Bw.Tundu Lissu siyo Intelligent!

Bw.Tundu Lissu siyo Intelligent!

Duh gombesugu, kwanza mimi kama utakuwa tayari kujadiliana na mimi bila kuingiza Udini, hapo tutaongea lakini mnapoingia kwenye Udini, huko hutaniona. Usitegemee kuona mchango wowote kutoka kwangu unaogusia imani ya watu, huko hunikuti hata kwa dawa! Hayo nawaachia wachochezi wanaoamini wana undugu na wakoloni na walowezi waliotuletea mila zao wakiziita dini kuliko sisi ndugu zao Watanzania.

Pili niliwahi kuelezea historia yangu kidogo lakini naona umesahau, mimi ni Mtanzania kwanza ndio mambo mengine yanafuatia. Sijawahi kujiunga na chama chochote cha siasa toka nizaliwe (tafadhali amini hilo) ila kwa kweli siipendi na wala sijawahi kuipenda CCM maishani. Kidogo nijiunge na NCCR Mageuzi mwaka 1994 lakini alipoingia Augustino Mrema akitokea CCM na kupewa uongozi, mimi huyoo...nikarudi kwenye ganda langu.

Unao uhuru wa kunihusisha na Bavicha ingawaje kwa umri wangu nadhani Bavicha ni kwa wajukuu zangu na hata hiyo Chadema naisikia tu ingawaje nawaunga mkono dhidi ya ufashisti na ukoloni mamboleo wa CCM. Sijawahi kuyumba katika msimamo wangu na naamini suluhisho pekee katika kuutatua huu muungano wa kero ni mfumo wa serikali tatu na ingawa serikali moja ingefaa zaidi, mimi siyo dreamer niko down to earth.

Kuhusu lugha yangu ya kwanza ni kwamba nilianza kuongea Kiswahili nikiwa na umri wa miaka mitano na ukweli ni kwamba nakielewa Kiswahili kuliko lugha yoyote ile, asante zimuendee Mwalimu Nyerere! Hata hivyo naunga mkono rasimu kama ilivyotolewa na Tume ya Katiba ikiongozwa na Jaji Joseph Sinde Warioba pamoja na maelezo aliyoyatoa Mh. Tundu Lisu ndani ya Bunge Maalum la Katiba kuhusu mfumo wa serikali tatu.

Upepo wa Mageuzi ukiwa umeshika kasi miaka ya 1990, kiongozi mojawapo wa Mageuzi akiitwa Mabere Nyaucho Marando bila kujua msimamo wa Mwalimu Nyerere alitoa kauli iliyodai Mwalimu kafilisika kisiasa. Taifa zima lilikuwa kama limepigwa radi! huyu kijana kathubutuje kutoa kauli kama hiyo! Woga mkubwa ulitanda ndani ya taifa na Marando akajikuta ametengwa na ndugu na marafiki..hakuna aliyetaka kukaa karibu yake.

Tofauti na walivyoamini wahafidhina ndani ya CCM wakiongozwa na Raisi Mwinyi, Waziri Mkuu Malecela, Waziri wa Mambo ya Ndani Agustino Mrema walioamua kuendesha operation ya kanyaga sisimizi, Mwalimu bila kuwaonea haya alitamka kwamba kuongelea vyama vingi si dhambi. Akawatahadharisha CCM kuwa wajiandae kwani hawataweza kuuzuia upepo wa mageuzi. Huyo ndiye Mwalimu, alienda na wakati, alisoma alama za Nyakati.
. T
Leo hii angekuwepo angewashangaa hawa malimbukeni wanaomnyooshea kidole Mhundu Lisu. Yawezekana Mwalimu alikuwa na sababu zake za kutotaka Muungano uhojiwe nyakati zile kama ambavyo hakutaka mfumo wa vyama vingi baada ya uhuru lakini baadaye akawa wa kwanza kuikemea CCM kutokuwa tayari kukaribisha mageuzi. Mwalimu alishaanza kutambua kuwa ndoto yake ya serikali moja haiwezi tena kutimia.

Mwalimu pole pole alianza kuwa na wasi wasi na chama alichokiasisi yeye mwenyewe na hata mara moja hakuficha hisia zake kuhusu manyang'au walioiteka CCM. Usemi wa "CCM si mama yangu" ni ushadhidi tosha kuwa hakuafiki gari la CCM lilikokuwa likielekea na alikuwa anasubiri tu kituo muafaka aweze kushuka. Mwalimu kuitelekeza CCM? CCM bila Mwalimu? Hiyo haingewezekana, manyang'au hawangebaki salama...ni ama wao au Mwalimu!

Nina hakika alipo Mwalimu, anapoliangalia hili toto tundu, anatabasamu kwa sababu alijua ni swala la muda ukweli lazima utajulikana tu muda wake ukiwadia. Na huo muda umewadia, asante Tume ya Katiba, asante Tundu Lisu na asante Watanzania waliotoa maoni yao. Muda muafaka wa serikali tatu umewadia na kama ilivyokuwa kwa mageuzi, Mwalimu angekuwepo angewakumbusha CCM kwamba si dhambi tena kuongelea serikali tatu.
Mkuu Mag3.
Nona umefika mbali mpaka kumtusi Mzee wetu wa Chadema muasisi jambo hili alikubaliki kabisa au umetumwa.
quote_icon.png
By Edwin Mtei
Nilisikiliza Mheshimiwa Tundu Lissu na nasikitika kwamba sikubaliani naye jinsi alivyoeleza shutma juu na dhidi ya Mwalimu Julius Nyerere, Baba na Muasisi wa Taifa letu. Inajulikana na umma wa Watanzania, kwamba mimi binafsi, kama Waziri wa Fedha, nilitofautiana na Mwalimu, nikajiuzulu Uwaziri Decemba,1979, nikimwomba ateuwe Mtanzania mwingine atakayeshauri mambo ya Uchumi na Fedha. Lakini tuliendelea kuwasiliana kwa maelewano bila chuki, na hata aliniteuwa niwe Mwakilishi wa Tanzania na Afrika inayoongea Kiingereza katika IMF (Shirika la Fedha Duniani) chini ya miaka mitatu baadaye Novemba, 1972. Nimekuwa na mawasiliano na maelewano mazuri sana na Mwalimu hata baada ya kuasisi CHADEMA, Julai 1992 na tulipokamilisha Katiba na Sera za Chadema, nilimtembelea Nyumbani kwake Butiama nikampa azisome ajionee jinsi tulivyonuia kuwahudumia Wananchi wetu. Hata siku moja siwezi kumtusi Muasisi wa Taifa letu. Iwe ni mwiko pia kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kumtusi Baba wa Taifa.

Ningewashauri uongozi wa Chadema na hasa Vijana wa M4C (Vuguvugu la Mabadiliko) tuendelee na uhamasishaji : kwa umakini, tukiwa na huruma kwa wanyonge maskini wa kutupwa, tukijiandaa kwa umakini na kiutaalamu Sera na Mikakati ya kuwakomboa toka katika umaskini wa kutupwa kwa kutumia nguvu ya umma (Peoples Power) tukitumia mikakati sahihi: kwani Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke: Mikakati na Sera sahihi ikiwa ni kutumia misingi ya Uchumi na Miundombinu tulionayo licha ya uhalisia dhoofu tulioridhi; tukiwaenzi walioijenga na kuturidhisha kwa unyofu wao. Roho ya Julius Nyerere ilale mahala pema Peponi. Amen!

With all due respect to Hon. Tindu Lissu, this smacks BAD TASTE.

Edwin Mtei
Founder Chairman of CHADEMA
.

Angalia hapo nilipokoleza wino mwekundu.
cc gombesugu
 
Last edited by a moderator:
imeandikwa... '' hakuna mwanadamu aliyemkamilifu''.

si tundulisu wala baba wa taifa.
 
/ɪn'tɛlɪdʒənt/

adjective

1. having the capacity for thought and reason especially to a high degree

2. endowed with the capacity to reason syn: reasoning, thinking

3. exercising or showing good judgment

4. possessing sound knowledge syn: well-informed

He has ALL four.
 
Mkuu Mag3.
Nona umefika mbali mpaka kumtusi Mzee wetu wa Chadema muasisi jambo hili alikubaliki kabisa au umetumwa.

Angalia hapo nilipokoleza wino mwekundu.
cc gombesugu

Kwanza kwa taadhima kuu naomba nikufahamishe kwamba mimi ni mtu huru, si mwana Chadema, sijawahi kuwa mwanachama wa Chadema wala kuhudhuria mkutano wowote wa Chadema. Pili sijawahi kukutana wala kuongea na kiongozi yeyote wa Chadema, sanasana nawasikia tu redioni na kuziona picha zao kwenye magazeti na mtandaoni. Kitu kimoja kinachoweza kunihusisha na Chadema ni msimamo wangu dhidi ya mafashisti na malimbukeni wa CCM, period. Hivyo msimamo wa Mwanzilishi wa Chadema, Edwin Mtei, unanihusu nini? Naomba pia usisahau kitu kimoja, mimi ni mtetezi mkubwa wa Mwalimu, si humu JF tu, dhidi ya vitendo na dharau anazofanyiwa na wanafiki ndani ya chama tawala...wanamkumbuka tu Mwalimu maji yanapowafika shingoni na hawana namna. Tendo gani ovu linazidi kutoa roho ya binadamu kwa uroho tu wa kubaki madarakani?
 
kweli Tundu lissu ni msomi wa sheria kawaida wanasheria wanaweza kukutoa kwenye hoja ya msingi ukaenda kwenye hasira hapo lengo lake linakuwa limetimia kuwa makini sana mwanasheria anapoongea na unapotaka kumjibu maswali mengi ni mtego na ni uchokozi ili ughazibike
 
hahaha, watu huwa wanajificha nyuma ya ukweli aisee.
ngoja kwanza, ina maana umetoa kura ya kulegalise bhange? :majani7::majani7:

Kama Peter Tosh.

Vitu vidogo havinisumbui.

This is just a matter of time, ikikubaliwa Cali na NY na Amsterdam, kwingine tutafuatilia tu.

Hata kama ni "medical marijuana" tu.
 
Bw.Tundu sio mtu intelligent kama watu wengi wanavyodhania, kwa maana mtu intelligent huwa ana uwezo wa kujua madhara ya kile anachokisema kabla hajakisema!

Mtu intelligent yoyote anapaswa kufahamu ktk Nchi kama TZ hauwezi kuanzisha Vita dhidi ya Mlm.Nyerere na ukashinda hata uwe nani, hata Raisi wa nchi leo hii akianzisha Vita dhidi ya Mlm.Nyerere hawezi kushinda mwishowe kuna mtu tu anaweza hata akajitoa mhanga kumlipua!

Ni sawa naleo hii Marekani mwanasiasa aanzishe Vita dhidi ya sijui Raisi Washington au Lincoln hawezi kushinda hata iweje hata kama huyo Mwanasiasa yuko sahihi kwa kiasi gani, vile vile kama ilivyo pia hakuna Mwanasiasa AK leo hii ambaye anaweza akaanzisha Vita dhidi ya Bw.Mandela na akashinda hata kama atakuwa sahihi kwa kiasi gani, na ndio maana utaona Wanasiasa wenye akili linapofika kwenye swala la hawa watu huwa wanakuwa waangalifu sana wawe ni Demokrats au Republikan hakuna anayethubutu kuwaongelea na kuwakashifu Lincoln hata kama walifanya makosa kiasi gani kwa maana wanafahamu kwamba hawa Watu nafasi yao imeshaandikwa kwenye Historia na huwezi kuifuta bila kukugharimu...

Bw.Tundu alipaswa aelewe kwamba hata kama Mlm.Nyerere amekosea kwa kiasi gani hakupaswa kumuongelea vile, alipaswa aelewe kwamba kuna watu wako tayari kufa kumtetea Mlm.Nyerere na hiyo ni Nchi nzima kuanzia jeshini mpaka Utingo wa daladala...

Kuna tofauti kubwa sana kati ya neno "intelligence" na "wisdom". Nadhani unachoongelea ni Lissu, kwa mtazamo wako, kukosa "wisdom".

Sidhani kama Lissu siyo "intelligent" kama unavyodai. Maana kazi ya kumchambua na kumuweka "uchi" Nyerere, ambayo Lissu amefanikiwa, si ya kichwa cha kitoto. Hata Nyerere angekuwepo, ange-divert issue za Lissu kwa vijembe na ukomedi, lakini si kwa uzito wa hoja.

Lazima taifa hili limpe heshima yake Lissu. Kama kwa hoja za Lissu articles za Muungano zimewekwa wazi, kitu ambacho kuna watu wanazeeka ndani ya CCM hawajawahi kukiona, you have to respect Lissu.
 
Duh gombesugu, kwanza mimi kama utakuwa tayari kujadiliana na mimi bila kuingiza Udini, hapo tutaongea lakini mnapoingia kwenye Udini, huko hutaniona. Usitegemee kuona mchango wowote kutoka kwangu unaogusia imani ya watu, huko hunikuti hata kwa dawa! Hayo nawaachia wachochezi wanaoamini wana undugu na wakoloni na walowezi waliotuletea mila zao wakiziita dini kuliko sisi ndugu zao Watanzania.

Pili niliwahi kuelezea historia yangu kidogo lakini naona umesahau, mimi ni Mtanzania kwanza ndio mambo mengine yanafuatia. Sijawahi kujiunga na chama chochote cha siasa toka nizaliwe (tafadhali amini hilo) ila kwa kweli siipendi na wala sijawahi kuipenda CCM maishani. Kidogo nijiunge na NCCR Mageuzi mwaka 1994 lakini alipoingia Augustino Mrema akitokea CCM na kupewa uongozi, mimi huyoo...nikarudi kwenye ganda langu.

Unao uhuru wa kunihusisha na Bavicha ingawaje kwa umri wangu nadhani Bavicha ni kwa wajukuu zangu na hata hiyo Chadema naisikia tu ingawaje nawaunga mkono dhidi ya ufashisti na ukoloni mamboleo wa CCM. Sijawahi kuyumba katika msimamo wangu na naamini suluhisho pekee katika kuutatua huu muungano wa kero ni mfumo wa serikali tatu na ingawa serikali moja ingefaa zaidi, mimi siyo dreamer niko down to earth.

Kuhusu lugha yangu ya kwanza ni kwamba nilianza kuongea Kiswahili nikiwa na umri wa miaka mitano na ukweli ni kwamba nakielewa Kiswahili kuliko lugha yoyote ile, asante zimuendee Mwalimu Nyerere! Hata hivyo naunga mkono rasimu kama ilivyotolewa na Tume ya Katiba ikiongozwa na Jaji Joseph Sinde Warioba pamoja na maelezo aliyoyatoa Mh. Tundu Lisu ndani ya Bunge Maalum la Katiba kuhusu mfumo wa serikali tatu.

Upepo wa Mageuzi ukiwa umeshika kasi miaka ya 1990, kiongozi mojawapo wa Mageuzi akiitwa Mabere Nyaucho Marando bila kujua msimamo wa Mwalimu Nyerere alitoa kauli iliyodai Mwalimu kafilisika kisiasa. Taifa zima lilikuwa kama limepigwa radi! huyu kijana kathubutuje kutoa kauli kama hiyo! Woga mkubwa ulitanda ndani ya taifa na Marando akajikuta ametengwa na ndugu na marafiki..hakuna aliyetaka kukaa karibu yake.

Tofauti na walivyoamini wahafidhina ndani ya CCM wakiongozwa na Raisi Mwinyi, Waziri Mkuu Malecela, Waziri wa Mambo ya Ndani Agustino Mrema walioamua kuendesha operation ya kanyaga sisimizi, Mwalimu bila kuwaonea haya alitamka kwamba kuongelea vyama vingi si dhambi. Akawatahadharisha CCM kuwa wajiandae kwani hawataweza kuuzuia upepo wa mageuzi. Huyo ndiye Mwalimu, alienda na wakati, alisoma alama za Nyakati.

Leo hii angekuwepo angewashangaa hawa malimbukeni wanaomnyooshea kidole Mh. Tundu Lisu. Yawezekana Mwalimu alikuwa na sababu zake za kutotaka Muungano uhojiwe nyakati zile kama ambavyo hakutaka mfumo wa vyama vingi baada ya uhuru lakini baadaye akawa wa kwanza kuikemea CCM kutokuwa tayari kukaribisha mageuzi. Mwalimu alishaanza kutambua kuwa ndoto yake ya serikali moja haiwezi tena kutimia.

Mwalimu pole pole alianza kuwa na wasi wasi na chama alichokiasisi yeye mwenyewe na hata mara moja hakuficha hisia zake kuhusu manyang'au walioiteka CCM. Usemi wa "CCM si mama yangu" ni ushadhidi tosha kuwa hakuafiki gari la CCM lilikokuwa likielekea na alikuwa anasubiri tu kituo muafaka aweze kushuka. Mwalimu kuitelekeza CCM? CCM bila Mwalimu? Hiyo haingewezekana, manyang'au hawangebaki salama...ni ama wao au Mwalimu!

Nina hakika alipo Mwalimu, anapoliangalia hili toto tundu, anatabasamu kwa sababu alijua ni swala la muda ukweli lazima utajulikana tu muda wake ukiwadia. Na huo muda umewadia, asante Tume ya Katiba, asante Tundu Lisu na asante Watanzania waliotoa maoni yao. Muda muafaka wa serikali tatu umewadia na kama ilivyokuwa kwa mageuzi, Mwalimu angekuwepo angewakumbusha CCM kwamba si dhambi tena kuongelea serikali tatu.

Mkuu Mag3,

Nimerejea kama nalivyokuahidi na nimekusoma vyema, kwa hayo maelekezo yako mareefu!

Kuna baadhi ya hoja nzito ulizozungumzia kwenye bayana yako,lakini naona umetumia hypotheticals!? Lakini haian neno!

Pia nimejaribu kukufahamu hizo grievances ulizonazo dhidi ya hao Wanasiasa/Viongozi wetu waliomo ndani ya CCM!?

Kwa context hiyo naona mnatafautiana kabisa na Mzee Mtei!? Daah! Pia nakhis labda ndo jambo jema!?

Mangi ulonena naona umekua-defensive mno!?...yaani nalitaka kutumia hoja/maneno makali,lakini umenifanza nasita kiduchu! Daah! Teeh! Teeh! Teeh!

Binafsi, nafikiri yakua yule Tundu Lissu aliyoyasema takriban mangi mno ni kweli tupu!

Tatizo linakuja yakua Watanzania takriban woote hawajazoeshwa kusikia ukweli juu ya yule Nyerere au kashfa zake zikianikwa hadharani kama vile....au mara kwa mara!?

Yaani Watanzania wameishi/wanaishi kwa kuabudu tu ile myth ya Nyerere...lakini sio Nyerere mwenyewe khalis! Yaani kwa mfano kiduchu, sio Nyerere kama yule alienyambuliwa na Tundu Lissu!?

Jangine kiduchu...labda pia ile approach alotumia yule Tundu Lissu katika ku-articulate zile hoja zake pale Bungeni,ndio pia imeleta khitilaf!? Yaani badala ya kujikita zaidi kwenye lugha ya kitaaluma/kiungwana...yeye alitumia maneno na tashtit za vinyozi au... taarabu za "Uwanja wa fisi"!? Daah!

Yeye Tundu Lissu,sidhani kama alitilia maanani ile sensitivity ya jina la yule Nyerere ndani ya mioyo ya Watanzania wengi mno walio misukule ya Nyerere mpaka kesho!? Daah!...hii bila ya kujali makosa yoyote yale au udhalimu uliofanywa na yule Nyerere!

Nafikiri umefika wakti muafaka sasa kwa Watanzania kujifunza kuweka mijadala ya wazi na ukweli....bila ya kutumia mihemuko ya kisiasa,kidini au hata makabila!?

La muhimu tu ni kuhakikisha yakua tunajitahidi kutumia lugha njema ili kufikia miafaka, ndani ya mijadala yetu yenye kulenga tija kwa Taifa...au hata mingineyo!?

Niwia radhi kama pana lolote/chochote labda nimenena hapa, nawe labda kimekukera!?

Nakutakia jioni njema na tutazungumza zaidi, penye uhai na majaaliwa!

Ahsanta.
 
Lissu amejipoteza kwenye siasa za Tanzania kwa kumtusi Nyerere na amezidi kuizamisha chadema kwenye ramani ya siasa za bongo...ni suala la muda tu..subirini upepo upite

mambo ya upepo kupita yako ugambani tu CDM ni facts mkuu.
 
Alichokiongea Lisu hakukitunga yeye ila alitumia rejea mbalimbali kwa hiyo hapaswi kulaumiwa. Ila kama angezungumza mambo aliyoyatunga yeye binafsi bila kurejea popote, basi angepaswa kulaumiwa. Mimi pia sifurahishwi na vitendo vya kuwadhalilisha viongozi na hasa waasisi, ila kama kwa jambo kubwa tena lenye manufaa kwa Taifa, haina chaguo maana ni bora uukate mkono wako ili kuunusuru mwili wako wote usiangamie.
 
Watanzania ni maarufu sana kwa UNAFIKI uliotukuka, kutamka na kuonesha makosa ya mtu ndio kumtukana; na zile zilikuwa ni rejea alizofanya ya nyerere ikiwa ya 4, kwa nini hizo nyingine zionekane zi sawa ya nyerere ndo si sawa; Enyi kizazi cha nyoka Acheni unafiki. Niliuliza hapa na sasa nawaulizeni tena; Kati ya Prof Shivji ktk kitabu chake au Dr mwakyembe ktk paper yake wakionesha na kukubali serikali 3, na Tundu Lisu nani alianza kumkosoa mwl kwenye dhana hii ya muungano? Kama wajua jibu utakubaliana na mm kuwa lisu ni wa mwisho. Hao nao wamemtukana nyerere ktk maandiko yao? Jibuni hili acheni kusema bila kuonesha uwiano wa statement zenu
 
mbona waislam na wazenj wanamtukana kila siku..tena makada wa CCM..Faiza FOX mwenyewe kamtukana sana Nyerere humu ndani....mbona waislam..wanamkufuru na kumtukana si Nyerere Tuu hadi YESU humu ndani na mitaani..sasa mnaishia singizia kutukanwa..si myasem ahayo matusi.
 
Mkuu kuna watu wanamwona Nyerere ka mungumtu vile.. Yaani hawaamini kwamba angeweza kufanya makosa. Naona hata hotuba zake hawasikilizi kwa sababu yeye mwenyewe anakiri kwamba kuna makosa walifanya kwani hawakuwa malaika. Sasa mtu anapokuja na hoja kwamba huwezi kumsema akimlinganisha na Lincoln....yeye nani asisemwe, asikosolewe??!!. Kama Lisu ktukana hata mimi siafiki na wala sishabikii hilo... Lakini kumsema, kumkosoa hiyo sawa kabisa.

Hao CCM wenyewe wanaojifanya wanamheshimu Mwalimu hata sijui ni kipi wanachomheshimia maana alichokuwa anakataza Chama kuendeshwa na wenye fedha sio kinachofanyika leo, ufisadi na uhuni ndani ya CCM ya leo ndio dini, CCM wawe wakweli wa nafsi zao kuwa wameacha maadili ya Mwalimu zamani sana wasijifanye kutuhadaa kisa Lissu amekosoa mambo kadhaa aliyofanya Mwalimu, ni kweli mkuu heshima ya Mwalimu itabaki pale pale lakini haitoi ukweli kuwa naye alikuwa binadamu.
 
Bw.Tundu sio mtu intelligent kama watu wengi wanavyodhania, kwa maana mtu intelligent huwa ana uwezo wa kujua madhara ya kile anachokisema kabla hajakisema!

Mtu intelligent yoyote anapaswa kufahamu ktk Nchi kama TZ hauwezi kuanzisha Vita dhidi ya Mlm.Nyerere na ukashinda hata uwe nani, hata Raisi wa nchi leo hii akianzisha Vita dhidi ya Mlm.Nyerere hawezi kushinda mwishowe kuna mtu tu anaweza hata akajitoa mhanga kumlipua!

Ni sawa naleo hii Marekani mwanasiasa aanzishe Vita dhidi ya sijui Raisi Washington au Lincoln hawezi kushinda hata iweje hata kama huyo Mwanasiasa yuko sahihi kwa kiasi gani, vile vile kama ilivyo pia hakuna Mwanasiasa AK leo hii ambaye anaweza akaanzisha Vita dhidi ya Bw.Mandela na akashinda hata kama atakuwa sahihi kwa kiasi gani, na ndio maana utaona Wanasiasa wenye akili linapofika kwenye swala la hawa watu huwa wanakuwa waangalifu sana wawe ni Demokrats au Republikan hakuna anayethubutu kuwaongelea na kuwakashifu Lincoln hata kama walifanya makosa kiasi gani kwa maana wanafahamu kwamba hawa Watu nafasi yao imeshaandikwa kwenye Historia na huwezi kuifuta bila kukugharimu...

Bw.Tundu alipaswa aelewe kwamba hata kama Mlm.Nyerere amekosea kwa kiasi gani hakupaswa kumuongelea vile, alipaswa aelewe kwamba kuna watu wako tayari kufa kumtetea Mlm.Nyerere na hiyo ni Nchi nzima kuanzia jeshini mpaka Utingo wa daladala...

Nakuunga mkono mia kwa mia
 
nashukuru kwa ufafanuzi wako una ukweli, lakini ninachokiona kwenye hoja ya Lisu ilikuwa ni kushindana na chama tawala na sio nyerere per se. TL hakuibuka tu na noja ya nyerere hivihivi, nadhani ni vile baadhi wanavyotaka kumwelewa sivyo tundu lisu alichotaka kumaanisha.Tundu lisu alipeleka hoja ya serikali 3 ipite na sio mafaili ya nyerere. Ikabidi atumie hoja za kumuhusu nyerere akilenga kupangua uwepo wa serikali 2. na hii ilitokana na chama tawala kutumia mgongo (hoja) za nyerere kutetea serikali 2 na kupinga serikali 3.

I know kuna watu duniani ni sensititive sana ikitokea kuna neno umetamka wanashikilia hapo na kupuuza hoja zote ulizosema kabla hata kama zinauzito kiasi gani. Hii ni kawaida.Na hii pengineTundu lisu pengine alitakiwa ajue na azingatie. Mimi sio fan wa chama chochote lakini TL nimemwelewa kama ninavyowaelewa CCM na serikali zao mbili wanavyozijengea hoja.

Angalizo ni kuwa CCM wajue katiba itakayotungwa ihakikishe inadumu miaka 50 tena kama haitakuwa hivyo basi whahakikishe kuwa wataendelea kutawala nchi hii milele, kama wataendelea kutupia hoja dubious ni wazi kuwa siku wakiondoka na kikaingia chama kingine kinaweza hata kuwadhohofisha hao waasisi vibaya kuliko walivyojengeka na huo muungano ukawa Hadithi za alinacha.
 
Back
Top Bottom