Bwawa la Mwalimu Nyerere na athari kwa vijiji vilivyopo bondeni mwa bwawa hilo

hizo ni athari za kawaida kwenye miradi mikubwa kama huu 🐒

na bahati nzuri dosari, kasoro, hatari na athari zinazoendelea kujionyesha zinadhibitika, zinarekebishika, zinaepukika na zaidi sana zinazuilika; na kwahivyo hakuna haja ya kuwa na wasiwasi 🐒

pongezi sana kwa Rais, Comrade Dr SSH, kiongozi wetu, ambae sote tunampenda sana, kwa kusimamia kikamilifu ukamilishwaji wa mradi huu muhimu sana, kwa maslahi mapana ya Taifa na Watanzania wote 🐒
 

Maji yaliyofunguliwa kutokana na bwawa kujaa na yale yaliyofunguliwa kwenye mlango wa turbine moja, mwishowe ni lazima yanaingia kwenye mkondo mmoja wa maji.

Swali ambalo ni muhimu la kujiuliza, je, milango yote 9 ikifunguliwa kwaajili ya kuzungusha turbines zote, unaamini milango yote 9 kwa pamoja itatoa maji pungufu kuliko overflow iliyoruhusiwa kutoka? Kama milango yote ikifunguliwa, itatoa maji mengi zaidi kuliko overflow iliyoruhusiwa, tarajia madhara makubwa zaidi ya haya ya sasa. Hali hii ya sasa ni wake up call kwa wahusika. Na siyo jambo la ajabu. Mara nyingi miradi mipya, pamoja na jitihada zote za tahadhari, ikifika kwenye uhalisia, aghalabu hutakosa kukumbana na mambo ambayo hayakutarajiwa, yanayotakiwa kufanyiwa kazi.
 
Je, wametafutiwa makazi mbadala? Wameandaliwa maeneo ya kufanyia shughuli zao za kiuchumi kufidia maeneo watakayoyapoteza.

Kama hayo yote yalikwishafanyika, kwa nini bado wapo kwenye maeneo hayp hatarishi kwa maisha yao na shighuli zao za kouchumi?
Wacha nikuunganishe na waziri mwenye dhamana!
 
Kwahiyo Arab Contractor wameelekeza milango ya mitambo kwenye makazi ya Watu?
 
Taarifa ya habari ya Ijumaa usiku kutoka Tanesco ni kuwa umwagaji wa maji utaendelea hadi mwezi Mei tarehe 15 hivyo wananchi wametahadharishwa kuwa wahame kabisa kutoka bondeni.
 
Umeeleza vzr ila watu hawakuelewi. Cha kushangaza ni kwamba tahadhari imetolewa wakati maji yameshafunguliwa ili hali ilitakiwa kutolewa kabla. Jambo lingine tuliambiwa bwawa litasaidia kupunguza mafuriko mbona sasa lenyewe ndio linaleta mafuriko?
 
Taarifa imetolewa kwamba maji yamefunguliwa kwa Sababu mitambo mingine bado haijawashwa

Very simple 😂
System ya Hydro Electric Power ni nguvu ya maji ndio inatumika kuzungusha hizo motors kwahio kunakuwa na catchment area kubwa ili maji yote katika safari zake za kushuka / kutembea yapite kwenye hizo mashine ili kuzalisha umeme kwahio yakishapita / zalisha huo umeme yanaendelea na safari zake...

Na kama ili kuzalisha umeme zinahitajika pipa kumi basi hizo pipa kumi lazima ziwe zinapita katika sehemu husika continously....

The only way nyingine ya kufanya badala ya hii kuwa generator pekee inaweza pia ikawa battery - wakati matumizi madogo ule umeme wa ziada unatumika kuyarudisha juu baadhi ya maji (labda pipa moja) ili umeme ukihitajika mwingi hilo pipa moja na nyingine zile tano ziweze kuendelea kupita na kuzalisha umeme


NB: (unless kama haya maji yanayoleta tafrani ni yale ambayo yameoverflow hence kwenda mkondo mwingine tofauti na ule ambao yatakuwa yanapita kuendelea na safari zake) and if that is the case itakuwa ni uzembe katika ujenzi
 
Umeeleza vzr ila watu hawakuelewi. Cha kushangaza ni kwamba tahadhari imetolewa wakati maji yameshafunguliwa ili hali ilitakiwa kutolewa kabla. Jambo lingine tuliambiwa bwawa litasaidia kupunguza mafuriko mbona sasa lenyewe ndio linaleta mafuriko?

Lisingefunguliwa mafuriko yangetokea?
 
K
Kila mtambo unahitaji kiasi fulani cha maji ili ufanye kazi. Kwa sasa wamefungulia maji kwa mtambo mmoja na tayari mashamba ya wanavijiji yamefurika na watu kuhama makazi yao. Kwa hiyo maji yataendelea kuongezeka kadri mitambo inavyowashwa.
Kwa nivyoelewa mimi, Kwanza bwawa ni shimo la kukusanyia maji maji toka kwenye mto/mito,
Kwahiyo likichimbwa haliruhusu maji kuendea na safari yake.

Hivyo bwawa la mwalimu nyerere, kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha, limajaa mpaka kiasi kinachohitajika na bado maji, yanazidi kuingia, hivyo inalazimika kuyapunguza kwa kuafungulia.

Na wala hayafunguliwi kwa sababu mtambo unafanya kazi.
 
Elimu ilitolewa kabla ya kuanza kazi ya ujenzi. Watu ni wabishi tu kama vile wa bonde la msimbazi . Acha wakione watakimbia
 
Vijiji vinaendelea kuogelea kwenye maji
 
Mkuu wa wilaya ya Rufiji Bw. Edward Gowele amewataka watu wote walio bondeni mwa Bwawa la Mwalimu Nyerere kuhama haraka kwa kuwa sasa Tanesco wamelazimika kufungulia milango 4 baada ya bwawa kuzidiwa na maji. Maji yanayotiririka baada ya kufunguliwa ni kama mita za ujazo 7500 kwa sekunde.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…