na Rasilimali za Asili

Mashariki mwa DRC ina utajiri mkubwa wa madini kama dhahabu, coltan, na almasi. Kuna madai kuwa waasi wa M23 wanapigania kudhibiti rasilimali hizi ili kujipatia mapato ya kufadhili harakati zao.

4. Udhaifu wa Serikali ya DRC na Jeshi

Jeshi la DRC (FARDC) limekuwa likikabiliwa na changamoto za uongozi, ufisadi, na ukosefu wa vifaa vya kisasa, jambo linalofanya iwe rahisi kwa makundi ya waasi kushambulia na kuteka maeneo.

5. Ukosefu wa Amani na Mazungumzo

Juhudi za kidiplomasia, ikiwemo majadiliano chini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Umoja wa Mataifa, zimekuwa zikiendelea, lakini bado hazijafanikiwa kumaliza mgogoro huu.

Kwa sasa, mapigano yanaendelea katika maeneo ya Kivu Kaskazini, huku maelfu ya raia wakikimbia makazi yao.

Akili mnemba anaendelea

Ili kumaliza mgogoro wa M23 na kuleta amani ya kudumu katika DRC, kunahitajika suluhisho la kina linaloshughulikia chanzo cha tatizo na siyo tu matokeo yake. Hapa kuna hatua muhimu zinazoweza kusaidia:

1. Mazungumzo ya Kisiasa na Utekelezaji wa Makubaliano

Serikali ya DRC inapaswa kushirikiana na waasi wa M23 kupitia mazungumzo yenye nia ya dhati.

Mkataba wa 2009, ambao M23 wanadai haujatekelezwa, unapaswa kutazamwa upya na kutekelezwa kwa haki.

Ushirikiano wa jumuiya za kikanda kama EAC, AU, na SADC ni muhimu kuhakikisha suluhisho la kisiasa linafanikiwa.

2. Kuzuia Uingiliaji wa Nchi za Nje

Rwanda na Uganda zimeshutumiwa kwa kusaidia M23, hivyo jumuiya za kimataifa zinapaswa kushinikiza nchi hizi kuacha kuingilia mambo ya ndani ya DRC.

Umoja wa Mataifa na AU wanapaswa kusimamia uchunguzi wa kina kuhusu uhusiano wa mataifa haya na waasi.

3. Kuimarisha Jeshi la DRC (FARDC)

Serikali ya DRC inapaswa kuimarisha jeshi lake kwa kuwapa mafunzo bora, vifaa vya kisasa, na kuhakikisha hakuna ufisadi ndani ya mfumo wa ulinzi.

Ushirikiano wa kijeshi na mataifa jirani unaweza kusaidia kuimarisha usalama katika maeneo yaliyoathirika.

4. Kudhibiti Rasilimali za Madini

M23 na makundi mengine ya waasi yanatumia madini kama chanzo cha mapato. Serikali ya DRC inapaswa kuweka mifumo thabiti ya udhibiti wa biashara ya madini ili kuzuia ufadhili wa waasi.

Jumuiya ya kimataifa inapaswa kuweka vikwazo kwa makampuni yanayonunua madini kutoka kwa waasi.

5. Kulinda Raia na Kutoa Misaada kwa Wakimbizi

Maelfu ya raia wamekimbia makazi yao kutokana na mapigano. UNHCR na mashirika mengine ya misaada yanapaswa kusaidia waathiriwa wa mgogoro huu.

Serikali inapaswa kuweka sera za kuwarudisha wakimbizi kwenye makazi yao kwa usalama.

6. Kusimamia Amani kwa Usimamizi wa Kikanda na Kimataifa

Nchi za EAC zinapaswa kuendeleza juhudi za kidiplomasia na kuimarisha kikosi cha kijeshi cha kikanda kilichopelekwa kusaidia hali ya usalama.

Umoja wa Mataifa unapaswa kuongeza ufanisi wa kikosi chake cha MONUSCO ili kiongeze ulinzi kwa raia na kusaidia kurejesha utulivu.

Kwa jumla, suluhisho la mgogoro wa M23 linahitaji mchanganyiko wa diplomasia, uimarishaji wa usalama, na usimamizi bora wa rasilimali.
Sio Kila kitu unamtegemea akili mnba wakati mwingine anakuingiza chaka.
 
Mi nachojiuliza, ulishatangaza kwamba vita vinagonga mlangoni kwako, kwamba baada ya Congo ni wewe. Af wanajeshi kama hao idadi kubwa kihivo, unapeleka nje ya nchi. Ndo maandalizi? ndo nini!
Ramani huijui,hapo bukavu ni karibu na burundi,kuna waasi red tabara wanaosapotiwa na Rwanda dhidi ya burundi,m23 wakichukua bukavu,maana yake red tabara Sooner or later wataingia burundi wakiwa na support kubwa,so unaweka buffer zone,pigana m23 asichukue bukavu, very simple
 
Hivi, kweli inawezekana raisi wa nchi apeleke wanajeshi elfu kumi vitani nchi nyingine? Hapa kuna watu wanaenda kupimana uwezo si bure.
Mbona unashangaa? Kwani mapank alipeleka wanajeshi wangapi kuisaidia Urusi dhidi ya Ukraine?
 
Nchi ya Burundi, inayohusika na vita vinavyoendelea mashariki mwa Congo, kupitia makubaliano ya ushirikiano kwa mambo ya kisalama, kuanzia Septemba 2023, na hili jambo liliifanya Burundi kuwa mshirika mzuri kikanda. Burundi imeweza kupeleka nchini Congo wanajeshi wapatao elfu 10 kulisaidia jeshi la FARDC kukabiliana na M23, waasi wanaoungwa mkono na Rwanda.

Kwa siku mbili sasa, kikosi cha 22, kinakusanyika mpakani Gatumba, kwa maandalizi ya kuingia Kivu kusini. Hili litafanya vikosi 16 vya jeshi la Burundi kuwa nchini DRC,ambapo inakadiliwa watakuwa kati ya elfu 8 na elfu 10. Wanajeshi hao watakuwa na kazi ya kulinda barabara zinazoingia Bukavu mjini, lengo likiwa kuzuia M23 kuingia mjini humo.

Source RFI/Afrique

Hili linafanyika wakati nchi za SADC zinajiandaa kuondoa wanajeshi wake nchini humo, kuanzia Malawi iliokwishatoa Tangazo, Afrika kusini na yenyewe ilionesha nia ya kuwaondoa wanajeshi wake.
Vita vya kikanda vinanukia ...
 
Hata mimi ningekuwa kagame ningesupppport M23. Yani serekali ya Congo haifanyi chochote cha maana kuondoa vikundi vya waasi cha mauaji ya 1994. Anachofanya kagame ndicho ambacho USA amefanya Iraq. Maana ukisema unaacha wanajippanga na kuja kukuondoa, kwa takwimu .....wahutu 80% .... 19% tusti.... kwa sababu Congo wameacha pori wajifiche waasi wa nchi mbalimbali na majambaz sugu . ....
Hata sababu ya GEN IDD AMIN DADA , ilikuwa waasi na wapinzani wake kuishi Tanzania , hakuna nchi safi ......
 
Nchi ya Burundi, inayohusika na vita vinavyoendelea mashariki mwa Congo, kupitia makubaliano ya ushirikiano kwa mambo ya kisalama, kuanzia Septemba 2023, na hili jambo liliifanya Burundi kuwa mshirika mzuri kikanda. Burundi imeweza kupeleka nchini Congo wanajeshi wapatao elfu 10 kulisaidia jeshi la FARDC kukabiliana na M23, waasi wanaoungwa mkono na Rwanda.

Kwa siku mbili sasa, kikosi cha 22, kinakusanyika mpakani Gatumba, kwa maandalizi ya kuingia Kivu kusini. Hili litafanya vikosi 16 vya jeshi la Burundi kuwa nchini DRC,ambapo inakadiliwa watakuwa kati ya elfu 8 na elfu 10. Wanajeshi hao watakuwa na kazi ya kulinda barabara zinazoingia Bukavu mjini, lengo likiwa kuzuia M23 kuingia mjini humo.

Source RFI/Afrique

Hili linafanyika wakati nchi za SADC zinajiandaa kuondoa wanajeshi wake nchini humo, kuanzia Malawi iliokwishatoa Tangazo, Afrika kusini na yenyewe ilionesha nia ya kuwaondoa wanajeshi wake.
Hao maskini wanaacha kujenga Nchi Yao wanahangaika huko DRC.
 
Back
Top Bottom