Butiku: Ningejua CCM itaingilia mchakato wa Katiba nisingeshiriki

Butiku: Ningejua CCM itaingilia mchakato wa Katiba nisingeshiriki


butiku+px.jpg

Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Joseph Butiku






Tanga. Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Joseph Butiku amesema asingekubali kushiriki katika Tume hiyo laiti kama angejua CCM ingeingilia mchakato huo.

Butiku ambaye alitoa kauli hizo kwa nyakati tofauti, wikiendi iliyopita kwenye Mabaraza ya Katiba ya Halmashauri ya Mji wa Soni, Lushoto na Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, alieleza kutokufurahishwa kwake na kitendo cha CCM kushinikiza maoni yake mbele ya mabaraza hayo.

Alilalamika kuwa kitabu cha mwongozo wa utoaji maoni kilichotolewa na CCM kinatumiwa vibaya kushinikiza maoni kwenye Rasimu ya Katiba Mpya.

"CCM imeandaa kitabu kizuri kweli kusaidia wanachama wake, tuliwaambia (Tume) hatukitaki; ni mwongozo kusaidia wanachama wake namna ya kutoa maoni, lakini kimekuwa kinatumika vibaya. Kinatumika kushinikiza maoni," alisema Butiku.

Butiku ambaye ni mwanachama wa Tanu tangu mwaka 1958 na CCM kuanzia 1977 alisema: "Ningejua itatokea chama kitafanya hivyo, nisingekula kiapo nilichokula kufanya kazi hii katika Tume ya Marekebisho ya Katiba. Kundi moja lisigeuke Tanzania. Mimi ni mzee nasema kitu kikubwa nataka Mwenyekiti (wa CCM) asikie, Halmashauri Kuu yangu (ya CCM) isikie. Mchakato huu usiingiliwe, madiwani saidieni wananchi wenu kujielewa. Muungano hautaponywa kwa helikopta zinazoruka au vitabu vinavyosambazwa."

Muungano

Kuhusu Muungano, Butiku aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini alisema: "Mimi ni mzee sasa, sitaki kwenda kaburini bila kuwaambia ukweli. Endeleeni kuujadili, msifanye jambo la kutaka asali bila kujua madhara yake," alisema.

Kauli hiyo ya Butiku ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Mfuko wa Mwalimu Nyerere ilitokana na wajumbe kuonyesha mvutano kuhusu muundo wa Serikali katika Muungano na wengi walionekana kuelemea upande wa Serikali mbili uliopo sasa, baadhi kuunga mkono Rasimu ya Katiba inayopendekeza Serikali tatu, huku wachache wakitaka Serikali moja.

Butiku aliwataka wajumbe wa Mabaraza ya Katiba kutoa maoni yanayolenga kulinda na siyo kuvunja Muungano na kwamba Tume ya Marekebisho ya Katiba imepewa kazi ya kuulinda akisisitiza kwamba haikuwa, wala haina ajenda ya kuvunja.

"Wapo pia viongozi wakubwa ndani ya Baraza la Wawakilishi, wengine wamestaafu, hawautaki Muungano. Tume inawafahamu wanaotaka Tume ya Katiba iwe na ajenda ya kuvunja Muungano. Muungano huu, ulimfukuza Aboud Jumbe madarakani, kiongozi mkubwa tu, mi nawaambia mambo mengine siri. Jumbe alitoka kwenye mkutano wa CCM, kaja pale nje akakuta gari lake lingine siyo la Makamu. Leo, (anamtaja kiongozi huyo) anasema tulifanya makosa kuungana, anajiunga na Jumbe, anaanza kufanana na Uamsho," alisema Butiku.

Butiku aliifananisha Katiba Mpya nzuri kuwa sawa na asali akieleza kuwa inahitaji umakini wakati wa kuiandaa, akifafanua kuwa unapoandaa asali lazima uwe makini vinginevyo unaweza kuambulia kushambuliwa na nyuki.

"Wajumbe msipokuwa wa kweli, badala yake watu wakaumwa na nyuki, mtatulaumu. Ukweli wanaufahamu wote ili waweze kuamua? Tumekubaliana kwenye Tume tuambiane ukweli ili tupate asali."​

Mzee Butiku anataka kusema nini hapa mbona simwelewi?

loh!
 
ccm wanawalisha watu sumu, kitu ambacho hakiwezi kutatua tata za muungano. muarubaini wa muungano si mbili wala moja. tuko kwenye mbili matatizo tulo nayo ni mengi.

sasa twende kwenye tatu kama kweli tunapenda muungano. tuloungana nao watanganyika tuwajue na ss ndio tupo, na tunachokiunda kiwe wazi. vifitna na unafiki wa mwanakijiji na wenziwe kwa sasa hazina nafasi
 
Butiku ni mingoni mwa wana Ccm wanache, wanao muishi Mwalimu, wengine ni Dr.Salim na Ibrahim Kaduma!.

Hapa Pasco unamaanisha mbali na Mwl, ni watatu hawa wanaoweza kuikosoa CCM bila kuuma maneno. Sasa je, watatu hawa wataweza 'kuyatingisha maji' yanayoonekana yametuama ndani ya 'beseni' la CCM?

btw, Pasco unaonaje mawazo ya Mzee Jaji Warioba? hayafanani na akina Mzee Butiku, Mzee Dr. Salim na Mzee Kaduma?
 
Anapaswa kujiuzulu ili kuonesha msimamo wake. CCM iachie tume wafanye kile kilicho matakwa ya wengi.
CCM ukiwasusia jambo huwa hawajali, cha msingi ni kukomaa nao hadi mwisho; by the way hawakuwa tayari pia nia ya dhati ya kuandika kabisa mpya hii, ndiyo maana watavutia kwao ili waendelee kutawala.
 
kama ana nia kweli basi awe kama Punda, utampeleka kisimani na kama hataki kunywa hatakunywa na wala hutamlazimisha, tume ndo itakayotoa rasimu kwa kuandika, wao waandike wanayoona ni sahihi na wala CCM hawana uwezo wa kuingia kwenye tume na kuandika wanayotaka akishindwa ajitoe.
 
pamoja na maonyo mazuri ya mzee Butiku, alipaswa kukataa huo ujumbe mapema kwa kuwa anaijua ccm fika. Kujitoa lawama muda huu ni kutughilibu
 
Ccm inadhani tanzania ndo yenyewe, lichama hili litavunja muungano kwa kuwapuuza watanzania!
 
Hakuna kujiuzulu,apambane humohumo hadi tuipate katiba mpya,kujiuzulu ni kumsusia nguruwe shamba la mihogo
 
pamoja na maonyo mazuri ya mzee Butiku, alipaswa kukataa huo ujumbe mapema kwa kuwa anaijua ccm fika. Kujitoa lawama muda huu ni kutughilibu


Huyu Mzee kuna habari ambazo siyo rasmi kua ana kiwanja cha wazi kila sekeseke la viwanja likiibuka na yeye anaibuka sasa sijui kama kuna uhusiano na kauli za safari hii.
 
Aache kupiga Siasa.Kama kweli anamaanisha anachokisema ajiuzulu hata sasa ili kutoa Somo kwa CCM,

Huyu Butiku alikuwa amechoka sana wakati alipoteuliwa kuingia kwenye hiyo tume sidhani kama ana ubavu wa kuweza kujiuzuru kutoka kwenye tume yenye ulaji mnono!!! Hiyo yote ni danganya toto tu.
 
Butiku ni mingoni mwa wana Ccm wanache, wanao muishi Mwalimu, wengine ni Dr.Salim na Ibrahim Kaduma!.
Pasco. Nadhani walimwelewa, na umuhimu wa kuwa watanzania kwanza. Tatizo watu tumejitwika vyama, na wengine hawaiju kabisa maana yake. Ebu fikiri mtu chama chake kina ahadi kwa kila mwanachama kuwa inayosema "nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko'. Ukisema neno ukweli, kwangu ni kuwa uwiano sawia kati ya kile unachokifiri, na kusema ama kukiandika na uhalisia wa jambo unalolijadili. Hebu fikiri mfano wa Mwigulu akijua fika kutakuwa na mkutano wa katiba chini ya chadema, naye anaondoa watu kwenda kuangalia mpira wa mchangani kwa kuwaita simba' kwenye mtandao anasema wanairamba wameikataa CDM, lakini mimi naona ilikuwa fitina tu. Kwa hiyo unaweza kuondoka na neno moja Mwigulu si Mkweli, ni mwongo na mtu wa fitina kinyume na ahadi ya chama chake. Sitaki kusema ile ya rushwa, manake unaweza rushwa toka ghorofani endapo uko huko.
 
Nilitarajia kuona neno kifo, kasema laziama aseme ukwel kabla hajafa! Miccm mingine inawaza kummwakyembe.
 
Butiku ni frustrated individual fulani hivi, bado ana hasira za kupigwa chini na Ben Mkapa alipotaka Uenyekiti wa bodi wa shirka nyeti. Since then amekuwa anti CCM in the name of Mwalimu Nyerere foundation.

Hana jeuri ya kujiuzulu and I can bet on that, kuacha posho ya 400,000 kwa siku Shangingi la ngvu na masurufu kedekede kunataka uzalendo wa hali ya juu na Butiku hana. Alikuwa kachoka uso umejaa michirizi kwa njaa, leo anawaka na kumemeremeta. Si basi kamkuta Kikwete muungwana mambo haya asinge thubutu kuyafanya wakati wa Ben Mkapa.

Hii ningejua kama CCM itaingilia nisingekubali, sasa washaingilia sii ujiuzulu tu kwani kuwa kwenye tume ni kufungwa jela huwezi kutoka kwa hiari yako?

Tumsubiri mwanae mmoja anajifanya Chadema saaaana ilhali wanakula fadhila za CCM atakuja tu kumwaga uharo wake
 
Huyu mzee ni mnafiki tu ,baada ya kuvimbiwa ndio anaanza kubwabwaja.
 
Back
Top Bottom