Bweni la Shule ya Sekondari ya Bwiru lateketea kwa moto, Wanafunzi zaidi ya 70 wanusurika kifo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
FWedJLbXkAAaox-.jpg

FWedJaGXEAARdNc.jpg

FWedJm-WQAA23jZ.jpg
Zaidi ya wanafunzi 70 wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Bwiru iliyopo Pasiansi Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza, wamenusurika kifo baada ya bweni walilokuwa wanalala kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo Juni 30, 2022 na kuunguza vitanda, magodoro, nguo pamoja na vifaa vyao vya shule

Moto huo unaodaiwa kuzuka majira ya saa 3:36 usiku ambapo kwa kawaida muda huo wanafunzi wote walikuwa madarasani wanajisomea ghafla wakasikia kengele ya dharura ndipo wakatoka nje na kuona bweni hilo ambalo walikuwa wanalala wanafunzi wa kidato cha kwanza likiteketea kwa moto.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mwanza, Ambwene Mwakibete amesema waliudhibiti moto na hakuna kifo, wanafanya uchunguzi kujua chanzo.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel, amefika katika shule hiyo na kusema uongozi wa mkoa utahakikisha unasimamia taratibu zote na kuhakikisha wanafunzi hao wanapata sehemu ya kulala ikiwemo na vifaa vyao vilivyoteketea kwa moto ili kuhakikisha wanaendelea na masomo yao.

FWedI-sWIAABbfE.jpg
 
Matukio ya moto yamezidi sasa lazima hili swala liangaliwe kwa jicho la tatu. .
 
Haiachi hii tabia ya moto
 
Kama n bwiru boys bhas sababu n connection hyo Simu nyng saiv shule na sehemu ya kuchaj hamna n kuconnect kmagendo tu

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
watoto wa siku hizi watukutu sana, wanachoma halafu wanajikausha.
mara nyingi wahusika ni wao, uchunguzi uanzia hapo.
 
Baridi limezidi huku!! Labda wanachemsha maji ya kuoga...
 
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mwanza, Ambwene Mwakibete amesema waliudhibiti moto na hakuna kifo, wanafanya uchunguzi kujua chanzo.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel, amefika katika shule hiyo na kusema uongozi wa mkoa utahakikisha unasimamia taratibu zote na kuhakikisha wanafunzi hao wanapata sehemu ya kulala ikiwemo na vifaa vyao vilivyoteketea kwa moto ili kuhakikisha wanaendelea na masomo yao.
Politics

Hivi kuungua kwa shule au bweni moja hakuwezi kuwa somo la kuchukua hatua za kujikinga na majanga hayo kwa shule zingine. Tume zinazoundwa huwa zinakuja na mapendekezo gani! Kwanini hayafanyiwi kazi kwa maeneo mengine!! Kufa kufaana
 
Back
Top Bottom