Burundi yatoa onyo dhidi ya shambulio lolote kutoka Rwanda

Burundi yatoa onyo dhidi ya shambulio lolote kutoka Rwanda

KU
PK hatostaafu Urais mpaka ahakikishe keshatwangana na Burundi.

Wakumnusuru Burundi ni baba yake Tanzania tofauti na hapo Burundi watakandwa mpaka wanye.
Kukandwa watakandwa,
Lakini kigali itakua Hovyo pia.

East Africa hapa hakuna mtu mwenye uchumi wa kupigana Vita, hivyo madhara lazima yaonekane tu.

Mfano, sisi tukimchokoza Rwanda tukaanza vita akabomoa bwawa la Nyerere itatuchukua miaka mingapi kulijenga?
 
Ndaishimiye ndio kiboko ya Kagame,kwanza anaongea kwa utulivu na haonyeshi hasira,halafu yeye hamung'unyi maneno,anakwambia Watashambulia Kigali muda wowote wakishambuliwa
 
Mdomo uliponza kichwa kuna kauli hazitakiwi kutolewa na viongozi. Kauli kama hizi ndio zimefanya sasa hivi congo isubiri miujiza.
 
"Tunafahamu Rwanda inajaribu kutuvamia kupitia ardhi ya DRC ili wasingizie kuwa ni waasi wa Red Tabara na M23. Lakini tunawaambia nasi tunaweza kushambulia Kigali"

Burundi imetishia kujibu vikali shambulio au uvamizi wowote utakaotokea nchini humo kutoka Rwanda.

Mahojiano ya kipekee na BBC, Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, amesema kuwa wamepata taarifa za kuaminika kuwa taifa la Rwanda linapanga kuishambulia Burundi.
===
" Tunafahamu Rwanda inajaribu kutuvamia kupitia ardhi ya DRC ili wasingizie kuwa ni waasi wa Red Tabara na M23. Lakini tunawaambia kwamba ikiwa mnaona kushambulia Bujumbura ni karibu kutoka Uvira basi nasi tunaweza kushambulia Kigali kutoka mji wa Kirundo" Alionya Rais Ndayishimiye.

Akiongea na BBC, Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, amesema kuwa wamepata taarifa za kuaminika kuwa taifa la Rwanda linapanga kuishambulia Burundi.

Hata hivyo serikali ya Rwanda imekanusha vikali madai ya serikali ya Burundi.

''Matamshi ya Burundi ni ya kushangaza kwasababu idara za ulinzi za nchi hizi mbili zimekuwa zikikutana kujadili namna ya kulinda mipaka yao haswa wakati huu kuna mzozo Mashariki mwa DRC,''msemaji wa serikali ya Rwanda Yolanda Makolo aeleza.

Ndayishimiye amesema Rwanda itakuwa imefanya kosa kubwa kuivamia Burundi kwa njia yoyote ile akisema Burundi itajibu kwa njia ya Kijeshi, na hivyo kuonya uwezekano wa kuzuka kwa vita vya kikanda.

Rais huyo wa Burundi amesema pia "hatutakubali kuchinjwa kama mbuzi, kama vile Wakongomani"
Ndayishimiye aliifahamisha BBC kuwa serikali yake tayari imetuma ujumbe kwa rais wa Rwanda Paul Kagame ili mchakato kwa kutekeleza makubaliano yao ya maridhiano ili kupunguza uhasama kati yao.

"Tumefanya mazungumzo na Rwanda kwa muda mrefu na tukakubaliana na ilipofika wakati wa utekelezaji, Rwanda ikasita" aliongeza Rais Ndayishimiye.

Burundi imeishutumu Rwanda kwa kuwapa hifadhi watu wanaoaminika walijaribu kufanya mapinduzi ya serikali nchini Burundi mwaka wa 2015. Aidha Burundi imedai kuwa utawala wa wa Rais Paul Kagame inawapa misaada waasi wa Red Tabara, ambão mara kwa mara hufanya mashambulizi ya kuvizia nchini Burundi kutoka Mashariki mwa DRC .

Amesema Burundi imejiandaa vilivyo kulinda mipaka yake na kamwe haitaruhusu uvamizi wa aina yoyote na kuishutumu, Rwanda kwa kufadhili makundi ya waasi yanayosababisha maafa Mashariki mwa Congo.

Mashambulizi ya hivi karibu kutoka kwa waasi wa Red Tabara, nchini Burundi, yalisababisha nchi hiyo kufunga mipaka yake na Rwanda.
Utawala wa Burundi umesema kuwa mchakata wa kuwakamata na kuwafungulia mashtaka viongozi wa waasi wa Red Tabara unaendelea na kuwa serikali haina nia yoyote ya kufanya mazungumzo nao. Rais Ndayishimiye amesema kuwa jukumu la serikali yake sasa ni kuwasaka waasi hao na kuwafikisha mahakamani.

Rais Ndayishimiye amesema Burundi haina nia yoyote ya kuvamia nchi nyingine au kuingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine na hivyo inastahili kupewa heshima kama hiyo pia.

Chanzo: BBC Swahili
Niliishawahi kusema na narudia kusema; Rwanda kwa ujinga ujinga tu akaivamia Burundi, basi ndio utakuwa mwisho wa Utawala wa Kagame na Watutsi nchini Rwanda.
Kwa ambaye haniamini, basi atanikuta nimekaa Mutukula Border nakula gonja!
 
Niliishawahi kusema na narudia kusema; Rwanda kwa ujinga ujinga tu akaivamia Burundi, basi ndio utakuwa mwisho wa Utawala wa Kagame na Watutsi nchini Rwanda.
Kwa ambaye haniamini, basi atanikuta nimekaa Mutukula Border nakula gonja!
Unafikiri vita kati ya Burundi na Rwanda itakuwa kama Congo? Sahau hilo!

Wewe unafikiri PK kwa nini kwa upande wa Burundi njama zake ni mapinduzi na si kuingia naye vita ya moja kwa moja?
 
Mdomo uliponza kichwa kuna kauli hazitakiwi kutolewa na viongozi. Kauli kama hizi ndio zimefanya sasa hivi congo isubiri miujiza.
Vita kati ya Rwanda na Burundi itakuwa ni umwagaji wa damu mkubwa.

Kingine ambacho unachotakiwa kukijua wahutu wapo wengi Rwanda na Burundi kwa idadi ya mmoja mmoja kwa nchi zote mbili.

Vita yao itabeba mengi.
 
Unafikiri vita kati ya Burundi na Rwanda itakuwa kama Congo? Sahau hilo!

Wewe unafikiri PK kwa nini kwa upande wa Burundi njama zake ni mapinduzi na si kuingia naye vita ya moja kwa moja?
Dah! Anyway,ulielewa nilimaanisha nini?
 
Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye ni jenerali. Inasikitisha habari yote hakuna mahali imetaja cheo chake hiko ukizingatia context ya habari yenyewe.

Waandishi wa siku hizi bure kabisa.
Acha uzwazwa wewe mbona Jakaya alikuwa mwanajeshi luteni kanal lakini jina lililotumika ni Rais, Geogre Bush alikuwa na cheo cha Lieutenant lakini hatukuwai kusikia Lieutenant George H.W. Bush.
Kwani usipotaja ndio itakuwa imeharibu maana nzima ya Rais.

Alafu wewe unaonesha unapenda sana misifa.
 
Vita kati ya Rwanda na Burundi itakuwa ni umwagaji wa damu mkubwa.

Kingine ambacho unachotakiwa kukijua wahutu wapo wengi Rwanda na Burundi kwa idadi ya mmoja mmoja kwa nchi zote mbili.

Vita yao itabeba mengi.
Mkuu vita haina macho kiongozi kutoa kauli za kikoro kama hizi haifai kwa sababu mwisho wa siku kikiwaka ataokoa familia yake madhara yatawakuta wananchi. Unadhani hii vita ya congo wanekufa wangapi? Kiongozi wao si huyo kutwa yupo katika ndege kama madhara yangekuwa yanawagusa viongozi moja kwa moja heshima ingekuwepo.
 
Ni kweli amefeli mara kadhaa, JK mwishoni mwa utawala wake, alimshikisha adabu sana tu hadi akawa hana hamu nae BUT I think Mr. Slim hakatagi tamaa akiwa na jambo lake, again I think Watutsi wana vikao vyao vya siri ambavyo wana mambo wamerithishana miaka kadhaa nyuma. Kama kuna mtu kawahi ku date na mabinti wa Kinyarwanda atajua jambo lifuatalo; say mko nae Mbeya au may be Zanzibar (sijaiweka Dar kwasababu Dar ina mwingiliano mkubwa wa makabila yote East and Central Africa ) then akakutana na either mwanaume au mwanamke mwenzie wa Kinyarwanda, huaga wana signal zao wanapeana, Watutsi wazaliwa wa Tanzania au hata nje ya Rwanda, Burundi or Uganda, signal yao ni moja; now the question is, wanafundishanaga wapi kama sio jambo la kurithishana vizazi na vizazi? PK anaweza kujua kwamba hiyo mission yake inaweza isifanikiwe katika utawala wake, but he will never leave the regime to another tribe in that country, next president MUST be a Tutsi cause they know their plan, as for him, he has a job to accomplish and that's what he is doing. Kua nae makini. Anacho kifanya sasa hivi ni kutafuta pesa ili awe imara financially, anafanikiwa sana kupitia madini ya Congo, sisi tunamchekea tu. Si ndio huyu alimuwezesha Kabila Sn ili amtoe Mabutu Seseko madarakani? Lazima kuna vitu walikubaliana, Kabila hakutekeleza, finally he was killed. RIP Christopher Mtikila
ok ngoja tione au tuone lakini ahsante sana CDF Mkunda John Jacob sasa hivi wanaondoka kisirisiri hata yule Balozi wake anahara damu
 
Back
Top Bottom