Butiku aibuka tena:Anasema Tanzania imekosa viongozi wawajibikaji

Butiku aibuka tena:Anasema Tanzania imekosa viongozi wawajibikaji

Dear Masatu mimi si mtu wa matusi .Sikumaanisha kukushia hadhi unless sijaelewa .Again naomba msamaha kama bandiko limekukwaza lakini nasema nia yangu ilikuwa kusema sifungamani na mtu na namuunga mkono mtu yeyote akimwaga point hata hata rafiki yangu Masatu napingana naye sana sana ila akifanya jambo zito sisiti kusema ni kweli Masatu .

Poa mkuu I was just pulling your leg....

Mjadala uendelee...
 
Field Marshall ES,
Mkuu nadhani Butiku kisha yasema mengi ktk hotuba zake zote na sioni sababu ya kuyataja majina ikiwa majina hayo tayari yameisha tajwa na kina Slaa. Tunachofuta kufahamu hapa ni kipi yaani kipi kimpya haswa?...Nina hakika kama atayataja basi mtakuja na hoja ya kuwa kwa nini hakutaja zamani kabla ya Slaa.
Majina yanajulikana kinachotakiwa ni viongozi kusimama na kukemea Ufisadi kwani kinachomuumiza mwananchi sio jina la mtu ila Ufisadi wenyewe...Na hakika neno Tanzania imekosa viongozi wawajibikaji linabeba uzito mkubwa kuliko majina ya watu ndio maana binafsi najiuliza kina Salim, Mwandosya, Kigoda na wengineo wako wapi?... hao wa Upinzani wako wapi tukiondoa wachache waliojitokeza. Huyo rais , makamu na waziri wake mkuu tunao wauliza kila siku wamo pia ktk pakacha la usemi wa Butiku.
Na tukumbuke kuwa ktk Siasa sii viuri kutaja majina ya watu ila mabaya yao kutangulia mwanzo kisha wao watachekecha wenyewe kutoa mbegu mbaya....
Kama alivyosema muungwana hapo juu kuwa Butiku ni mfano bora sana kwetu kuweza kuona jinsi nchi yetu inavyopoteza viongozi na neno KUKOSA viongozi wawajibikaji ina beba uzito mkubwa zaidi ya majina ya mafisadi.... Hii inawakemea hata wale waliokaa kimya pembeni.

Mkandara:
Hili haliwezi kuwekwa sawa zaidi ya ulivyolielezea hapa.
Tunataka na hao viongozi wengine walio safi wanaosemekana wamo humo CCM na wao wajitokeze na msimamo huo huo wa kukemea mabaya, hata kama hawamtaji yeyote yule. Hiyo tu inatosha kututambulisha kuwa wakiungwa mkono hata hiyo hatua ya kutaja wanaweza.

Mfano mzuri sana huo wa hao waliogombea urais na baada ya kushindwa wakawa ni bubu. Hili linawaondolea heshima ya kuwa viongozi wa kutegemewa.
 
Ulikuwa ni uamuzi binafsi wa Butiku, kuamua kusema, na pia ulikuwa ni uamuzi wa binafsi wa Dr. Slaa na Zitto, kuamua kusema,

Hakuna maswali kama Slaaa na Zitto, walisema kwa niaba ya nani betweeen wanachi na matumbo yao, can the same be said about Butiku?

Zitto na Slaa, wamewasema wazi viongozi wabovu, now can we do away na viongozi wengine wa upinzani ambao hawajaiga mfano wa Zitto na Slaaa? Je should it be kipimo cha heshima ya viongozi wetu kuanzia upinzani mpaka CCM, maana kama sikosei urais uligombewa na viongozi wengi kuanzia upinzani to CCM?
 
Mzalendo Halisi,

Nitajibu maswali yako kuhusiana na maoni yangu ya kutaka Bunge na Serikali vivunjwe na vyama vya siasa visitishwe.

Rev.
Hizo point hapo juu zimekaa vizuri- ila nikuulize- do we have a political crisis in Tanzania kwa sasa?
Yes we have political crisis looming. Instability of polictical parties due to lack of morals, strong leadership, emptiness of policies and ideology has resulted into corruption and abuse of politics and people presentation in Government (Wabunge). Vyama vyote havina mwelekeo wowote kulitumikia Taifa ila kupinduana na kukimbilia Ikulu. Look at Zanzibar's crisis between CUF and CCM, look at Muungano, look at the struggle of power between Parliament, Executive Branch and Judiciary Branch. Worse enough is a screwed up constitution that favors one party that is in power and unwillingness of CCM to come to the table to clean up the obstacles to achieve sincere democracy that ensures fair elactions and strict checks and balances on Serikali.

JK na CCM hawawezi kukubali kuvunja Bunge- na hakuna guarantee Bunge jipya will be better!
It is not CCM, but JK as Raisi. Uraisi is an institution by itself, he needs to use constitutional powers to formulate a new political system/structure and after all mechanism are in play, we can have a Parliament and new Government that is for the people, run by the people not a political group or few individuals who are manipuliative using their wealth to enrich themselves.

Haya unayosema ni kama kuna serious Political Crisis!
Usidhani kufumuka kwa Ufisadi na Umasikini si dalili za mpasuko wa kisiasa. We do not need to reach a stage ambapo Kenya wamefikia. We can prevent the mayhem by doing the right thing for the Nation.

We do have a crisis when the Speaker of the Parliament halts tabling of investigative reports due to his absence and worse enough undermining and belittling the deputy Speaker who has same powers per our constitution!

Tambua pia pamoja na mapungufu Tz- bado JK amechaguliwa kuongoza AU!
So was Bashir, Amin, Ghadafi and Mugabe!

Uhuru wa Habari Tz uko juu leo kuliko wakati wowote na hakuna mtu aliyeuawa au kukamatwa na kuonewa!
Not true, sheria ya usalama wa taifa 1970 imetangazwa tena, Kubena kamwagiwa Tindikali, CCM inatumia ubabe wa dola na rushwa kumiliki vyombo vya habari na kuchuja habari.

Haya mambo ya rushwa- well yapo sehemu nyingi tu pia duniani!
So is Ukimwi, upo dunia nzima! That does not justify that we should just let go and accept it as if its a Well we have to deal with our issues our way! not other way and look for excuses!

My dime for the day!
 
Field Marshall ES,
Bila shaka kama kuna kiongozi yeyote ambaye hakukemea maovu, huyu kiongozi hafai kabisa kugombea nafasi ya Urais na tuna kila haki ya kumshutumu. Huwezi kugombea urais wa nchi kwa tiketi ya chama chochote kile ikiwa wewe mwenyewe huyafahamu mabaya maanake siasa za Tanzania zina nadi zaidi AHADI kuliko uwajibikaji. Hakuna mpango wa kuangalia mapungufu ama uzembe wa mgombea na hii huitwa kufuru kubwa kiasi kwamba utaombwa uombe msamaha hata kama maneno yako ni ya kweli.
Hivyo basi Ufisadi huu uwe somo kwetu kuelewa nani ana uchungu na nchi yetu, tena basi ni kutokana na kelele za wananchi JK anmeweza kulitupia macho swala hili, what if ingekuwa toka kwa viongozi wagombea wenzake?...
Mkuu, Tanzania hatuna viongozi wawajibikaji na huu ndio ukweli ambao Butiku kausema iwe kamlenga mtu mmoja, CCM ama vyama vya Upinzani...
 
Joseph Butiku kiumri sasa anapaswa kumshukuru mungu kwani ameshaanza kumkopa mola siku zake hapa duniani,We heard about Mkapa since 2005 todate, what a song? Huyu jamaa anamuogopa JK kwa kujua nguvu za kidola alizonazo , kwa vile ya Mkapa alishayaongea na nilidhani amehitimisha kwa kushangilia na kutoa sababu za Mkapa kuikosa aki highlight-Ufisadi wa Mkapa kama kigezo kikubwa kilichomuangusha na pia Pemba 2001 siku ile pale Channel Ten Chisano alipopewa Mo Ibrahim Prize. Give us a break mtu mzima, sasa kila likijitokeza jambo basi ana simama na kuhoji uadilifu wa Top Leaders of CCM without mentioning,akibanwa atakwambia Mkapa!!!,aache uhuni huo maana sasa tunaanza kuona game hii imewafaa wengi wanaotaka tuwafananishe na Mwal.Nyerere au kujitafutia uhalali wa kusikilizwa ktk CCM na serikalini kama mwalimu.

Ninapenda kuthubutu kusema kuwa kama huyu mzee haogopi dola ya JK basi ametumwa na wenye Dola kuufanya mchezo huu.

Tumewaona wana habari sasa wanamuomba msamha mzee Mwinyi na kumhukumu Mkapa,sasa wameenda mbali zaidi maana Alhaj mwini sasa ni kioo chao cha uadilifu dhidi ya Mkapa,tumeyasikia maoni ya Alhaj Mwinyi siku za karibuni na jana pal;e M/nyamala,tumemsikia JK akilalama juu kukosekana kwa uadilifu kwa viongozi wa umma,jana amethubutu kuwa muwazi zaidi kwa kutuambia kuwa hata kama kiongozi atajenga mabarabara kibao kama si muadilifu wananchi watamchukia tu,so issue ni nini hapa waungwana?

Tuamini kuwa Butiku ni mtetezi wa wa wanyonge? Mtumwa wa Dola ktk kushambulia ? Msemaji wa kundi fulani ndani ya chama au?

Wana habari baada ya kumtakatifuza Mzee Mwinyi sasa naye ameanza kuwashukia watesi wake taratibu na vijembe na kwa mbali Muungwana akichombeza.

Pazuri sana hapo wakuu,tuombe mungu kuwa kauli za wakuu ziendane na matendo yao 1.Mwacheni mzee Mkapa apumzike 2. Usifanye biashara above 40 3.Sintashughulika na watangulizi wangu4. Hata kama umejenga mabarabara lukuki kama siyo muadilifu wananchi hawatakupenda,na tumeanza kuiona hali hii.

Binafsi sidhani hili sakata ni EL,Kara,Dial na Rostam ,huu ni mchakato wa kuondoana ktk kiwango cha utukufu mbele ya jamii yetu zaidi kuliko kuijenga nchi yetu.

Mungu ibariki Tanzania
 
Ri urimi rako rimeanza kuterezaga na unaongea kiruga cha Taifa sawasawa au ni loho mtakatifu kakuingia? Tafuna urimi wako uenderee kuongea kwa rugha ya Mrakuka!

iri naro sirierewi rinafutaga na renyewe au rinataka kuretaga kurete kurete,
 
Ri urimi rako rimeanza kuterezaga na unaongea kiruga cha Taifa sawasawa au ni loho mtakatifu kakuingia? Tafuna urimi wako uenderee kuongea kwa rugha ya Mrakuka!

iri naro sirierewi rinafutaga na renyewe au rinataka kuretaga kurete kurete. simifidore irikoseaga kwani nakandamisaga kwa riurimi.rroo,
 
Back
Top Bottom