Buy it for Life: Tujuzane brand ama model za bidhaa zinazodumu kwa muda mrefu ili tuepukane na usumbufu wa kununua upya

Buy it for Life: Tujuzane brand ama model za bidhaa zinazodumu kwa muda mrefu ili tuepukane na usumbufu wa kununua upya

Uzi huu tujuzane bidhaa zenye viwango vya juu hasa kwa wale wasio na pesa za ziada za kununua upya kitu kile kile ama wanaopenda kukaa na vitu vinavyodumu.

Tujadiliane brand ama model za bidhaa zenye kutumika muda mrefu bila kuchoka ama kufubaa haraka, durable vyenye uwezo mkubwa wa kuhimili mazingira mengi, yaani ukinunua ni mpaka uje ukichoke mwenyewe ama kikiharibika huna cha kudai.

Pasi ya uhakika ambayo haijachuja kwa ubora wake hapa kwetu ni phillips, Binafsi niliwahi kununua pasi yenye manjonjo ya kutoa mvuke na kumwaga maji ila nililazimika kurudi phillips.

View attachment 2868879


Furniture zako jipinde chonga za mbao ya Mninga, utazitumia miaka nenda rudi hata wajukuu wanaweza zikuta

View attachment 2868518

Laptop inayodumu nunua Chapa ya LENOVO THINKPAD, hili dude utalitumia mpaka uchoke mwenyewe, zimetengenezwa kwajili ya kudumu.

View attachment 2868506

Jeans - chapa ya Levis ukiikuta hata mtumbani ibebe haraka, utaivaa sana ukifulia sabuni ya kipande

View attachment 2868708
Mmmmmmh apa sasa mnatupanga kunakitu kisichoisha jmn
 
Hio iphone ni gereza la kifahari inapewa wa promo tu, simu battery inakaa kidogo, haina radio, system yake inakuwa obselete ndani ya miaka michahche, earphone zake mpaka uchaji huwezi tumia kawaida, kuhamisha mafaili kwenye computer ni shughuli pevu, apps zake ni chache, bando likiisha huwezi tumia internet bure kwa vpn, n.k.

Leo hii wamezitosa usb cable zao kwa kukubali ukweli zilikuwa hazina nguvu na speed, wanatumia usb c za android ila bado wana jeuri kuwakataza wateja wao wasitumie usb za android wakati zinapiga kazi fresh na ni wao wameiga teknolojia, sio wao waliozibuni hizo cable, ni sawa na mwanafunzi kutaka kumfundisha mwalimu.

[emoji16] pole sana

Vp kuhusu bidhaa nyingine kando na simu zenyewe uchambuzi vp?
 
Kitanda cha mninga kinahitaji kusafishwa kila baada ya miaka kadhaa, kinapigwa vanish na kurudi kwenye ubora wake kama zamani.
Kuhusu dhambi anakipeleka Kwa Mwamposa tu hapo Kawe.
 
Sendo-maasai made
Mkanda-maasai made
Medicine - maasai made

Hawa jamaa hawanaga fake product 😂
 
Back
Top Bottom