Burundi yatoa onyo dhidi ya shambulio lolote kutoka Rwanda

Burundi yatoa onyo dhidi ya shambulio lolote kutoka Rwanda

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708
"Tunafahamu Rwanda inajaribu kutuvamia kupitia ardhi ya DRC ili wasingizie kuwa ni waasi wa Red Tabara na M23. Lakini tunawaambia nasi tunaweza kushambulia Kigali"

Burundi imetishia kujibu vikali shambulio au uvamizi wowote utakaotokea nchini humo kutoka Rwanda.

Mahojiano ya kipekee na BBC, Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, amesema kuwa wamepata taarifa za kuaminika kuwa taifa la Rwanda linapanga kuishambulia Burundi.
===
" Tunafahamu Rwanda inajaribu kutuvamia kupitia ardhi ya DRC ili wasingizie kuwa ni waasi wa Red Tabara na M23. Lakini tunawaambia kwamba ikiwa mnaona kushambulia Bujumbura ni karibu kutoka Uvira basi nasi tunaweza kushambulia Kigali kutoka mji wa Kirundo" Alionya Rais Ndayishimiye.

Akiongea na BBC, Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, amesema kuwa wamepata taarifa za kuaminika kuwa taifa la Rwanda linapanga kuishambulia Burundi.

Hata hivyo serikali ya Rwanda imekanusha vikali madai ya serikali ya Burundi.

''Matamshi ya Burundi ni ya kushangaza kwasababu idara za ulinzi za nchi hizi mbili zimekuwa zikikutana kujadili namna ya kulinda mipaka yao haswa wakati huu kuna mzozo Mashariki mwa DRC,''msemaji wa serikali ya Rwanda Yolanda Makolo aeleza.

Ndayishimiye amesema Rwanda itakuwa imefanya kosa kubwa kuivamia Burundi kwa njia yoyote ile akisema Burundi itajibu kwa njia ya Kijeshi, na hivyo kuonya uwezekano wa kuzuka kwa vita vya kikanda.

Rais huyo wa Burundi amesema pia "hatutakubali kuchinjwa kama mbuzi, kama vile Wakongomani"
Ndayishimiye aliifahamisha BBC kuwa serikali yake tayari imetuma ujumbe kwa rais wa Rwanda Paul Kagame ili mchakato kwa kutekeleza makubaliano yao ya maridhiano ili kupunguza uhasama kati yao.

"Tumefanya mazungumzo na Rwanda kwa muda mrefu na tukakubaliana na ilipofika wakati wa utekelezaji, Rwanda ikasita" aliongeza Rais Ndayishimiye.

Burundi imeishutumu Rwanda kwa kuwapa hifadhi watu wanaoaminika walijaribu kufanya mapinduzi ya serikali nchini Burundi mwaka wa 2015. Aidha Burundi imedai kuwa utawala wa wa Rais Paul Kagame inawapa misaada waasi wa Red Tabara, ambão mara kwa mara hufanya mashambulizi ya kuvizia nchini Burundi kutoka Mashariki mwa DRC .

Amesema Burundi imejiandaa vilivyo kulinda mipaka yake na kamwe haitaruhusu uvamizi wa aina yoyote na kuishutumu, Rwanda kwa kufadhili makundi ya waasi yanayosababisha maafa Mashariki mwa Congo.

Mashambulizi ya hivi karibu kutoka kwa waasi wa Red Tabara, nchini Burundi, yalisababisha nchi hiyo kufunga mipaka yake na Rwanda.
Utawala wa Burundi umesema kuwa mchakata wa kuwakamata na kuwafungulia mashtaka viongozi wa waasi wa Red Tabara unaendelea na kuwa serikali haina nia yoyote ya kufanya mazungumzo nao. Rais Ndayishimiye amesema kuwa jukumu la serikali yake sasa ni kuwasaka waasi hao na kuwafikisha mahakamani.

Rais Ndayishimiye amesema Burundi haina nia yoyote ya kuvamia nchi nyingine au kuingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine na hivyo inastahili kupewa heshima kama hiyo pia.

Chanzo: BBC Swahili
 
Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye ni jenerali. Inasikitisha habari yote hakuna mahali imetaja cheo chake hiko ukizingatia context ya habari yenyewe.

Waandishi wa siku hizi bure kabisa.
Waandishi wa vichochoroni naona hapo kanukuu kwa kuandika "hatutakubali kuchinjwa kama mbuzi, kama vile Wakongomani"

Wakati Video ya mahojiano hakuna mahali kasema hayo maneno ya kuchinjwa kama mbuzi.
 
Taaratibu, unabii wa askofu Christopher Mtikila (RIP ) unataka kutimia. Watutsi wanataka kuanzishwa kwa Bahima empire, wanataka ardhi. Naweza kuhisi hivi, "Kagame anatamani Burundi impate rais Mtutsi na sio Mhutu kama huyu" akifanikiwa kwenye hilo then PK atakua anaziongoza both Congo and Burundi by remote, madini ya Congo yaki finance mipango yake. Tupo tunamwangalia tu PK, PK ni jipu, tuendelee tu kumchekea, siku 1 tutajuta, will be too late
 
Back
Top Bottom