Bush na Kikwete; Hizi ndio sababu za kupayuka kwetu?

Bush na Kikwete; Hizi ndio sababu za kupayuka kwetu?

Haki.tupu,
Hapo umesema. Salim kwa lugha tu na kufafanua issues kweli tulikuwa na foreign minister. Hata JKN alikuwa akiwatoa vijampo akina Henry Kissinger. Acha bwana. Kuna standard ambayo mbali na Mkapa (ukiweka kando ufisadi) Tanzania ilikuwa imeiweka katika mambo ya foreign relations.

Hapo kwenye Mkapa sikubaliani!
Na pia sikubaliani na watu kuwa viongozi wetu simply kwasababu ya lugha!
Tunataka MISIMAMO ISIYOYUMBA!
Hiyo inatutosha especially if misimamo hiyo ni kwa maslahi ya Mnyonge na masikini!
 
Wadanganyika,
Hebu tuendeleee kuangalia yale yanayomfanya JK kuchukua misimamo ya ajabu ajabu kwenye masuala ya Africa.

Statement by President Bush and President Kikwete of Tanzania after G8

PRESIDENT BUSH: I'm really pleased to be standing with a really good friend of the American people and a great leader in Africa, President Kikwete of Tanzania. I just -- first of all, I'd like to announce that he's coming to visit in late August. I'm really looking forward to having you to the White House; looking forward to giving you a good dinner. And we'll have a good visit.

PRESIDENT KIKWETE: Looking forward.

Ama kweli wadanganyika twaliwa. Yaani kodi ya Mdanganyika italipa mafuta ya ndege na marupurupu ya JK's entourage kwenda US eti kupata GOOD DINNER. Mmmh na Prezidaa naye bila ajizi anajibu "LOOKING FORWARD" JK hii ni ya karne, Mobutu ndiye alikuwa Rais Afrika aliyekuwa anapanda ndege kwenda Paris kupata Breakfast kabla hajaingia Ikulu kufanya kazi. JK ni vizuri uwaeleze wenye hizo pesa (Wadanganyika) unakwenda kufanya nini DC mwezi ujao. Kwani huko Japan hamkuweza kuongea mkamaliza mpaka urudi DC. Jamani siku hizi satelite hamna? Kama Rweyemamu hana si unaweza kutumia Webcam basi mkaongea mkamaliza, jamani hizi gharama zisizo za lazima za nini!!!
Hapa kuna kitu na gharama yake si ndogo, guess what.... wadanganyika ndo tutalipa......LOOKING FORWARD.
 
Bush ni bingwa lakini bwege....kambeba Musharaf kwa sababu ya Afghanistan kwa sababu ya gas ya huko manchi mengi tu ya ..stan.

Alimbeba Blair kwa kujua blair was good orator kuliko yeye ili ahalalalishe vita vya kumiliki oil Iraq.

Sasa amekuja Afrika anambeba muungwana kwa sababu ya kumwogopa mchina na kwa sababu ya Mugabe.

Kitu kimoja wengi huwa hawaelewi ni kuwa wazungu awe Mrussia au Mfaransa au Mmarekani wao wote lao ni moja,na vilevile ni macuzin...kwa hiyo wanapokaa wanaangalia kwanza maslahi yao na sisi tukikakaa tunaangalia maslahi yao na hivyo ndivyo ilivyo.

Muungwana tokea mwanzo policy yake ilikuwa ni ya kushikamana na USA...na ni makosa makubwa sana.
 
Ningependekeza abadilishiwe jina from Vasco da Gama to LOOKING FORWARD. Hayo majibu yalikuwa mazuri sana kwa JK alipokuwa ana-respond mwaliko wa Dinner kutoka kwa Kichaka. Kuanzia sasa aitwe President Looking Forward.
 
Wadanganyika,

Hebu tuendeleee kuangalia yale yanayomfanya JK kuchukua misimamo ya ajabu ajabu kwenye masuala ya Africa.

Ama kweli wadanganyika twaliwa. Yaani kodi ya Mdanganyika italipa mafuta ya ndege na marupurupu ya JK's entourage kwenda US eti kupata GOOD DINNER. Mmmh na Prezidaa naye bila ajizi anajibu "LOOKING FORWARD"

JK ni vizuri uwaeleze wenye hizo pesa (Wadanganyika) unakwenda kufanya nini DC mwezi ujao. Kwani huko Japan hamkuweza kuongea mkamaliza mpaka urudi DC. Jamani siku hizi satelite hamna? Kama Rweyemamu hana si unaweza kutumia Webcam basi mkaongea mkamaliza, jamani hizi gharama zisizo za lazima za nini!!!
Hapa kuna kitu na gharama yake si ndogo, guess what.... wadanganyika ndo tutalipa......LOOKING FORWARD.

Hapa ndipo unaona kuwa nchi haina wabunge wala waandishi wa habari.

Mambo kama haya katika nchi za ughaibuni...wabunge wangelikemea waandishi wa habari wangeweka cost zote za safari juu ya meza....tunajua Muungwana amesafiri sana ...je tunajua kiasi gani cha walipa kodi ametumia katika hii misafara?

Kitu cha kushangaza huko bungeni,mbunge anaweza akasimama badala ya kuuliza swali, akaanza kumsifia Muungwana kwa muda wote alopewa aulize swali. Ndio maana hawa viongozi wakishapata kiti wanajisahau kama wao ni binadamu na ukichanganya na mijisifa mengi kutoka kwa wapambe(mawaziri na wabunge).

Ni lazima ipatikane njia ya kuweza kuwaajibisha viongozi wetu hawa,ambao kwa kweli hakuna kinachowakera wanaiba mapesa bayana na hakuna wa kuwanyoshea kidole na kuwafungulia mashtaka...kila siku tunapewa majibu ya ajabu ajabu yaani hata mtoto wa miaka minane anajua kuwa ni ujinga.

Kila siku unaambiwa tuwe na subra...mpaka lini?
 
Papa Benedict huyo kaja Marekani miezi michache iliyopita...katoa hotuba kibao....kiingereza chake kibovu....lakini hakuna aliyemshikia bango. Tena wenyewe wanafurahi kichizi wanapomwona anazungumza kiingereza....

Huwezi kumlinganisha Papa Benedict na Kikwete, Papa Benedict yupo kwenye establishment, anaweza ku afford kuongea kiingereza kibovu.Kikwete ni mtu wa South-South anayeenda ku bargain kwa niaba ya watu masikini, wasio na nuclear, wasio na currency ya world trade, wasio na cultural imperialism, wasio na empire ya Roman Catholicism, wasio na immune system ya kuzuia economic hitmen and so on and so forth.Waswahili walisema usiige Tembo kunya...

Halafu on top of everything anashikiwa bango na yeye vile vile.
 
Bush ni bingwa lakini bwege....kambeba Musharaf kwa sababu ya Afghanistan kwa sababu ya gas ya huko manchi mengi tu ya ..stan.

Alimbeba Blair kwa kujua blair was good orator kuliko yeye ili ahalalalishe vita vya kumiliki oil Iraq.

Sasa amekuja Afrika anambeba muungwana kwa sababu ya kumwogopa mchina na kwa sababu ya Mugabe.

Kitu kimoja wengi huwa hawaelewi ni kuwa wazungu awe Mrussia au Mfaransa au Mmarekani wao wote lao ni moja,na vilevile ni macuzin...kwa hiyo wanapokaa wanaangalia kwanza maslahi yao na sisi tukikakaa tunaangalia maslahi yao na hivyo ndivyo ilivyo.

Muungwana tokea mwanzo policy yake ilikuwa ni ya kushikamana na USA...na ni makosa makubwa sana.

Especially kwenye sera za Bush ambazo zili i defy dunia na kwenda vitani kwa coalition of willing
Matokeo yake ni well...Disastrous.
 
Ukweli ni kwamba tumepayuka kwa ajili ya masters, na Mugabe mpaka leo bado anatustahi wabongo, ingawa Mugabe according to the dataz aliwahi kumpa vipande vizito sana Mama Tibaijuka uso kwa uso, mpaka akalia machozi mbele ya watu kule zimbabwe,

Mugabe ana makosa yake, lakini haya-amount kwa sisi Tanzania the God fathers wa Zimbabwe kuwaa-abandon katika kipindi hiki kigumu sana kwao, kwa sababu ya vipande vichache vya silver, hawa hawa wanaomsaidia Mushaarafu kuiba kura kule Pakistan, leo wanatuambia kuwa ni makosa kwa Mugabe kuiba kura Zimbabwe, halafu cha kushangaza wao wala sio wanachama wa ile Court ya The Hague WHY? Kwa sababu wanajua kuwa huko kwao wana the Mugabes kibao na sisi Tanzania wala hatuwezi kuulizia hilo,

Hii ni aibu kubwa sana kwetu kama waa-Afrika!

Watu wanaliangalia swala la Zimbabwe kama Mugabe vs The West wana distort mambo na kuwafanyia watu wa Zimbabwe bonge la injustice.

Hebu fikiria tu Mugabe and his goons kidnapped and killed the wife of Harare's new MDC mayor, yaani jitu uaji kama hili linaweza kuwachezea watu wazima akili kwa ku spin mambo kuwa wazungu wanamfanyia kampeni? Huu ni mfano mmoja tu wa mtu prominent anayejulikana, wananchi wa kawaida waliopigwa na kuuawa ni kibao.

Hata kama wazungu wanamfanyia kampeni kwa kuua watu Mugabe ame stoop too low na hafai kuongoza nchi.
 
Papa Benedict huyo kaja Marekani miezi michache iliyopita...katoa hotuba kibao....kiingereza chake kibovu....lakini hakuna aliyemshikia bango. Tena wenyewe wanafurahi kichizi wanapomwona anazungumza kiingereza....

Marais kibao tu wanaongea English mbovu tu kina Musharaf na wengineo...tatizo letu waafrika ni bado tuna kasumba ya ukoloni wote hata hawa jamaa wa DRC wanadai kuwa Kibila haongei kifaransa kizuri kama Mobutu...mbona kina Sarkozy wanajua English lakini wanaongea kifaransa?au mtasema kwa vile ni super power?...bollocks.

Kidogo nawasifia Mi Nigeria ikiongea english bila accent yao wanakucheka na kukuita coconut......kikwete kama kakosea grammar hata kichaka mara ngapi anakosea grammar?...swali ni je message intended imefika na kueleweka?..period.

Ilishawahi tokea mwl wetu mmoja,alipotoka kozi uingereza, akawa anakiongea kimombo cha pua....nasi tukawa tunamzimia sana.....ndio tulivyo.
 
Kuna mama mmoja alikuwa ni mmoja wa wasimammizi katika safari ya Bush huko Tanzania aliniambia kwamba Bush alikuwa na furaha sana alivyokuwa Tanzania na alikuwa anawashukurun sana kwa kufanikisha safari yake, na kitu kingine ni kitu cha ajabu kidogo kwa Raisi wa Marekani kukaa siku kadhaa katika nchi yoyote Duniani especial Africa. Halafu Bush aliandika Check (Alisaighn mbele ya Wabongo) na sasa hivi Marekani ina madeni kibaoo na inakopa kutoka China mpaka sasa hivi kununua mafuta halafua bado ianatoa misaada (Kama huo wa Bongo) In short ni kwamba nchi imeshauzwa. GWB ni mfanyabiashara na asingeweza kupoteza muda wake Tanzania kama alivyofanya na kumuita Kikwete rafiki, na achana na hii aliweka Slide show kwenye Website ya White house na aliisifia sana safari yake. Kwa kifupi ni kwamba NCHI IMESHAUZWA. Maana mpaka anamuita rafiki kama hivyo kumbuka hata Sinclair anamuita JK rafiki. Hawa watu esp weupe huwa hawaiti mtu rafiki kirahisi hivyo. Kaa macho JK yasije yakakurudi hayaa.
 
Namkumbuka JKN, namlilia JKN. Alituacha maskini lakini alitupa fahari.
 
Huwezi kumlinganisha Papa Benedict na Kikwete, Papa Benedict yupo kwenye establishment, anaweza ku afford kuongea kiingereza kibovu.Kikwete ni mtu wa South-South anayeenda ku bargain kwa niaba ya watu masikini, wasio na nuclear, wasio na currency ya world trade, wasio na cultural imperialism, wasio na empire ya Roman Catholicism, wasio na immune system ya kuzuia economic hitmen and so on and so forth.Waswahili walisema usiige Tembo kunya...

Halafu on top of everything anashikiwa bango na yeye vile vile.

Museveni anaongea kiingereza kibovu...Kibaki anaongea kiingereza kibovu...Kagame anaongea kiingereza kibovu...Salim Ahmed Salim anaongea kiingereza kibovu....Mbeki naye cha hivyo hivyo tu...ni viongozi wachache mno Afrika wanaoongea kiingereza fasaha....anayekuja kichwani ni Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia....Obasanjo wa Nigeria ndo kabisaa hata mimi mwenyewe huwaga simwelewagi....na yule aliyemrithi Yar'Adua naye sijui hata huwaga anaongea nini.....kuna kipindi watu wa magharibi walikuwa wanamwona Museveni kama success story ya Afrika....wakaanza kumpa misaada kibao.....haya Kagame huyo na kiingereza chake hicho hicho kibovu lakini ameweza na anaendelea kuvutia uwekezaji kutoka makampuni makubwa kama Starbucks....

Nadhani unaweza ku-bargain hata kama kiingereza chako ni kibovu....wewe Pundit una mapenzi yako tu na lugha ya kiingereza na unawaona watu wasiokijua vizuri (at least katika kuongea) kuwa ni bomu. Hiyo ni dhana potofu!!!
 
Kabisa Pundit na Kitila wana mapenzi yao binafsi na lugha ya Malkia. Ohhh nearly forgot, Mugabe is said to be the best english orator in Africa!

As long as the english words, however wll spoken, will never bring food on the table. Hicho kiingereza kikusaidieni nyinyi hatukihitaji!

Ngoja nitafute blog ambayo wazungu wanaulizana who can speak better swahili or Hausa!
 
Museveni anaongea kiingereza kibovu...Kibaki anaongea kiingereza kibovu...Kagame anaongea kiingereza kibovu...Salim Ahmed Salim anaongea kiingereza kibovu....Mbeki naye cha hivyo hivyo tu...ni viongozi wachache mno Afrika wanaoongea kiingereza fasaha....anayekuja kichwani ni Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia....Obasanjo wa Nigeria ndo kabisaa hata mimi mwenyewe huwaga simwelewagi....na yule aliyemrithi Yar'Adua naye sijui hata huwaga anaongea nini.....kuna kipindi watu wa magharibi walikuwa wanamwona Museveni kama success story ya Afrika....wakaanza kumpa misaada kibao.....haya Kagame huyo na kiingereza chake hicho hicho kibovu lakini ameweza na anaendelea kuvutia uwekezaji kutoka makampuni makubwa kama Starbucks....

Nadhani unaweza ku-bargain hata kama kiingereza chako ni kibovu....wewe Pundit una mapenzi yako tu na lugha ya kiingereza na unawaona watu wasiokijua vizuri (at least katika kuongea) kuwa ni bomu. Hiyo ni dhana potofu!!!

Kwani nani kasema huwezi ku bargain? Tatizo ni kuwa deal la milioni 100 wewe utapewa milioni tatu na visifa vya hapa na pale, na picha kwenye New York Times na mialiko White House kazi kwisha.

Trust me katika hao wote uliowataja -I don't know much about Yar'Adua- sifikiri kama kuna mtu anayehitaji handlers kama Kikwete. Kagame na Museveni angalau wana msimamo na guts za kusema wanachoamini, hata kama wako wrong, which half the time they are not.Obasanjo eminent person huyo (pamoja na mzee John Samwel 🙂 ) huwezi kumuweka level moja na Kikwete, alikuwa anadrop jewels wakati Kikwete mtoto wa shule mlimani.

Tofautisha mtu kuwa na accent na kutojua lugha, Minaija karibu yote ina accent thick lakini ukiikuta ianijua lugha ndiyo hiyo mi Chinua Achebe.Obasanjo si mtupu kama muungwana, labda accent.Halafu kuna ujanja tu, wewe msome muungwana hapo juu halafu uniambie kasema nini, hakuna alichosema amebwabwaja nil!
 
kikwete halaumiwi kwa accent yake.....wala halaumiwi kuwa hazungumzi perfect english.
anacholaumiwa ni kwa nini anazungumza english wakati anashindwa kuji elezea inavyostahiki?
akipewa maswala magumu tu, basi unakuta anashindwa kuyakimbia kwa vile lugha haipo. angekuwa anazungumza kwa kiswahili nahisi ingekuwa rahisi kwake kuongea vitu vingi zaidi bila ya kujifunga kwenye point fulani.

nb: bush anamaliza urais hivi karibuni. lakini familia ya bush ina biashara ya ulinzi/silaha na mafuta. sasa huu urafiki wa aina hii, yawezekana ikawa ni njia moja ya kujitayarishia soko lake la silaha.
ama zitumike hapa tz, au iwe ndio njia /sababu ya kuuzia silaha hizo barani afrika
 
The whole thread is very interesting, indeed. Pundit you put across some really good food for thought stuff! Makes one wonder and think deep!
 
Kwani nani kasema huwezi ku bargain? Tatizo ni kuwa deal la milioni 100 wewe utapewa milioni tatu na visifa vya hapa na pale, na picha kwenye New York Times na mialiko White House kazi kwisha.

Trust me katika hao wote uliowataja -I don't know much about Yar'Adua- sifikiri kama kuna mtu anayehitaji handlers kama Kikwete. Kagame na Museveni angalau wana msimamo na guts za kusema wanachoamini, hata kama wako wrong, which half the time they are not.Obasanjo eminent person huyo (pamoja na mzee John Samwel 🙂 ) huwezi kumuweka level moja na Kikwete, alikuwa anadrop jewels wakati Kikwete mtoto wa shule mlimani.

Tofautisha mtu kuwa na accent na kutojua lugha, Minaija karibu yote ina accent thick lakini ukiikuta ianijua lugha ndiyo hiyo mi Chinua Achebe.Obasanjo si mtupu kama muungwana, labda accent.Halafu kuna ujanja tu, wewe msome muungwana hapo juu halafu uniambie kasema nini, hakuna alichosema amebwabwaja nil!

Ohh.... you forgot that John Macsame was a PoW in Vietnam in service of his country.... when the young Barack was in Nursery school somehwere in Jakarta?
 
kikwete halaumiwi kwa accent yake.....wala halaumiwi kuwa hazungumzi perfect english.
anacholaumiwa ni kwa nini anazungumza english wakati anashindwa kuji elezea inavyostahiki?

akipewa maswala magumu tu, basi unakuta anashindwa kuyakimbia kwa vile lugha haipo. angekuwa anazungumza kwa kiswahili nahisi ingekuwa rahisi kwake kuongea vitu vingi zaidi bila ya kujifunga kwenye point fulani.

nb: bush anamaliza urais hivi karibuni. lakini familia ya bush ina biashara ya ulinzi/silaha na mafuta. sasa huu urafiki wa aina hii, yawezekana ikawa ni njia moja ya kujitayarishia soko lake la silaha.
ama zitumike hapa tz, au iwe ndio njia /sababu ya kuuzia silaha hizo barani afrika

I have never been an ardent supporter wa JK..ila kwa kweli kwa hili mnamuonea! Big time! Yaani mtu mkishamchukia basi hawezi fanya lolote zuri! Ohh noo!!!

Hivi hii kasumba ya kulink matatizo yetu na wazungu itaisha lini? mbona msiseme anakuwa rafiki yake..kusudi Bush awape uraia wabeba box wabongo walioko huko majuu?

Hii issue ya kuongea kizungu watu mnabwabwaja tuu..halina mantiki yoyote...whatever he says..as long as kuna substance thats perfect. Kama hakuna basi...

Hapa tuchambue kama aliyoyasema yana umuhimu kwetu ila tukianza kuangalia nani anajua kizungu zaidi ya mwingine..we easily miss the point!
 
I will look for some,

Kabbah alikuwa nahojiwa siku moja na BBC, alikuwa rais wa mpito wa Sierra Leone, jamaa alivyojibu maswali nikaona kuwa kumbe haya mambo ya kuhalalisha poor language / communication skills "eti kwa sababu sisi ni waafrika" hayana msingi, jamaa alitoa majibu yana data, yamepangiliwa halafu yana ile political hope mongering ambayo ilihitajika sana wakati ule wa vita Sierra Leone.Jamaa anaongea na presidential grace na gravita. Kikwete anaongea vibaya kuliko mtoto wa high school anayejua kuongea.

Simaanishi kwamba jamaa ni some african Noam Chomsky, ila alinifurahisha sana kutupa challenge kuwa siyo lazima rais wa Afrika kutojua kujieleza vizuri.

Kikwete ni mtu wa commonwealth kwa hiyo nategemea ajue kiingereza, akienda kwa Sarkozy na kujaribu kifaransa i will cut him some slack.
HAHAHA!!! Wabongo bwana matatizo hivi nyie kimombo mnahusudu saana. kama kiingereza kibovu shauri yao kwani JK anaasili hiyo. mbona maraisi wengine nao huongea hivyo hivyo .iadha kuwa rafiki wa marekani ni vibaya.hivi kuna haja ya kuwa na uhasama na marekani bila sababu.acheni kujifanya mnajua kila kitu kwa kweli maoni yenu ni ziro upuuzi mtupu kikwetu endelea kuimarisha uhusiano na mataifa ya nje utaovunja ngebe za hao watu ambao wamezoea kupakazia tanzania huko
 
Back
Top Bottom