Yaani waziri wa pesa anadai madarasa ya tril 1.3 yamejengwa lakini ukizunguka hapa nchini unakuta watoto wanakaa chini.
Bwawa la Nyerere linakamailika, Mv Nyerere imekamilika. Hii yote ni sababu ya hayati JPM kusimama kidete.
NB: Mimi siko genge lolote.
Mkuu,
Kwanza inaelekea hujajua mpango wote wa fedha za Covid-19 kwa ujumla wake. Mpango mkuu ulikuwa kwa ajili ya kupunguza upungufu wa madarasa especially kwenye shule za sekondari (madarasa 12,000 - main schools, madarasa 3000 - shule shikizi na mabweni 50).
Mpaka December 2021, fedha zilizokuwa disbursed kwenye sekta za Afya shilingi bilioni 180.4; Elimu shilingi bilioni 353.4; Maji shilingi bilioni 32.7; Utalii shilingi bilioni 26.8; na uwezeshaji wa kaya maskini kupitia TASAF shilingi bilioni 5.5.
Mpango huu ni multi-sectoral kwa mfano ununuzi magari ya wagonjwa ya kisasa (20) na magari ya kawaida (365), Ujenzi wa vituo vya dharura na vifaa kwa hospitali zote kuanzia Taifa hadi halmashauri, Uimarishwaji wa mfumo wa usambazaji na ununuzi wa mitungi ya gesi katika hospitali za rufaa, Usimikaji wa vinu (44) vya hewa ya Oksijeni kwa ajili hospitali za Taifa na halmashauri, Ununuzi wa mashine za X-Ray (85), Ufungaji wa mashine za MRI kwa hospitali za Taifa, kanda na mikoa, pamoja na Ujenzi wa vituo vinne vya Telemedicine. Ujenzi wa vy (ICU) 72 kwa ngazi ya Taifa, kanda, mikoa na baadhi ya halmashauri.
Bwawa la Nyerere liko 82% mkuu na halijakamilika, plus bado transmission line bado hata kuanza. Kumbuka JPM aliacha ujenzi uko kwenye 35%. Ingawa hatuwezi kuweka pembeni juhudi zake na push ya mradi huu.
Tatizo la kukaa chini kwa watoto wetu lipo na lilikuwepo wakati wa JPM, si hilo tu kuna issue za vyoo na majengo chakavu, majengo ya waalimu, mabweni, tehama nk. Mahitaji ya madarasa na nyumba za waalimu zinahitaji kama Trillion 4 ili kila kitu kijitosheleze kwa quality inayokubalika, hii ni kutokana na Serikali kutoweka kipaumbele miaka mingi kwenye sekta ya elimu.
Mwisho, ni vizuri kusifia serikali kama taasisi na si mtu mmoja kwa sababu hawezi kufanya kila kitu. Tunaweza kusifia uongozi kuwa na push au kuwa results oriented lakini si kusema Samia au JPM alifanya hiki na kile, si afya na ni ushamba flani.
Adios.