Bwawa la Mwalimu Nyerere na athari kwa vijiji vilivyopo bondeni mwa bwawa hilo

Haiwezekani kuwa sababu ni kuwashwa mtambo mmoja lazima sababu itakuwa ni mvua chini au juu ya bwawa. Ikiwa maji yamejaa bwawani na mvua zinazidi inabidi wafungulie maji yamwagige na hii athari hata lisingekuwepo bwawa ingekuwepo.
 
Uliza jambo kama hulijui. Kuwashwa kwa mtambo hakuna uhusiano wowote na maji kufurika katika vijiji vilivyopo chini ya Bwawa. Ni kwa Bwawa limejaa na linatishia kuvunja kingo hivyo ni kawaida maji yanapojaa kupita kiasi kufunguliwa kiasi ili yapungue kwa ajili ya usalama wa kingo za bwawa. Hata Mtera na Kidatu maji yakijaa kupita kiasi huwa yanafunguliwa kwa utaratibu ili kunusuru bwawa kupasuka. Hivyo, hayo maji hayatokani na kuwashwa kwa mtambo.
 
Soma hoja siyo kudandia! Sijasema kuwashwa kwa hicho kinu kimoja kumesababisha mafuriko! Lini ulisikia kufunguliwa kwa Mtera na Kidatu kumesababisha mafuriko?
 
Kama wananchi wanapata athari ni vyema wakawalipa fidia
 
Wajichunge siku lisije poromoka😷 waweke mpango mzuri maana maji huwa yananguvu na ujenzi wetu huwa janja janja nimingi kila miradi watu lazima wapige iyo piga uwa laziiima....
 
Iko hivi, maji "yaliyofunguliwa" hayatumiki kuzungusha huo mtambo bali yanatoka huru ili kupunguza ujazo bwawani, yanayopita kwenye huo mtambo uliowashwa yanaendelea na safari ya kawaida mtoni kama njia zake zilivyowekwa, hivyo wakiwasha mitambo yote tisa maji hayatafunguliwa kupunguza ujazo bali yatapita kwenye turbines zote na kuendelea na safari ya baharini kama kawaida

Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
 
Maji yaliyofunguliwa ni mengi kuliko maji yatayotumika kusukuma mitambo yote Tisa
 
Hao watakuwa wameshajulishwa kinachoendelea. Kama bado mashirika ya sheria za mazingira yaende kuwasaidia kisheria. Sie tunataka umeme tu.
 
Samahani jamani, kuuliza si ujinga.

Kwa hali iliyopo hivisasa yaonekana maji kusimama ama kupungua mto Rufiji, Ninapotaka kujua kuwa je yatafunguliwa tena?

Samahani mwenye ufahamu sahihi kutoka huko kwenye chanzo cha maji haya (STIGO) naomba anisaidie
 
Kila mtambo unahitaji kiasi fulani cha maji ili ufanye kazi. Kwa sasa wamefungulia maji kwa mtambo mmoja na tayari mashamba ya wanavijiji yamefurika na watu kuhama makazi yao. Kwa hiyo maji yataendelea kuongezeka kadri mitambo inavyowashwa.
Kabla ya kujengwa bwawa maji yalikuwa yanapita wapi? Wakizidiwa na maji tutawahamishia msomera
 
Kuna mshenzi mmoja alisema kujenga bwawa ni upuuzi kwani maji yakujaza bwawa hakuna kutokana na mabadiliko ya tabianchi, mie naona tujenge bwawa la pili liwe kubwa kuliko hilo
 
Ilitakiwa kujengwa bwawa la pili kuvuna maji ya ziada yasiishie yote bahari ya Hindi.

Maji hayo ya bwawa la pili yangetumika kwa kilimo cha kumwagilia na maji kwa huduma za kijamii
 
Tayari walishapewa elimu nzima kuhusu kinachoendelea!

Je, wametafutiwa makazi mbadala? Wameandaliwa maeneo ya kufanyia shughuli zao za kiuchumi kufidia maeneo watakayoyapoteza.

Kama hayo yote yalikwishafanyika, kwa nini bado wapo kwenye maeneo hayo hatarishi kwa maisha yao na shighuli zao za kiuchumi?
 
Tusibiri Lema na Mdude kwanza wanasemaje kuhusu hili jambo
 
Kwanini yaongezeke?
Duh! Mnyalu unajiaibisha kweli. Ina maana huelewi kabisa mabwawa ya kuzalishia umeme yanavyofanya kazi?

Haya, ngoja nikupeleke taratibu na shule hii ya darasa la nne:

Ili kuwa na maji mengi ya kutosha kuzalishia umeme kwa muda mrefu, mabwawa makubwa huwa yanajengwa, mara nyingi kwa kuzuia mito inayotiririsha maji. Hiyo huwa inafanyika kwa kuzuia mkondo wa maji wa asili.

Wakati wa uzalishaji umeme, milango ya bwawa huwa inafunguliwa. Ukifunguliwa mlango mmoja, maji yatakayotoka yatakuwa kiasi fulani. Na huko yanakoelekea wahusika wataona. Ukifungua mlango wa pili, na wa tatu, maji yanayotoka yatazidi kuongezeka huko yanakoenda, na kama tahadhari hazikuwekwa sawasawa, yanaweza kutokea mafuriko yanayozidi hata ya mvua, na kusababisha maafa makubwa. Hata ikitokea kwa bahati mbaya kingo za bwawa zikavunjika, ni balaa kubwa, kama yanakoelekea maji kuna makazi ya watu au wanyama wa porini au viumbe vingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…