Watanzania tuna shida kubwa sana. Rais akibeba ukoo wake wote tunapiga kelele. Aki-play fair tunapiga kelele! Hivi vichwa vyetu vikoje? Mtoto wa dada yake mwalimu ni mtu wa mbali kabisa kwenye familia ya mwalimu, hasa ukizingatia kuwa familia yake ni kubwa sana. Wewe ndugu
Kinjekitile Jr huwa una-take care watoto wote wa dada yako? Dada yako ameolewa na pengine unaweza kuwa na dada hata sita, utafuatilia watoto wake wote na kuhakikisha wamesoma? Nadhani huyu dada yake aliolewa na kwenda kuanzisha familia nyingine kabisa na wa kulaumiwa na huo huyo baba aliyemuoa na familia yake. Sikulaumu ila pengine ni hii tabia ya kutambulisha watu wote wa ukoo wa Nyerere kwa kutumia phrase ''....................wa baba wa taifa Nyerere kafanya................''. Yaani hata watu ambao walikuwa hawapaswi kutambulishwa kwa kutumia jina la Nyerere wanatambulishwa hivyo. Binamu wa baba wa taifa, mjukuu wa baba wa taifa, mtoto wa shangazi wa baba wa taifa, kitukuu cha baba wa taifa, mtoto wa dada yake na shangazi wa baba wa taifa etc. Hii ndiyo inakuwa kama ullusion ya kufanya watu waone kuwa Nyerere alitakiwa ashughulike na watu wote walio associated na ukoo mzima.