Mshume Kiyate
JF-Expert Member
- Feb 27, 2011
- 6,764
- 896
Mkuu Mag3.Duh gombesugu, kwanza mimi kama utakuwa tayari kujadiliana na mimi bila kuingiza Udini, hapo tutaongea lakini mnapoingia kwenye Udini, huko hutaniona. Usitegemee kuona mchango wowote kutoka kwangu unaogusia imani ya watu, huko hunikuti hata kwa dawa! Hayo nawaachia wachochezi wanaoamini wana undugu na wakoloni na walowezi waliotuletea mila zao wakiziita dini kuliko sisi ndugu zao Watanzania.
Pili niliwahi kuelezea historia yangu kidogo lakini naona umesahau, mimi ni Mtanzania kwanza ndio mambo mengine yanafuatia. Sijawahi kujiunga na chama chochote cha siasa toka nizaliwe (tafadhali amini hilo) ila kwa kweli siipendi na wala sijawahi kuipenda CCM maishani. Kidogo nijiunge na NCCR Mageuzi mwaka 1994 lakini alipoingia Augustino Mrema akitokea CCM na kupewa uongozi, mimi huyoo...nikarudi kwenye ganda langu.
Unao uhuru wa kunihusisha na Bavicha ingawaje kwa umri wangu nadhani Bavicha ni kwa wajukuu zangu na hata hiyo Chadema naisikia tu ingawaje nawaunga mkono dhidi ya ufashisti na ukoloni mamboleo wa CCM. Sijawahi kuyumba katika msimamo wangu na naamini suluhisho pekee katika kuutatua huu muungano wa kero ni mfumo wa serikali tatu na ingawa serikali moja ingefaa zaidi, mimi siyo dreamer niko down to earth.
Kuhusu lugha yangu ya kwanza ni kwamba nilianza kuongea Kiswahili nikiwa na umri wa miaka mitano na ukweli ni kwamba nakielewa Kiswahili kuliko lugha yoyote ile, asante zimuendee Mwalimu Nyerere! Hata hivyo naunga mkono rasimu kama ilivyotolewa na Tume ya Katiba ikiongozwa na Jaji Joseph Sinde Warioba pamoja na maelezo aliyoyatoa Mh. Tundu Lisu ndani ya Bunge Maalum la Katiba kuhusu mfumo wa serikali tatu.
Upepo wa Mageuzi ukiwa umeshika kasi miaka ya 1990, kiongozi mojawapo wa Mageuzi akiitwa Mabere Nyaucho Marando bila kujua msimamo wa Mwalimu Nyerere alitoa kauli iliyodai Mwalimu kafilisika kisiasa. Taifa zima lilikuwa kama limepigwa radi! huyu kijana kathubutuje kutoa kauli kama hiyo! Woga mkubwa ulitanda ndani ya taifa na Marando akajikuta ametengwa na ndugu na marafiki..hakuna aliyetaka kukaa karibu yake.
Tofauti na walivyoamini wahafidhina ndani ya CCM wakiongozwa na Raisi Mwinyi, Waziri Mkuu Malecela, Waziri wa Mambo ya Ndani Agustino Mrema walioamua kuendesha operation ya kanyaga sisimizi, Mwalimu bila kuwaonea haya alitamka kwamba kuongelea vyama vingi si dhambi. Akawatahadharisha CCM kuwa wajiandae kwani hawataweza kuuzuia upepo wa mageuzi. Huyo ndiye Mwalimu, alienda na wakati, alisoma alama za Nyakati.
. T
Leo hii angekuwepo angewashangaa hawa malimbukeni wanaomnyooshea kidole Mhundu Lisu. Yawezekana Mwalimu alikuwa na sababu zake za kutotaka Muungano uhojiwe nyakati zile kama ambavyo hakutaka mfumo wa vyama vingi baada ya uhuru lakini baadaye akawa wa kwanza kuikemea CCM kutokuwa tayari kukaribisha mageuzi. Mwalimu alishaanza kutambua kuwa ndoto yake ya serikali moja haiwezi tena kutimia.
Mwalimu pole pole alianza kuwa na wasi wasi na chama alichokiasisi yeye mwenyewe na hata mara moja hakuficha hisia zake kuhusu manyang'au walioiteka CCM. Usemi wa "CCM si mama yangu" ni ushadhidi tosha kuwa hakuafiki gari la CCM lilikokuwa likielekea na alikuwa anasubiri tu kituo muafaka aweze kushuka. Mwalimu kuitelekeza CCM? CCM bila Mwalimu? Hiyo haingewezekana, manyang'au hawangebaki salama...ni ama wao au Mwalimu!
Nina hakika alipo Mwalimu, anapoliangalia hili toto tundu, anatabasamu kwa sababu alijua ni swala la muda ukweli lazima utajulikana tu muda wake ukiwadia. Na huo muda umewadia, asante Tume ya Katiba, asante Tundu Lisu na asante Watanzania waliotoa maoni yao. Muda muafaka wa serikali tatu umewadia na kama ilivyokuwa kwa mageuzi, Mwalimu angekuwepo angewakumbusha CCM kwamba si dhambi tena kuongelea serikali tatu.
Nona umefika mbali mpaka kumtusi Mzee wetu wa Chadema muasisi jambo hili alikubaliki kabisa au umetumwa.
By Edwin Mtei![]()
![]()
Nilisikiliza Mheshimiwa Tundu Lissu na nasikitika kwamba sikubaliani naye jinsi alivyoeleza shutma juu na dhidi ya Mwalimu Julius Nyerere, Baba na Muasisi wa Taifa letu. Inajulikana na umma wa Watanzania, kwamba mimi binafsi, kama Waziri wa Fedha, nilitofautiana na Mwalimu, nikajiuzulu Uwaziri Decemba,1979, nikimwomba ateuwe Mtanzania mwingine atakayeshauri mambo ya Uchumi na Fedha. Lakini tuliendelea kuwasiliana kwa maelewano bila chuki, na hata aliniteuwa niwe Mwakilishi wa Tanzania na Afrika inayoongea Kiingereza katika IMF (Shirika la Fedha Duniani) chini ya miaka mitatu baadaye Novemba, 1972. Nimekuwa na mawasiliano na maelewano mazuri sana na Mwalimu hata baada ya kuasisi CHADEMA, Julai 1992 na tulipokamilisha Katiba na Sera za Chadema, nilimtembelea Nyumbani kwake Butiama nikampa azisome ajionee jinsi tulivyonuia kuwahudumia Wananchi wetu. Hata siku moja siwezi kumtusi Muasisi wa Taifa letu. Iwe ni mwiko pia kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kumtusi Baba wa Taifa.
Ningewashauri uongozi wa Chadema na hasa Vijana wa M4C (Vuguvugu la Mabadiliko) tuendelee na uhamasishaji : kwa umakini, tukiwa na huruma kwa wanyonge maskini wa kutupwa, tukijiandaa kwa umakini na kiutaalamu Sera na Mikakati ya kuwakomboa toka katika umaskini wa kutupwa kwa kutumia nguvu ya umma (Peoples Power) tukitumia mikakati sahihi: kwani Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke: Mikakati na Sera sahihi ikiwa ni kutumia misingi ya Uchumi na Miundombinu tulionayo licha ya uhalisia dhoofu tulioridhi; tukiwaenzi walioijenga na kuturidhisha kwa unyofu wao. Roho ya Julius Nyerere ilale mahala pema Peponi. Amen!
With all due respect to Hon. Tindu Lissu, this smacks BAD TASTE.
Edwin Mtei
Founder Chairman of CHADEMA.
Angalia hapo nilipokoleza wino mwekundu.
cc gombesugu
Last edited by a moderator:
