Ilitokea zali tiketi yangu ilikuwa ni kama vile haitambuliki. Mfumo wao ulikuwa na matatizo wakanikatia tiketi kwenye trip ambayo kumbe ilishakuwa revoked na ikatakiwa kuondolewa kwenye system. Nafika airport system haisomi maana safari ya hiyo tiketi haipo. Halafu ni lisafari lirefu kutoka LAX mpaka Heathrow. Twende huku mara kule hakuna suluhisho maana ilikuwa ni full flight economy kumejaa. Vu bin vu mpaka kwa meneja simu zinapigwa makao makuu Chicago (United Airlines)
Mara naambiwa kuna siti moja imepatikana business class twende. Sema nilikuwa nimetia pamba safi nilipofika huko sikuonekana out of place sana japo ni kweli kuku mgeni hakosi kamba mguuni. Kiti tu kilivyo na entertainment system nikaona leo nimepanda level mpaka nikawa najiuliza huko first class huko kukoje?
Wahudumu wapole, vinywaji na vyakula bwerere, kiti kikubwa halafu kinasukumika kwa nyuma unalala kwa raha, yaani mpaka chooni kuko tofauti. Ni kati ya safari nilizosafiri kwa raha kabisa. Nikawa najisemea kuna haja kubwa ya kutafuta pesa kwa bidii aisee. Ila pesa nazo sasa mh! It has been more than 7 years na pesa ndo kwanza zinazidi kupiga chenga. Pesa hovyo sana aisee!😁