CAF Champions League: Al Ahly vs Yanga 20/04/16

CAF Champions League: Al Ahly vs Yanga 20/04/16

Natamani Yanga washinde ili wawahi kurudi nyumbani kuja kufanya ule uchaguzi wao waliouweka kiporo miaka nenda.
 
Timu ya Al Ahly ya Misri inawaalika Yanga ya Tanzania katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo kwenye mchezo wa kwanza uliofanyika Dar Es Salaam walitoka sare ya 1-1.
Al-Ahly-vs-Yanga.jpg

Yanga ili isonge mbele inahitaji ushindi wowote ule au sare ya 2-2 na kuendelea kinyume na hapo itayaaga mashindano hayo.
-2444-b87b4.jpg

Mechi hii itaonyeshwa live na kituo cha Azam Tv kupitia chaneli yake ya Azam two kuanzia saa 2:30 usiku kwa saa za hapa nyumbani.

Tukutane hapahapa kwenye ukumbi wetu wa JF tupeane updates kinachojiri kabla, wakati na baada ya mchezo.

cc: Makoye Matale mkolaj Katavi Amavubi


Yanga waache kupiga magoti kwenye picha, its like they're surrendering.
 
Mkuu Makoye Matale, kumbe bado upo kiongozi!!!!! Aiiisee mungu akujalie kheiri umalize mission zako urudi tena humu jukwaani, I Missed you.
Ila wale members wengi wa hili kundi hasa Mikia Fans ambao ilikuwa unawafahamu siku hizi hawapatikani tena, waliobaki humu ni Amavubi, @Katavi,GENTAMYCINE.
@graffani, OKW BOBAN SUNZU, wao wako busy kumdai Hans Poppe awape timu yao.

Hata Masuke naye kaadimika mithili ya Klabu ya Simba ilivyoadimika kwenye michuano ya CAF!
 
Wanacheza saa Napier wakuu kwa saa za hapa kwetu na TV gn itaonesha?
 
Yanga ni kama bibi harusi ambaye mida hii anapambwa saloon...akimngoja mumewe mtarajiwa aje kumchukua
 
Yanga kama mmeanza kuwa na hofu namna hii,mkifungwa si watu watazirai kabisa! Tunataka kuona Ukimataifa kwenye hii mechi.Ila kama mtacheza kama sisi,hilo jina life kabisa.leo 4bila inawahusu.
 
Alooo leo nitalala mapema sana na kesho sitaki utani wa aina yoyote ile nisije pelekwa selo bure kwa kumtoa ngeo mtu!
Mkong'oto wa leo sijui itakuaje.... nikisikia gooooooo, nafumba macho na kuvuta shuka
 
Alooo leo nitalala mapema sana na kesho sitaki utani wa aina yoyote ile nisije pelekwa selo bure kwa kumtoa ngeo mtu!
Mkong'oto wa leo sijui itakuaje.... nikisikia gooooooo, nafumba macho na kuvuta shuka
Wewe ni mnafki na wala hujui mpira, mara ya mwisho hawa waarabu waliwatowa Yanga kwa penati. Hawana lolote la ajabu na wanafungika hata kwao.
 
Yanga wanafungwa, and thats it hakuna haja ya kujipa matumaini ambayo hayapo, maandalizi mabovu ligi mbovu ushindi hata siku moja hautatokea hewani...mpira wa tanzania ni wa kwenye tv na magazeti, mpira wa kufungana simba na yanga..hakuna kitu...we still have a very long way to go.
 
Back
Top Bottom