Cadet za ubora wa juu zinazouzwa Tanzania zinatokea nchi gani?

Cadet za ubora wa juu zinazouzwa Tanzania zinatokea nchi gani?

sio bongo mkuu naulizia nchi zinakotokea hizo Cadet ili nizinunue huko
Ni vizuri kwanza ukawajua wateja wako.
cadet OG kabisa hapa bongo bei ni 150+, maduka ya mlimani city na kwenye ma-mall. hizi hutokea sana sana uturuki

fake grade one (hata fake nazo zina grade) hizi hupatikana china. kuanzia sh 35-50 kulingana na maduka

fake grade 2 kuanzia 25-30

fake ya mwisho kuanzia 15-20

sasa hapo kama ww ni mfanyabiashara unaangalia purchasing power ya wateja wako.
maana zote hizo zina wateja wake
 
Mkuu ( Splash huwa zipo nzuri pia na hata streetsoul sio wabaya sana na hawa jamaa woolworths ) 😀😀😀😀.. inabidi Alu ukimtoa tu umepele sehemu moja wapo hapo ang'ae ng'ari ng'ari nitakuwa mpambe wako nashika maji yako mkononi
Hapo woolworths bei zao sio za kitoto,kuna mdada mmoja nilimuona amenunua kadeti kumuuliza ananionyeshea risiti kucheki amenunua Laki moja,ila ile kadeti nisikufiche haipauki ufue unavyoifua ama uiloweke unavyoiloweka lakini haipauki,vizuri gharama
 
Niliwahi kununua kadeti Mlimani City elfu 60, nilivyoifua mara moja sikutamani kuivaa tena. Yaani ilikuwa rangi ya blue ikabadilika ikawa rangi ya udongo. Kwa sasa navaa brand za Masimo Dute na Vicobbs. Nazinunua kuanzia 35k Kariakoo nikienda ushuani wananipiga kuanzia 40k. Siwezi kusema ni bora sana lakini zinapauka kidogo kidogo (sio magotini pekee) baada ya kuzitirimba kwa muda mrefu sana.
 
Ukitaka kadwti au jeans au mashati ya mtumba saaafi kabisa, nenda Ilala Sokoni kila siku wanafungua mzigo mnagombania bei hapo mnadani. Zipo zinazovutika pia zisizovutika, zisizovutika kwa sasa hazina bei kubwa kabisa sababu soko lake ni gumu kwa sasa, wengi wanapenda za mpira. Juzi tu hapa mimi nimetoka kununua jeans 9 kwa elfu 40.

Hizo kadet ukikuta wanafungua mzigo, ile unayoiona kali ya hatari bei kubwa unayoweza kuuziwa ni elfu 8. Ila ikipigwa pasi hapo Complex utauziwa hata 30 au 25
 
hapana mkuu, nataka kujua hao wanaowauzia wengine wanafungia mizigo nchi gani?? Hilo ndio swali langu sihitaji kuchukulia mzigo Dar
 
Mkuu kumbe kitu Cha mjeremani nikajua Kitu cha Monaco!!
20210614_181100.jpg
20210614_181237.jpg
Nilipewa zawadi hii kombati, imepitia jua vumbi na subuni za aina zote lakini kama mpya tu.
 
hapana mkuu, nataka kujua hao wanaowauzia wengine wanafungia mizigo nchi gani?? Hilo ndio swali langu sihitaji kuchukulia mzigo Dar
Ukitaka za namna hiyo, nenda Uturuki kafunge mzigo ao China zile second grade ambayo ukiwa sio mtu wa tamaa mzigo utausukuma vizuri tu utaisha.
 
Mi nilijua unangua hizo yoka ,america ,Italy ,German ,england ,kumbe unauliza wapi utazipata,njoo geto utazipata
 
Kwa wauzaji wengi wa Tanzania, mizigo wanatoa China.

Huko China kuna classes, kuanzia za bei ndogo ambazo tunakuja kuuziwa elfu 17-20 hadi za bei kubwa, ambazo tunakuja uziwa elfu 40+.

Tanzania tunapenda vya bei ndogo. Za kuvutika bei ndogo. Zinapendwa.

Ila cardet kali zile nzito nzito mzee baba.
Nimekuwa nikinunua kadeti mtumbani za alfu kumi kumi kisha naenda kupunguza kwa fundi wangu mmoja mkali.

Snaweza sema sina pesa ya kununua kadet moja 40K ila nahisi nimezowea tu kufanya hivyo.
 
Ni vizuri kwanza ukawajua wateja wako.
cadet OG kabisa hapa bongo bei ni 150+, maduka ya mlimani city na kwenye ma-mall. hizi hutokea sana sana uturuki

fake grade one (hata fake nazo zina grade) hizi hupatikana china. kuanzia sh 35-50 kulingana na maduka

fake grade 2 kuanzia 25-30

fake ya mwisho kuanzia 15-20

sasa hapo kama ww ni mfanyabiashara unaangalia purchasing power ya wateja wako.
maana zote hizo zina wateja wake
Hivi kadet og ina sifa gani za ziada mkuu ?

Mimi huwa kuna mshkaji wangu huwa ananishtua akifungua mzigo wa mtumba nachagua kadet nzito kali(kwa ninavyoona) naenda kuounguza kama ni kubwa.
 
Ukitaka kadwti au jeans au mashati ya mtumba saaafi kabisa, nenda Ilala Sokoni kila siku wanafungua mzigo mnagombania bei hapo mnadani. Zipo zinazovutika pia zisizovutika, zisizovutika kwa sasa hazina bei kubwa kabisa sababu soko lake ni gumu kwa sasa, wengi wanapenda za mpira. Juzi tu hapa mimi nimetoka kununua jeans 9 kwa elfu 40.

Hizo kadet ukikuta wanafungua mzigo, ile unayoiona kali ya hatari bei kubwa unayoweza kuuziwa ni elfu 8. Ila ikipigwa pasi hapo Complex utauziwa hata 30 au 25
Huu ndo mchezo wangu mkuu.

Huwa naenda mtumbani tu kucheki kadeti.

Sina kadet hata moja ya duka.
 
Nimekuwa nikinunua kadeti mtumbani za alfu kumi kumi kisha naenda kupunguza kwa fundi wangu mmoja mkali.

Snaweza sema sina pesa ya kununua kadet moja 40K ila nahisi nimezowea tu kufanya hivyo.
Mtumba ukimpata fundi mzuri zinanyooka fresh knm.
 
Ngoja aje Holy Man atupe machimbo.

Wengi siku hizi wameamua kununua mitumba tu maana hizi nyingine unadanganywa haipauki ila inapauka.

Mr Kadeti anakupa tips 10 za kufanya kadeti isipauke. Ova masherti ya mganga.

Au kama vipi amia staff-jeans.
Bro, hvi zile staff jeans nazipata maduka gani?? Asee hz kadet za cku hz miyeyusho..unavaa week mbili zmepauka,,,haya sie wengne suruali za vitambaa hatupendi,,haya hz jeans za kawaida huwez vaa ofisin. Pls naomba nijulishe chimbo la kupata staff jeans
 
Mkuu. Nina cadeti ndani kama 15 hivi. Yaani zote hazifai ata kuziangalia.

Staff Jeans ninazo 2 tu nilizibahatisha Kariakoo ata duka silikumbuki. Atleast hizo naona zinanisaidia saidia.

Hafu sijui nini kimetokea, kuna kadeti nilinunua zamani naona hadi leo zipo fresh ni nzito hafu bei ya kawaida tu.

Ila kama umewahi jaribu, cadeti za khaki ngumu sana kupauka kwasababu ya rangi yake, ila izi za rangi rangi rahisi sana kuonekana zimepauka.
 
Back
Top Bottom