Bwawa la Nyerere ni uamuzi mgumu na wa kijasiri uliofanywa na Magufuli!

Bwawa la Nyerere ni uamuzi mgumu na wa kijasiri uliofanywa na Magufuli!

Suzy Elias

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2021
Posts
1,067
Reaction score
6,200
gersonmsigwa~p~CjvuOaSt3OF~6.jpg

gersonmsigwa~p~CjvuOaSt3OF~1.jpg


Tunaposema Hayati Magufuli alikuwa mtu na nusu hasa kwenye mambo yaliyohusu kuamliwa kijasiri bila kujali faida na hasara zake hakika alikuwa kinara kwalo.

Mfano ni uamuzi wa kujenga hilo bwawa hapo juu (Bwawa la Nyerere) ki-ukweli ili ujenzi wake uanze ilihitaji mtu jasiri na asiyeyumbishwa kama Magufuli.

Kelele, vitisho, hujuma na hata usaliti vilimea kwa kasi lakini mwamba hakujali na alisimamia kile alichokiamini!

R.I.P JPM.
 
Kama yeye alikuwa na vyeti halali kwanini alimpoteza Bensàa8
kwa hiyo ben saanane alikuwa anaijuwa elimu ya jpm[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hata kama alihoji hakuwa na ushahidi wa kutosha kujuwa kama ni msomi au siyo msomi kwani ben alikuwa ninani hadi awe na taarifa za kutosha kuhusu elimu ya JPM
 
kwa hiyo ben saanane alikuwa anaijuwa elimu ya jpm[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hata kama alihoji hakuwa na ushahidi wa kutosha kujuwa kama ni msomi au siyo msomi kwani ben alikuwa ninani hadi awe na taarifa za kutosha kuhusu elimu ya jpm

Elimu ni jambo lililo wazi, sio ugonjwa useme ni siri kati ya mgonjwa na daktari wake.
 
Ok JPM alikuwa anathubutu, lakini alikuwa hajali ipasavyo ushauri wa kitaalamu au kuwa na subira utafiti kamili utangulie ujenzi wa mradi.
WWF wana msemo " the true cost of a dam never shows up on a balance sheet". Aswan Dam huko Misri kmf uliongeza eneo la umwagiliaji maji kwa wakulima, lakini mimea iliyopandwa ilikuwa hafifu kwa kukosa virutubisho vilivyonaswa bwawani. Matumizi ya mbolea yakaongeza sana gharama. Huko kwenye delta ya mto Nile uzalishaji wa kamba (prawns) ulitoweka- $7 bilioni kwa mwaka zikapotea.
Nini tunajifunza toka mgao wa umeme uliopo sasa hivi wakati tuna mabwawa ya Kidatu, Kihansi, Pangani,Mtera nk?
 
Kwahiyo hiyo miti kwako ni muhimu kuliko maisha ya watanzania yaliyokuwa yanateketea kwa ukosefu wa nishati hii muhimu?

Miti pia ni mali ya watanzania lazima waambiwe ilipelekwa wapi baada ya kukatwa.
 
View attachment 2388796
View attachment 2388797

Tunaposema Hayati Magufuli alikuwa mtu na nusu hasa kwenye mambo yaliyohusu kuamliwa kijasiri bila kujali faida na hasara zake hakika John yake ilikuwa namba moja.

Mfano ni uamuzi wa kujenga hilo bwawa hapo juu ( Bwawa la Nyerere) ki-ukweli ili ujenzi wake uanze ilihitaji mtu jasiri na asiyeyumbishwa kama Magufuli. Kelele, vitisho, hujuma na hata usaliti vilimea kwa kasi lakini mwamba hakujali na alisimamia kile alichokiamini!

R.I.P JPM.
Suala la umeme hata mimi ninaliunga mkono, lakini kutekeleza miradi 5 ya billions of shillings ndani ya muda mfupi kwa nchi masikini kama Tanzania hayakuwa maamuzi sahihi.
 
Back
Top Bottom