Tate Shebughe
JF-Expert Member
- Jan 4, 2016
- 324
- 265
Timu ya Al Ahly ya Misri inawaalika Yanga ya Tanzania katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo kwenye mchezo wa kwanza uliofanyika Dar Es Salaam walitoka sare ya 1-1.
Yanga ili isonge mbele inahitaji ushindi wowote ule au sare ya 2-2 na kuendelea kinyume na hapo itayaaga mashindano hayo.
Mechi hii itaonyeshwa live na kituo cha Azam Tv kupitia chaneli yake ya Azam two kuanzia saa 2:30 usiku kwa saa za hapa nyumbani.
Tukutane hapahapa kwenye ukumbi wetu wa JF tupeane updates kinachojiri kabla, wakati na baada ya mchezo.
cc: Makoye Matale mkolaj Katavi Amavubi
Yanga waache kupiga magoti kwenye picha, its like they're surrendering.
Mkuu Makoye Matale, kumbe bado upo kiongozi!!!!! Aiiisee mungu akujalie kheiri umalize mission zako urudi tena humu jukwaani, I Missed you.
Ila wale members wengi wa hili kundi hasa Mikia Fans ambao ilikuwa unawafahamu siku hizi hawapatikani tena, waliobaki humu ni Amavubi, @Katavi,GENTAMYCINE.
@graffani, OKW BOBAN SUNZU, wao wako busy kumdai Hans Poppe awape timu yao.
Elekeza macho yako Azam TWO itakapotimu saa 1:00 usiku wa leo.Wanacheza saa Napier wakuu kwa saa za hapa kwetu na TV gn itaonesha?
Kama najua soka angalia miaka mitatu ya mwisho ubashiri matokeo ya leo. Toka 1-6 hadi 3-4. After all hizo zote ni mechi za kimataifa kwa timu ya kimataifa.
Mkuu nipo ila si unajua timu yetu inatukatisha tamaa sana.Hata Masuke naye kaadimika mithili ya Klabu ya Simba ilivyoadimika kwenye michuano ya CAF!
Wewe ni mnafki na wala hujui mpira, mara ya mwisho hawa waarabu waliwatowa Yanga kwa penati. Hawana lolote la ajabu na wanafungika hata kwao.Alooo leo nitalala mapema sana na kesho sitaki utani wa aina yoyote ile nisije pelekwa selo bure kwa kumtoa ngeo mtu!
Mkong'oto wa leo sijui itakuaje.... nikisikia gooooooo, nafumba macho na kuvuta shuka
usimchoshe Mungu,ana mengi yakufanya....Yanga wapigwe mkono moyo wangu utulieAllah ijalie Yanga leo iwafanyie kitu mbaya Al ahly