Bwawa la Nyerere na MV. Mwanza ni kielelezo tosha kuwa Hayati Magufuli alitumia vyema pesa za umma. Sio hii habari ya tril 1 kujenga madarasa hewa

Amejenga kwa akili kubwa sana ya kuenvite wawekezaji ili kukusanya Kodi pamoja na uwezo binafsi wa kwenda njie na kutafuta loans zenye masharti nafuu. Jpm asingeweza mana machinga wasingeweza kulipa Kodi na kujenga hivi vitu
Malizia kula chakula cha mchana nakuja kulipa.
 
Ni nchi pekee ambayo marehemu huwa hawafi
Hata Mengi huoni bado anahesaabika kuwa ni mmoja wa matajiri Tz?

Waacheni wafu waliko na maisha yaendelee
 
Ninachojua ni kwamba awamu hii inajitahidi sana kuhakikisha miradi yote aliyoianzisha Mwendazake inakamilika, kwa gharama yoyote ile maana wakiipuuza inakula kwao. Wataikamilisha halafu watajisifu ndio utaratibu wa serikali ya CCM.
 
Unajenga madarasa kwa hela ya mkopo si kituko hicho jamani
 
Acha kulinganisha viongozi... Hayati Magufuli na Mama hawafanani na Hawawezi kufanana.. kila mtu ana alama alio acha hapa..
 
Amejenga kwa akili kubwa sana ya kuenvite wawekezaji ili kukusanya Kodi pamoja na uwezo binafsi wa kwenda njie na kutafuta loans zenye masharti nafuu. Jpm asingeweza mana machinga wasingeweza kulipa Kodi na kujenga hivi vitu
Tuseme tu ukweli nchi hii ni tajiri ila kuna watu kila mradi wanasema hatuna hela hiyo ni miradi mikubwa ila akipita hivi unasekia 100b zimeibiwa mara simbioni 350b zimelipwa
 


Pesa ya Bwawa haijalipwa bado labda kama unaongelea umuhimu wa mradi lakini pesa wanalipa mpaka saaa.

Mkopo wa kujenga madarasa ulikuwa mzuri inawezekana haujawlewa riba za mikopo hii mikubwa nenda kasome zaidi kabla ya kulalama
 
Ninachojua ni kwamba awamu hii inajitahidi sana kuhakikisha miradi yote aliyoianzisha Mwendazake inakamilika, kwa gharama yoyote ile maana wakiipuuza inakula kwao. Wataikamilisha halafu watajisifu ndio utaratibu wa serikali ya CCM.
We mjinga Sana hivi kwamfano mama asingeikamilisha ungemfanya nini?
 
Wazee wa kujipimia, kula mpaka kuvimbiwa na phd zao.

Misunderstanding imenipa matusi.

Hivi hamjaona kampeni inayokataza kumtaja Magufuli kwa mema?

Jana meli ya MV Mwanza imeshushwa ziwani. Ulisikia Magufuli ametajwa mchango wake?

Ndiposa upeo mdogo wetu Watanzania unajikita kwenye matusi kutukana tusiowajua. Aibu!
 
Kwani jpm kafanya Nini kwenye hiyo meli zaidi ya kutamka ambapo hata Mimi ni ningeweza kutamka bila vitendo
 
Mkuu,

Kwanza inaelekea hujajua mpango wote wa fedha za Covid-19 kwa ujumla wake. Mpango mkuu ulikuwa kwa ajili ya kupunguza upungufu wa madarasa especially kwenye shule za sekondari (madarasa 12,000 - main schools, madarasa 3000 - shule shikizi na mabweni 50).

Mpaka December 2021, fedha zilizokuwa disbursed kwenye sekta za Afya shilingi bilioni 180.4; Elimu shilingi bilioni 353.4; Maji shilingi bilioni 32.7; Utalii shilingi bilioni 26.8; na uwezeshaji wa kaya maskini kupitia TASAF shilingi bilioni 5.5.

Mpango huu ni multi-sectoral kwa mfano ununuzi magari ya wagonjwa ya kisasa (20) na magari ya kawaida (365), Ujenzi wa vituo vya dharura na vifaa kwa hospitali zote kuanzia Taifa hadi halmashauri, Uimarishwaji wa mfumo wa usambazaji na ununuzi wa mitungi ya gesi katika hospitali za rufaa, Usimikaji wa vinu (44) vya hewa ya Oksijeni kwa ajili hospitali za Taifa na halmashauri, Ununuzi wa mashine za X-Ray (85), Ufungaji wa mashine za MRI kwa hospitali za Taifa, kanda na mikoa, pamoja na Ujenzi wa vituo vinne vya Telemedicine. Ujenzi wa vy (ICU) 72 kwa ngazi ya Taifa, kanda, mikoa na baadhi ya halmashauri.

Bwawa la Nyerere liko 82% mkuu na halijakamilika, plus bado transmission line bado hata kuanza. Kumbuka JPM aliacha ujenzi uko kwenye 35%. Ingawa hatuwezi kuweka pembeni juhudi zake na push ya mradi huu.

Tatizo la kukaa chini kwa watoto wetu lipo na lilikuwepo wakati wa JPM, si hilo tu kuna issue za vyoo na majengo chakavu, majengo ya waalimu, mabweni, tehama nk. Mahitaji ya madarasa na nyumba za waalimu zinahitaji kama Trillion 4 ili kila kitu kijitosheleze kwa quality inayokubalika, hii ni kutokana na Serikali kutoweka kipaumbele miaka mingi kwenye sekta ya elimu.

Mwisho, ni vizuri kusifia serikali kama taasisi na si mtu mmoja kwa sababu hawezi kufanya kila kitu. Tunaweza kusifia uongozi kuwa na push au kuwa results oriented lakini si kusema Samia au JPM alifanya hiki na kile, si afya na ni ushamba flani.

Adios.
 
Kama tungekuwa na watu kama wewe as decision makers nchi hii ingekua imejaa mafukara mara mia tulivyo sasa.
 
Shetani utashindwa.
 
It is dangerous to be right when the government is wrong
Voltaire
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…