Business Class ina raha yake - tafuteni pesa

Business Class ina raha yake - tafuteni pesa

Sawa mkuu
Wanaopanda hzo business class wala hawaji hapa watu wanapanda maisha yao yote ya uwajibikaji tena wana UN au diplomatic passport sijawah kuwaona wakianzisha threads hadi wanastafu nahisi ww ulipewa nafasi kampuni ya Mr magurue kwenda Kenya imekua case study kuna raha kujichanganya usiombe ww watu kuanzia check in pale nyerere una mwenge wa UN kandahar unaelekea utawaona wale wSimamiz wanakwambia usikae laini hii njo huku unawambia niachen8 niongee na watz wenzangu hapo upo simply ety ww unafraid kuwa business always
 
Ilitokea zali tiketi yangu ilikuwa ni kama vile haitambuliki. Mfumo wao ulikuwa na matatizo wakanikatia tiketi kwenye trip ambayo kumbe ilishakuwa revoked na ikatakiwa kuondolewa kwenye system. Nafika airport system haisomi maana safari ya hiyo tiketi haipo. Halafu ni lisafari lirefu kutoka LAX mpaka Heathrow. Twende huku mara kule hakuna suluhisho maana ilikuwa ni full flight economy kumejaa. Vu bin vu mpaka kwa meneja simu zinapigwa makao makuu Chicago (United Airlines)

Mara naambiwa kuna siti moja imepatikana business class twende. Sema nilikuwa nimetia pamba safi nilipofika huko sikuonekana out of place sana japo ni kweli kuku mgeni hakosi kamba mguuni. Kiti tu kilivyo na entertainment system nikaona leo nimepanda level mpaka nikawa najiuliza huko first class huko kukoje?

Wahudumu wapole, vinywaji na vyakula bwerere, kiti kikubwa halafu kinasukumika kwa nyuma unalala kwa raha, yaani mpaka chooni kuko tofauti. Ni kati ya safari nilizosafiri kwa raha kabisa. Nikawa najisemea kuna haja kubwa ya kutafuta pesa kwa bidii aisee. Ila pesa nazo sasa mh! It has been more than 7 years na pesa ndo kwanza zinazidi kupiga chenga. Pesa hovyo sana aisee!😁
Pesa ni hitaji moja kubwa na muhimu sana kwenye maisha/mwili wa binadamu
 
Shughuli zangu za kutafuta kipato zinanilazimisha kusafir mara nyingi kwenda nje kwa (ndege) za mashirika mbalimbali hususani Emirates, Qatar na KLM.

Sasa kutokana na Miles nilizo nazo mara kadhaa nimekua nikifanya upgrade kukaa Business Class aisee treatment yake si ya kitoto kuanzia CHECK IN, EXCLUSIVE LUXURY LOUNGE na inflight menu na huduma super.

Tutafute pesa.

NB: Samahani kwa wote watakaohisi nimewakwaza kwa bandiko hili. Ila ndio uhalisia
Kitimoto ipo kwenye hiyo business class?
 
Hahahaha!! Shimba ya Buyenze bhana😅

Huku kwema/salama kabisa kaka

Eng'wasi bhageshi
Ng'wagūkū nkoyi.

Nalīgūlombela ng'waka mpya gobuza ūbebe na bitogwa bako nkoyi. Ūngw'wakūguzile (2025) ītagūtole nzunone. Amanyo adakanyiyagwa bahebu. Tolaga! 😁🏃🏿‍♂️🏃🏿‍♂️
 
Kweli tutafute pesa ila. Hatuwezi kuepuka viwango na madaraja ya masikini na tajiri, classes are there for every level.
Kuna tajiri mmoja alikuwa anahojiwa kwa nini anatumia private jet kwenye safari zake zote , akajibu kwenye ndege za kawaida anachukia kupanga foleni na kukalishwa lounges and check ins kwamba anaona anakuwa treated like cattle.
Yaan hata hiyo bussiness class anayosifia mdau hapa kuna mtu anaiona ni useless
 
Shughuli zangu za kutafuta kipato zinanilazimisha kusafir mara nyingi kwenda nje kwa (ndege) za mashirika mbalimbali hususani Emirates, Qatar na KLM.

Sasa kutokana na Miles nilizo nazo mara kadhaa nimekua nikifanya upgrade kukaa Business Class aisee treatment yake si ya kitoto kuanzia CHECK IN, EXCLUSIVE LUXURY LOUNGE na inflight menu na huduma super.

Tutafute pesa.

NB: Samahani kwa wote watakaohisi nimewakwaza kwa bandiko hili. Ila ndio uhalisia
Masikini wakiotea huwashwa .......hawakubali jambo lipite bila kuhadithia
 
Back
Top Bottom