Kaandika Bibi Happy
MBOWE NI NANI?
Kwa hiyo Mbowe ni Kamati kuu ya CHADEMA? Au Mbowe aishurutishe kamati kuu?
Ngoja kwanza....
Kwamba Mdee alivunjika akiwa anazungumza na Mbowe? Au Bulaya ALIPIGWA na Mbowe hadi akazimia? Au Matiko alilazwa kisa alifumwa na Mbowe? Yaani MBOWE ni nani jamani hata hakamatiki akipiga hawa wanawake?
Kwamba Nusrat aliwekwa mahabusu na Mbowe sio? Kwamba Mbowe alimweka huko ili afie magereza? Wow! Kwamba Mbowe ANAMILIKI magereza, mahakama na wanasheria wote? Wow!
Sasa mkuu, mbona sijaelewa? Kwamba wabunge hawa wapewe nafasi kwa kuwa MBOWE amewanyanyasa? Kwamba ofisi ya BUNGE inawatambua kwa kuwa ndiyo ILIYOAMUA wapewe nafasi hizo?
Kama kweli wabunge hawa HAWAKUJITEUA na walitokana na uteuzi RASMI toka CHADEMA, je, haimaanishi kwamba CHADEMA ILIWAJALI? Kwa nini CHADEMA iwape nafasi halafu IWAFUKUZE uwanachama?
Je, kauli zako hizi zinathibitisha kuwa hawa wabunge HAWAKUTEULIWA na CHADEMA?
Nani aliyemtoa NUSRAT mahabusu? Kama ni CHADEMA ILIMTOA ILI AKAAPE, kwa nini huoni hili ni jambo jema? Kama CHADEMA walimtoa huko mahabusu, unataka kusema CHADEMA ndio wana nguvu ya kumtoa mahabusu yeyote wanayetaka? Hii inaleta picha gani kwa huu mhimili mkuu wa serikali?
Kwamba ALIYEMTOA Nusrat ili akaapishwe, alikuwa ANAMWEPUSHA na unyanyasaji ambao MBOWE aliufanya?
Basi, ni NANI huyo ALIYEMTOA AKAAPE ILI ASIFIE MAGEREZA kama alivyotaka Mbowe ?
Bado najiuliza, MBOWE NI NANI KATIKA NCHI HII? Spika anamlalamikia tu, hata hamfanyi kitu.
Aliyeelewa anieleweshe...
Its so confusing.