Bush stars na Born Town first eleven.....

Du kumbe kuna wanabodi wa zamani humu.Tukumbushane pia na mambo ya majeshi kwa waliopitia huko kwa mujibu wa sheria,Pamoja na burudani ya gazeti la sani tujikumbushe jinsi tulivyohenyeshwa jeshini pia:wink::wink:.
 
Enzi za mwalimu watu na vipaji vyao! Madenge na Pimbi walitufurahisha sana enzi hizo! Gazeti la uhuru vileee??😇
 
Mamaaah nifah na wewe unakujaga huku! Cc tumewazoea cute b na dada everlenk. Nasikia madenge alisajiliwa toka born town. Ndio maana anavaaga shati.

HahahAha siku mingi sana kina sokomoko, Lodilofa,Madenge, mzee Meko........hivi DrLove Pimbi naye alikuwa anacheza au yeye na mademu tu?
 
Last edited by a moderator:

Wewe ni chibokooo!!! Maneno yote yamekutoka!!!!
 
Last edited by a moderator:
Mimi nilikuwa napenda ile training sessions zao tuu...mazoezi y kijinga kweli.... Km vile...

1. Kuchemshwa miguu kwenye pipa la maji

2. Kuruka mikuki mirefuu..

3. Kuvunjiwa chupa kichwani

4. Kukimbizwa na mbwa wakali...

5. Kupiga mawe ukiwa peku( bush stars)....
 
Enzi za mwalimu watu na vipaji vyao! Madenge na Pimbi walitufurahisha sana enzi hizo! Gazeti la uhuru vileee??😇
Pimbi ndio alikuwa kiboko mzee, alikua anapenda sana mademu lakini hakuwahi fanikiwa kula tunda, isitoshe alikua anapenda wale warefu kumzidi yeye.
 
Dah! Nimewakumbuka kina Chino, Mayuku na Obi.
Kwenye soka mzee meko alikuwa ni magician, bao zake kali alafu akiwala vyenga vya mauzi anawaacha kwenye vumbi kali. Nakumbuka mara nyingi born town walikuwa wanachezea, born town: sokomoko, ndumila kuwili, lord lofa, pimbi, etc
Bush star: kipepe, madenge, mzee meko, etc
 
Kunya boga ..

Huo ndio mwisho wako wa kufikiri? Huna jipya jipange wewe halafu njoo tena,nikiamua ku deal na wewe utaona uchungu na faida ya kukashifu mtu usiyemjua,kaa mkao wa kula tu nikuchemshie Dawa
 


Huu ni utajiri mkubwa tunaupoteza
kulikuwa na jarida lingine lenye bi kisebengo na kapelo...
kulikuwa na hadithi kama za 'mzungu halei mwana'
 
Superstar wa bushstar alikua ni mapungo..mzee wa vibaiskeli.

Nakukumbusha kidogo

Mapung'o ilikuwa gazeti la Bongo na hawa Bush stars ilikuwa gazeti la sani

star wa Bush star alikuwa mzee Meko na katuni zilikuwa za Ibra radi washokera miaka hiyo
 
kuna mtu anakumbuka first eleven....ya timu hizi...
mimi namkumbuka Madenge tu mzee meko wa bush stars
na mtangazaji sukununu...
CHEPE.....alikuwa hatari sana kwa mashuti na tik tak...............
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…