Bwana Ndugai anahitaji msaada wa haraka wa saikolojia

Bwana Ndugai anahitaji msaada wa haraka wa saikolojia

Bwana Ndugai anahitaji msaada wa haraka wa saikolojia.

Malisa GJ

Mosi; Huu uchungu anaouonesha Ndugai sio wa Mzee Halima na wenzake kupigwa, ni uchungu wa kupoteza yale matrilioni ya wafadhili. Ameshaona dalili zote kwamba hata akiwalinda akina Mzee Halima na wenzake waendelee kuwa wabunge, wafadhili wanaweza kugomea kutoa yale matrilioni.

Pili; Mzee Halima na wenzake hawakupigwa kwa ajili ya Mbowe. Walipigwa kwa sababu ya kutetea haki zao. Walipotolewa Segerea askari magereza waliwapiga kama vibaka kwa sababu tu walienda kupokelewa na wafuasi wao. Mashinji alipokelewa na msafara wa wafuasi wa CCM wakiongozwa na Chakubanga lakini hakupigwa. Double standards. Kama kweli Ndugai ana uchungu angewakemea wale askari waliofanya unyama ule sio Mbowe.

Tatu; Mzee Halima na wenzake hawajafukuzwa bila kusikilizwa. Walipewa haki ya kusikilizwa (audi alteram partem) lakini wakakataa kuitumia. Waliitwa kwa maandishi kwenye kamati kuu ili wasikilizwe wakagoma. Sasa Bwana Ndugai alitaka chama kifanyeje? Hata mahakamani mtuhumiwa akikataa kujitetea bila sababu za msingi, mahakama hulazimika kuamua kwa kusikikiza upande mmoja.

Nne; Maamuzi ya Chadema hayakufanywa na Mbowe. Yalifanywa na Kamati kuu ambayo ina wajumbe zaidi ya 40. Ni ujinga kuamini wajumbe wote hawakua na sauti isipokua Mbowe peke yake. Ndugai elewa kwamba Mbowe sio kamati kuu ya Chadema.

Tano; kumbe Ndugai anajua Mzee Halima na mwenzake walipigwa hadi wakazimia pamoja na kuvunjwa mikono na askari magereza? Unyama huu aliwahi kuulaani popote? Aliwahi kumuita Kamishna Mkuu wa Magereza kwenye kamati za bunge ajieleze kwanini Askari wake walifanya unyama ule tena kwa wabunge wanawake? Au aliona ni sawa tu kwa sababu walikua Chadema. Leo wamefurushwa ndio anasikia uchungu.

Huu utaratibu wa mtu kuonewa lakini unakaa kimya kwa sababu sio wa chama chako sio ubinadamu kabisa. Ningemuona Ndugai ana hoja kama angekemea tukio lilipotokea. Sasa Mzee Halima ameshapona na kusahau ndio Ndugai anasikia uchungu leo? Haina tofauti na mkeo kulia kwa uchungu na kukuomba msamaha kwa sababu ya vita vya majimaji eti babu yake alishirikiana na wakoloni kuwapiga wazawa. Wendawazimu.!
Ndugai anajua anachokifanya , kufanya kazi na Jiwe lazima ujitoe fahamu uweke fahamu za bandia .
 
Hakuna spika
Tanzania tuna spika hewa.

Ile siku bwana mdogo Ndugai anamuapisha Polepole lakini anaongelea mambo ya Chadema na kusema kuna "unyanyasaji wa kijinsia" akiwatumia akina Halima Mdee kama Mfano. Halima anafanya press yake na kusema Chadema hakuna mfumo dume kama inavyoelezwa, maana wao wamekuwa viongozi huko. Ndugai anajionaje?
 
Ndugai hana akili

Anachopaswa kujua ni kuwa kuna njia 2 za mtuhumiwa kutoka gerezani

1. Kwa amri ya Mahakama

2. Kwa msamaha wa Raisi

Endapo DPP ataona hana nia ya kuendelea na kesi na anataka kumuachia mtuhumiwa aliyepo gerezani ni lazima aende kwanza kuitaarifu mahakama na mahakama ndo inatoa amri ya kumtoa mtuhumiwa gerezani. DPP hana mamlaka ya kumtoa mtuhumiwa gerezani , ni lazima apitie kwa mahakama.

Kwa upande wa Raisi yeye ndo pekee mwenye amri ya kumtoa mtuhumiwa au mfungwa gerezani.
Kwa suala la Nusrat ni hekima kwa Ndugai kuchutama maana hili suala limewavua nguo. Nusrati hata kama kulikuwa na nole ya DPP lakini hakukuwa na amri ya mahakama ya kumtoa gerezani.

Kwa upande wa Raisi hakuna popote Raisi alipotoa amri ya kuachiwa kwa Nusrat.

Hivyo Ndugai aambiwe, achutame tu. Wako uchi
Rais husamehe waliokwishahukumiwa na mahakama.
Kama ni mtuhumiwa, hawezi kumtoa kwa amri/msamaha wa moja kwa moja, atatumia njia ya kisheria ya kupitia DPP
 
Inakuwaje Spika badala kutoa ufafanuzi wa kilichotokea na matakwa ya kisheria amekazia kuleta ushonganishi wa kijinsia kama kwamba ndio tatizo.Yaani Mobwe na chama chake walichofanya si sahihi kwa vile wamewatendea akina dada na hata kama kikatiba ya chama chao wametenda sawa. Ameng'ang'ania kuwa wataendelea kuwa waabunge,kwa kigezo gani ?.Ni ubabe au ni matakwa ya kikatiba.
Halima Mdee wakirudishwa chamani watakuwa vidudu mtu na wataleta madhara chini kwa chini kuliko huo usaliti wa mwanzo.
 
Mkoa

Mimi huyu mgogo nilikuwa nimempa job namlipa vizuri tu,mwisho Wa siku akaniambia anatakiwa arudi nyumbani Mdogo wake kafaulu LA saba shule ya kata iko mbali kidogo na kwao,kwa hiyo amepangisha chumba ,anatakiwa awe anamchotea maji.
Mgogo akaacha ajira
Ndoyo maana omba omba wengi ni wagogo
 
Bwana Ndugai anahitaji msaada wa haraka wa saikolojia.

Malisa GJ

Mosi, Huu uchungu anaouonesha Ndugai sio wa Halima na wenzake kupigwa, ni uchungu wa kupoteza yale matrilioni ya wafadhili. Ameshaona dalili zote kwamba hata akiwalinda akina Mzee Halima na wenzake waendelee kuwa wabunge, wafadhili wanaweza kugomea kutoa yale matrilioni.

Pili, Halima na wenzake hawakupigwa kwa ajili ya Mbowe. Walipigwa kwa sababu ya kutetea haki zao. Walipotolewa Segerea askari magereza waliwapiga kama vibaka kwa sababu tu walienda kupokelewa na wafuasi wao. Mashinji alipokelewa na msafara wa wafuasi wa CCM lakini hakupigwa. Double standards. Kama kweli Ndugai ana uchungu angewakemea wale askari waliofanya unyama ule sio Mbowe.

Tatu, Mzee Halima na wenzake hawajafukuzwa bila kusikilizwa. Walipewa haki ya kusikilizwa (audi alteram partem) lakini wakakataa kuitumia. Waliitwa kwa maandishi kwenye kamati kuu ili wasikilizwe wakagoma. Sasa Bwana Ndugai alitaka chama kifanyeje? Hata mahakamani mtuhumiwa akikataa kujitetea bila sababu za msingi, mahakama hulazimika kuamua kwa kusikikiza upande mmoja.

Nne, Maamuzi ya Chadema hayakufanywa na Mbowe. Yalifanywa na Kamati kuu ambayo ina wajumbe zaidi ya 40. Ni ujinga kuamini wajumbe wote hawakua na sauti isipokua Mbowe peke yake. Ndugai elewa kwamba Mbowe sio kamati kuu ya Chadema.

Tano, kumbe Ndugai anajua Halima na mwenzake walipigwa hadi wakazimia pamoja na kuvunjwa mikono na askari magereza? Unyama huu aliwahi kuulaani popote? Aliwahi kumuita Kamishna Mkuu wa Magereza kwenye kamati za bunge ajieleze kwanini Askari wake walifanya unyama ule tena kwa wabunge wanawake? Au aliona ni sawa tu kwa sababu walikua Chadema. Leo wamefurushwa ndio anasikia uchungu.

Huu utaratibu wa mtu kuonewa lakini unakaa kimya kwa sababu sio wa chama chako sio ubinadamu kabisa. Ningemuona Ndugai ana hoja kama angekemea tukio lilipotokea. Sasa Halima ameshapona na kusahau ndio Ndugai anasikia uchungu leo? Haina tofauti na mkeo kulia kwa uchungu na kukuomba msamaha kwa sababu ya vita vya majimaji eti babu yake alishirikiana na wakoloni kuwapiga wazawa. Wendawazimu!
Nahofia sana neno "ndugai" kuja shabihiana na "kihiyo" maana matukio huwafanya watu waunde misamiati mipya.
 
Mwendawazimu namba moja anaamua wendawazimu wengine waongee au kufanya nini.
 
Back
Top Bottom