MISULI
JF-Expert Member
- Jan 15, 2014
- 7,843
- 5,476
Alipeleka ufipa na mingine ubeligiji.Alipeleka wapi miti iliyokatwa kwenye eneo hilo? Au ndio katika hayo hayo ya kutokujali watakaohoji?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Alipeleka ufipa na mingine ubeligiji.Alipeleka wapi miti iliyokatwa kwenye eneo hilo? Au ndio katika hayo hayo ya kutokujali watakaohoji?
Muache Rais JPM si Sawa kumuita hivyo aisee..Magufuli alikuwa ni takataka japo kwenye bwawa na sgr nilimuunga mkono.
Kama yeye alikuwa na vyeti halali kwanini alimpoteza Bensàa8
Elimu ni jambo lililo wazi, sio ugonjwa useme ni siri kati ya mgonjwa na daktari wake.
Hakuna project iliyohitaji maamuzi magumu na uthubutu wa ajabu kama project ya serikali kuhamia Dodoma. Inashangaza nchi kubwa kama hii viongozi wa aina ya Magufuli wanatokea nadra sana.
Unataka kupingana na maazimio ya serikali toka awamu ya baba wa taifa?Dar es Salaam kulikuwa na shida gani hadi watu wahamie Dodoma??
Alipeleka ufipa na mingine ubeligiji.
sasa kama jambo liko wazi huyu bwana ako alikuwa anahoji ili apate chakula au???
unakurupuka huko umeshiba makande unaanza na vyeti vya rais!!!
Mjomba Magu alikuwa na nia nzuri lakini wakati ulikuwa umeishapita wa kujenga Bwawa hilo.Ok JPM alikuwa anathubutu, lakini alikuwa hajali ipasavyo ushauri wa kitaalamu au kuwa na subira utafiti kamili utangulie ujenzi wa mradi.
WWF wana msemo " the true cost of a dam never shows up on a balance sheet". Aswan Dam huko Misri kmf uliongeza eneo la umwagiliaji maji kwa wakulima, lakini mimea iliyopandwa ilikuwa hafifu kwa kukosa virutubisho vilivyonaswa bwawani. Matumizi ya mbolea yakaongeza sana gharama. Huko kwenye delta ya mto Nile uzalishaji wa kamba (prawns) ulitoweka- $7 bilioni kwa mwaka zikapotea.
Nini tunajifunza toka mgao wa umeme uliopo sasa hivi wakati tuna mabwawa ya Kidatu, Kihansi, Pangani,Mtera nk?
Hakuna project iliyohitaji maamuzi magumu na uthubutu wa ajabu kama project ya serikali kuhamia Dodoma. Inashangaza nchi kubwa kama hii viongozi wa aina ya Magufuli wanatokea nadra sana.
Unaweza ukafanya uamzi mgumu na ukawa wa kipuuzi vilevile..
Kwanza angekuwepo Mwendazake hilo Bwawa lingemalisika 2040 maana hakuwa na pesa..
Baada ya mwaka na nusu ujenzi uko zaidi ya 70% kutoka 30% ya miaka 2 ya kujengwa na Mwendazake,zaidi ya mara 2.
Sina uwezo wa kujua uhakika wa hiyo "R.I.P". Mwenye mamlaka makubwa juu ya hilo anajuwa mwenyewe.
Ila nikubaliane na wewe, kuna maamuzi ambayo aliyafanya Magufuli, katika hali ya kawaida angestahili heshima zote zinazowezekana ndani ya nchi hii.
Binafsi nitaongezea na uamzi wa kwenda Dodoma, na mengine kadhaa wa kadhaa.
Lakini nisichojuwa kingine ni jinsi akili yake ilivyokuwa ikifanya kazi; kiasi kwamba hayo mazuri yakichanganywa na yale ya hovyo kabisa, mazuri yote yanaonekana yana uchafu mkubwa sana.
Mkuu heb acha kukaririshwa.Mjomba Magu alikuwa na nia nzuri lakini wakati ulikuwa umeishapita wa kujenga Bwawa hilo.
Mwalimu Nyerere aliambiwa na maswaiba wake wa Nordic Countries kujenga hilo bwawa miaka ya 70,lakini Vita vya Kagera vikavuruga mapesa ya kulijenga.
Mjomba Magu kaja kujenga bwawa hilo tena kubwa kuliko makisio ya utawala wa Mwl Nyerere, miaka 40 baadae mazingira yamekuwa tofauti,tabia nchi,maji ya mto Rufiji sio kama enzi hizo kwa sababu vyanzo vya maji vimeharibiwa na shughuli za binadamu.
Pili,Sasa tuna gesi asilia nyingi tu,alitakiwa atumie gesi asilia kama nishati namba mmoja,in a long run matumizi ya kuni yangepungua,na uoto wa asili kwenye mabonde yetu ugerudi.
Lakini walikata miti milioni 6 kupisha ujenzi wa bwawa hilo unategemea hiyo miti ilichukuwa miaka mingapi?
Kuna uwezekano wa huo mradi ukawa white elephant sababu ya kitu muhimu kimoja kikuu UPATIKANAJI WA MAJI YA KUTOSHA KUENDESHA TURBINE ZOTE KWA WAKATI WOTE.
Majangili ya ufipa hayatakuelewa.View attachment 2388796
View attachment 2388797
Tunaposema Hayati Magufuli alikuwa mtu na nusu hasa kwenye mambo yaliyohusu kuamliwa kijasiri bila kujali faida na hasara zake hakika John yake ilikuwa namba moja.
Mfano ni uamuzi wa kujenga hilo bwawa hapo juu ( Bwawa la Nyerere) ki-ukweli ili ujenzi wake uanze ilihitaji mtu jasiri na asiyeyumbishwa kama Magufuli. Kelele, vitisho, hujuma na hata usaliti vilimea kwa kasi lakini mwamba hakujali na alisimamia kile alichokiamini!
R.I.P JPM.
Dah!Una ushahidi wa hayo mabaya?