CAF Champion Leagues 2024/2025

CAF Champion Leagues 2024/2025

Inawezekana wewe ndiye unatakiwa ujifunze zaidi. Miaka yote hakuna timu inayoanzia hatua ya pili. Kuna kuna kuanza preliminary kwa zile timu dhaifu na baadaye ndio wanaofuzu preliminary wanaanza raundi ya kwanza kuungana na wale walioanza moja kwa moja raundi ya kwanza. Sasa mwaka jana Yanga akiwa bingwa alianza preliminary na timu nyingine dhaifu lakini Sima japo hakuwa bingwa alianza moja kwa moja raundi ya kwanza. Hiyo ni sawa? Kwa nini Yanga aonekane dhaifu wakati ni bingwa na aliyechukua nafasi ya pili yyani Simba aonekane mkubwa zaidi? Au wewe ndugu yangu hukujua hayo?
Nilitegemea ungeingia chimbo kujifunza baada ya kukwambia ipo siku utaona hakuna timu yeyote itakayoanzia raundi ya pili kwenye msimu husika wa klabu bingwa. Hatua ya awali huwa zinatakiwa timu ziwe 64 ili ikichezwa mechi timu 32 zitoke na 32 zingine ziende hatua inayofuata. Ukiona timu kadhaa zinarushwa hadi hatua ya pili huwa inatokana na idadi ya timu kutofika 64 hivyo ile gap ndio idadi ya timu zinazorushwa hatua.

Mfano msimu uliopita kulikuwa na jumla ya timu 54 hivyo kutoka kwenye timu 64 kuna gap ya timu 10 hapo. Hivyo timu 10 zinalazimika kuanzia raundi ya pili na kubakia timu 44 pekee ambazo zinaanzia hatua ya awali ambazo zikicheza zitabakia timu 22 kisha jumlisha na zile 10 unapata jumla ya timu 32 zinazotakiwa kucheza hatua ya pili.

Msimu huu kuna jumla ya timu 59 hivyo kwenye 64 kuna gap ya timu tano, hivyo hizo timu 5 zinalazimika kuanzia raundi ya pili huku timu 54 zitacheza wenyewe kwa wenyewe na kubakia timu 27 ambazo zitaungana na zile 5 kutimiza timu 32.

Nakumbusha tu kuwa mashindano ya klabu msimu wa 2019/2020 ili shuhudia Al Ahly pamoja na ukubwa wake, kaanzia hatua ya awali kutokana na idadi ya timu zilizoshiriki klabu bingwa kuwa 61. Al Ahly alicheza mechi ya hatua ya awali dhidi ya Atrabara na kumtoa kwa aggregate ya magoli 13.

Mwisho kabisa nakurudisha kwenye hoja kwanini nimesema usishangae siku ukiona timu zote zinaanzia hatua ya awali kwenye klabu bingwa?
Ni kwa sababu CAF ina wanachama zaidi ya 50 hivyo endapo tu ikitokea wanachama 52 wameshiriki michuano ya klabu bingwa, hakutakuwa na nafasi ya timu kuanzia hatua ya pili kwasababu wanachama 40 kati ya 52 watatoa timu 40 na wanachama 12 watatoa timu 24 kwavile wanaruhusiwa kuingiza timu mbili mbili klabu bingwa hivyo jumla kutakuwa na timu 40+24 = 64

Timu zinazoshiriki michuano ya CAF hazifiki 64 ni kwasababu kuna wanachama wengine wa CAF hawatoi timu kushiriki michuano kwasababu ya sababu mbalimbali kama za kiuchumi na kimiundombinu na ndio maana kila msimu idadi ya timu zinabadilika badilika.

Kingine neno pili lisikuchanganye lilipotumika, maanake ni hatua inayofuata baada ya hatua ya nyuma yake. Usikariri bali uelewe.
 
Hii mifumo kama vile haiko sawa eti.

Sasa timu kama Gor Mahia FC ya Kenya ambayo haijashiriki hii michuano

Haendi popote yani.

Akishinda mechi yake ya kwanza, mechi ianyofuatia anakutana na Al Ahly.

Sasa hii ni nini?
Kuna timu hazitakiwi😁
 
Zamaleki anapoint zinazomwingiza moja kwa moja hata kama asipomaliza watatu au wanne
Kwani kigezo cha kushiriki hii michuano kwa timu za huko Egypt ni point timu ilizonazo huko CAF au nafasi timu iliyonayo kwenye ligi yao au FA yao?
 
Al Ahly wana qualify kwenye klabu bingwa kama bingwa mtetezi haijalishi atamaliza wa ngapi kwenye ligi yao. Na Zamalek ana qualify kama bingwa mtetezi wa kombe la shirikisho.
 
Nilitegemea ungeingia chimbo kujifunza baada ya kukwambia ipo siku utaona hakuna timu yeyote itakayoanzia raundi ya pili kwenye msimu husika wa klabu bingwa. Hatua ya awali huwa zinatakiwa timu ziwe 64 ili ikichezwa mechi timu 32 zitoke na 32 zingine ziende hatua inayofuata. Ukiona timu kadhaa zinarushwa hadi hatua ya pili huwa inatokana na idadi ya timu kutofika 64 hivyo ile gap ndio idadi ya timu zinazorushwa hatua.

Mfano msimu uliopita kulikuwa na jumla ya timu 54 hivyo kutoka kwenye timu 64 kuna gap ya timu 10 hapo. Hivyo timu 10 zinalazimika kuanzia raundi ya pili na kubakia timu 44 pekee ambazo zinaanzia hatua ya awali ambazo zikicheza zitabakia timu 22 kisha jumlisha na zile 10 unapata jumla ya timu 32 zinazotakiwa kucheza hatua ya pili.

Msimu huu kuna jumla ya timu 59 hivyo kwenye 64 kuna gap ya timu tano, hivyo hizo timu 5 zinalazimika kuanzia raundi ya pili huku timu 54 zitacheza wenyewe kwa wenyewe na kubakia timu 27 ambazo zitaungana na zile 5 kutimiza timu 32.

Nakumbusha tu kuwa mashindano ya klabu msimu wa 2019/2020 ili shuhudia Al Ahly pamoja na ukubwa wake, kaanzia hatua ya awali kutokana na idadi ya timu zilizoshiriki klabu bingwa kuwa 61. Al Ahly alicheza mechi ya hatua ya awali dhidi ya Atrabara na kumtoa kwa aggregate ya magoli 13.

Mwisho kabisa nakurudisha kwenye hoja kwanini nimesema usishangae siku ukiona timu zote zinaanzia klabu bingwa?
Ni kwa sababu CAF ina wanachama zaidi ya 50 hivyo endapo tu ikitokea wanachama 52 wameshiriki michuano ya klabu bingwa, hakutakuwa na nafasi ya timu kuanzia hatua ya pili kwasababu wanachama 40 kati ya 52 watatoa timu 40 na wanachama 12 watatoa timu 24 kwavile wanaruhusiwa kuingiza timu mbili mbili klabu bingwa hivyo jumla kutakuwa na timu 40+24 = 64

Timu zinazoshiriki michuano ya CAF hazifiki 64 ni kwasababu kuna wanachama wengine wa CAF hawatoi timu kushiriki michuano kwasababu ya sababu mbalimbali kama za kiuchumi na kimiundombinu na ndio maana kila msimu idadi ya timu zinabadilika badilika.

Kingine neno pili lisikuchanganye lilipotumika, maanake ni hatua inayofuata baada ya hatua ya nyuma yake. Usikariri bali uelewe.
Nice Analysis 👍
 
Al Ahly wana qualify kwenye klabu bingwa kama bingwa mtetezi haijalishi atamaliza wa ngapi kwenye ligi yao. Na Zamalek ana qualify kama bingwa mtetezi wa kombe la shirikisho.
This time tunaweza kukutana tena na hawa Zamaleki kwenye final ya Confedaration tuwawashe vizuri tena.
Kikosi cha Mnyama kimenyooka sana
 
Mpaka waje wajipate inakuwa kazi kweli kweli.

Nimewahurumia sana Gor Mahia na Azam kwa sababu hakuna muujiza utakaowapeleka Group Stage.
Means hata msimu ujao waki qualify wataendelea kuteseka.
Mateso yanakuwa pale pale 🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom