Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Uliza jambo kama hulijui. Kuwashwa kwa mtambo hakuna uhusiano wowote na maji kufurika katika vijiji vilivyopo chini ya Bwawa. Ni kwa Bwawa limejaa na linatishia kuvunja kingo hivyo ni kawaida maji yanapojaa kupita kiasi kufunguliwa kiasi ili yapungue kwa ajili ya usalama wa kingo za bwawa. Hata Mtera na Kidatu maji yakijaa kupita kiasi huwa yanafunguliwa kwa utaratibu ili kunusuru bwawa kupasuka. Hivyo, hayo maji hayatokani na kuwashwa kwa mtambo.Juzi niliona katika taarifa ya habari ya ITV wananchi wa vijiji mbalimbali bondeni mwa Bwawa la Mwalimu Nyerere wakihaha kuokoa maisha yao baada ya kuzingirwa na maji ya mto Rufiji. Hii inatokana na kujaa kwa bwawa hivyo kulazimisha kufungulia maji kutoka bwawani.
Pia tumekwisha fahamishwa kuwa mtambo mmoja kati ya tisa ya kuzalisha umeme bwawani hapo umewashwa na kuzalisha MW 235. Kwa hiyo bado mitambo nane ambayo baada ya kukamilika kufungwa itawashwa na bwawa kuanza kuzalisha MW 2115. Hakika ni jambo jema sana.
Wasiwasi ni kuwa kama kuwashwa kwa mtambo mmoja tu kumesambaratisha wanavijiji na kuanza kuhama makazi yao, hali itakuwa vipi pale mitambo yote tisa itakapowashwa? Je, vijiji vilivyopo bondeni mwa Bwawa vitaendelea kuwepo? Je, wananchi wamekwisha taarifiwa lo lote kuhusu hali ya baadaye ya makazi na mashamba yao?
Ikumbukwe kuwa mitambo yote itakapokuwa inafanya kazi hakutakuwa na kupungua maji tena kwa kuwa maji yatafunguliwa kwa kiwango kile kile mwaka mzima.
Soma hoja siyo kudandia! Sijasema kuwashwa kwa hicho kinu kimoja kumesababisha mafuriko! Lini ulisikia kufunguliwa kwa Mtera na Kidatu kumesababisha mafuriko?Uliza jambo kama hulijui. Kuwashwa kwa mtambo hakuna uhusiano wowote na maji kufurika katika vijiji vilivyopo chini ya Bwawa. Ni kwa Bwawa limejaa na linatishia kuvunja kingo hivyo ni kawaida maji yanapojaa kupita kiasi kufunguliwa kiasi ili yapungue kwa ajili ya usalama wa kingo za bwawa. Hata Mtera na Kidatu maji yakijaa kupita kiasi huwa yanafunguliwa kwa utaratibu ili kunusuru bwawa kupasuka. Hivyo, hayo maji hayatokani na kuwashwa kwa mtambo.
Mi nimekaa zangu hapa pembeni😀Soma hoja siyo kudandia! Sijasema kuwashwa kwa hicho kinu kimoja kumesababisha mafuriko! Lini ulisikia kufunguliwa kwa Mtera na Kidatu kumesababisha mafuriko?
Iko hivi, maji "yaliyofunguliwa" hayatumiki kuzungusha huo mtambo bali yanatoka huru ili kupunguza ujazo bwawani, yanayopita kwenye huo mtambo uliowashwa yanaendelea na safari ya kawaida mtoni kama njia zake zilivyowekwa, hivyo wakiwasha mitambo yote tisa maji hayatafunguliwa kupunguza ujazo bali yatapita kwenye turbines zote na kuendelea na safari ya baharini kama kawaidaWewe nadhani huelewi hoja! Ili turbines zizunguke unatakiwa ufungulie maji katika mahandaki yake. Maji yakisha zungusha hizo turbines yanaendelea katika mkondo wake na kutumika katika shughuli nyingine. Kwa sasa wamefungulia handaki moja ukichanganya na yaliyofunguliwa kupunguza maji bwawani yamesabisha mafuriko. Hoja ni kuwa kama handaki moja limeleta tafrani, vipi mahandaki yote tisa yakifunguliwa.
Ni muhimu nchi iwe na umeme wa kutosha uchumi ukue na hao waliokuwa pembezoni mwa mto wahame .
Maji yaliyofunguliwa ni mengi kuliko maji yatayotumika kusukuma mitambo yote TisaNajaribu kuwaza uwezo wako wa kuelewa! Maji yamefunguliwa kwa sababu Bwawa limejaa ili kupunguza maji. Lakini pia kuna maji yameelekezwa katika kuendesha mtambo uliowashwa. Hii imesababisha mafuriko bondeni. Sasa hoja hapa ni kuwa je maji yakifunguliwa kuwasha mitambo yote tisa hali ya mafuriko itakuaje?
Kabla ya kujengwa bwawa maji yalikuwa yanapita wapi? Wakizidiwa na maji tutawahamishia msomeraKila mtambo unahitaji kiasi fulani cha maji ili ufanye kazi. Kwa sasa wamefungulia maji kwa mtambo mmoja na tayari mashamba ya wanavijiji yamefurika na watu kuhama makazi yao. Kwa hiyo maji yataendelea kuongezeka kadri mitambo inavyowashwa.
Kwa hiyo kama mitambo yote ingekuwa inafanya kazi bado maji yangefunguliwa na hivyo mafuriko yangetokea!Maji yaliyofunguliwa ni mengi kuliko maji yatayotumika kusukuma mitambo yote Tisa
Tayari walishapewa elimu nzima kuhusu kinachoendelea!
Tusibiri Lema na Mdude kwanza wanasemaje kuhusu hili jamboJuzi niliona katika taarifa ya habari ya ITV wananchi wa vijiji mbalimbali bondeni mwa Bwawa la Mwalimu Nyerere wakihaha kuokoa maisha yao baada ya kuzingirwa na maji ya mto Rufiji. Hii inatokana na kujaa kwa bwawa hivyo kulazimisha kufungulia maji kutoka bwawani.
Pia tumekwisha fahamishwa kuwa mtambo mmoja kati ya tisa ya kuzalisha umeme bwawani hapo umewashwa na kuzalisha MW 235. Kwa hiyo bado mitambo nane ambayo baada ya kukamilika kufungwa itawashwa na bwawa kuanza kuzalisha MW 2115. Hakika ni jambo jema sana.
Wasiwasi ni kuwa kama kuwashwa kwa mtambo mmoja tu kumesambaratisha wanavijiji na kuanza kuhama makazi yao, hali itakuwa vipi pale mitambo yote tisa itakapowashwa? Je, vijiji vilivyopo bondeni mwa Bwawa vitaendelea kuwepo? Je, wananchi wamekwisha taarifiwa lo lote kuhusu hali ya baadaye ya makazi na mashamba yao?
Ikumbukwe kuwa mitambo yote itakapokuwa inafanya kazi hakutakuwa na kupungua maji tena kwa kuwa maji yatafunguliwa kwa kiwango kile kile mwaka mzima.
Duh! Mnyalu unajiaibisha kweli. Ina maana huelewi kabisa mabwawa ya kuzalishia umeme yanavyofanya kazi?Kwanini yaongezeke?