Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation, Joseph Butiku amewaonya wanasiasa na wanachama wa CCM kuacha mara moja kampeni za kumchangia Rais Dkt. Samia Suluhu fomu ya kuwania nafasi hiyo tena kwa mwaka 2025-2030, akisema kuendelea kufanya hivyo ni kuunga mkono rushwa.
Butiku ameyasema hayo katika Kongamano la Miaka Mitatu ya Taasisi ya Kizalendo ya Tanzania Patriotic Organisation (TPO) lililofanyika katika Ukumbi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Posta jijini Dar es Salaam.
Katika ufunguzi wa Kongamano hilo Taasisi ya Tanzania Patriotic Organisation nayo haikusita kukemea ubadhirifu na rushwa huku ikiwataka Watanzania kuwa wamoja na wazalendo wanaposimamia mali za umma
Pia soma:
- Kuelekea 2025 - A-Z ya kinachoitwa michango ya kumchangia Rais Samia pesa ya kuchukua fomu ya kugombea Urais 2025
- Kuelekea 2025 - Wakuu wa shule kumchangia fedha ya kuchukua fomu ya Urais Rais Samia 2025, hiki ni "kituko" cha kufungia mwaka
- Makundi mbalimbali yajipanga kumchangia Rais Samia pesa ya kuchukulia Fomu ya Urais 2025
- Vijana kumchukulia Fomu ya Urais Rais Samia 2025
- Kuelekea 2025 - UWT yamchangia Samia Suluhu Hassan Tsh milioni 2 kwa ajili ya kuchukulia fomu ya urais ifikapo mwaka 2025