CAF: Ripoti ya Mkaguzi imeonesha Uwanja wa Mkapa hauwezi kukamilika kwa ajili ya Fainali ya Simba Vs Berkane

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708
​


CAF ilishirikiana na kusaidia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (“TFF”) pamoja na Wadau wengine kuwezesha Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kuwa mwenyeji wa Mchezo wa Marudiano wa Fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF la TotalEnergies 2024/25

Shirikisho la Soka Barani Afrika (“CAF”) lilitumia muda mrefu kushirikiana na kusaidia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (“TFF”) pamoja na Wadau wengine kuhakikisha kuwa Mchezo wa Marudiano wa Fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF la TotalEnergies 2024/25 unafanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei 2025.

Ahadi hii ni kwa mujibu wa sera mpya iliyozinduliwa miaka michache iliyopita na Rais wa CAF Dkt. Patrice Motsepe, inayotaka Sekretarieti ya CAF kushirikiana, kusaidia na kufanya kila liwezekanalo kwa mujibu wa Katiba, Kanuni, Utawala Bora na Usawa wa CAF ili kuhakikisha kuwa kila Klabu ya Soka na Timu ya Taifa katika Nchi 54 Wanachama wa CAF zinacheza katika Uwanja wa Nyumbani uliotambuliwa na kupewa kipaumbele na Viongozi wa Shirikisho la Soka la Nchi husika pamoja na Viongozi wa Klabu.

Sera hii ni sehemu ya malengo ya Rais Motsepe ya kukuza, kuendeleza na kuimarisha Soka la Klabu na Timu za Taifa katika kila moja ya Nchi 54 Wanachama wa CAF, na kuchangia katika kuhakikisha kuwa zinaweza kujitegemea na kuwa na uendelevu wa kifedha.

CAF inatoa shukrani zake kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (“TFF”), Rais wake Wallace Karia na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ya Tanzania kwa mikutano na majadiliano yaliyofanyika, pamoja na michango yao na jitihada walizofanya katika kusaidia Uwanja wa Benjamin Mkapa kufikia viwango na kanuni za CAF.

Kwa bahati mbaya, kutokana na changamoto za muda, Ripoti ya kampuni huru ya kimataifa ya tathmini ya viwanja ilihitimisha kuwa matengenezo muhimu na maboresho katika Uwanja wa Benjamin Mkapa hayawezi kukamilika kwa wakati kwa ajili ya kuandaa Mchezo wa Marudiano wa Fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF la TotalEnergies 2024/25 uliopangwa kufanyika tarehe 25 Mei 2025. Kama ilivyotangazwa katika Taarifa ya Awali kwa Vyombo vya Habari kutoka CAF, mchezo huo wa marudiano sasa utafanyika katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

CAF imejidhatiti kuendelea kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (“TFF”), Serikali ya Tanzania na Wadau wote kuhakikisha kuwa Uwanja wa Benjamin Mkapa na viwanja vyote vingine, miundombinu na vifaa muhimu kwa ajili ya maandalizi ya Mashindano ya Mataifa ya Afrika (CHAN) ya TotalEnergies Kenya, Tanzania, Uganda 2024, vinakidhi Kanuni na Viwango vya CAF. Mashindano haya yanatarajiwa kuanza tarehe 2 Agosti 2025 na CAF ina imani kuwa yatakuwa yenye mafanikio makubwa.


=============================

​
CAF assisted and cooperated with Tanzania Football Federation (“TFF”) and other Stakeholders to enable the Benjamin Mkapa Stadium in Dar Es Salaam to host the Second Leg of the TotalEnergies CAF Confederation Cup 2024/25 Final

The Confédération Africaine de Football (“CAF”) spent quite some time assisting and cooperating with the Tanzania Football Federation (“TFF”) and other Stakeholders to enable the hosting of the Second Leg of the TotalEnergies CAF Confederation Cup 2024/25 Final to take place at the Benjamin Mkapa Stadium in Dar Es Salaam on 25 May 2025.

This commitment is in accordance with the new policy that was introduced a few years ago by the CAF President Dr Patrice Motsepe requiring the CAF Secretariat to cooperate, assist and do everything possible in accordance with the CAF Statutes, Regulations, governance and fairness to ensure that every Football Club and National Team in the 54 CAF Member Association Countries, plays in a local Stadium that has been identified and is preferred by the local Member Association and Club Leadership.

This policy is part of President Motsepe’s objective to develop, promote and grow Club and National Team Football in each of the 54 CAF Member Association Countries and to contribute towards them becoming self-supporting and financially sustainable.

CAF is grateful to the Tanzania Football Federation (“TFF”), its President Wallace Karia and the Tanzania Ministry of Information, Culture, Arts and Sports for the meetings and discussions which took place, as well as their contributions and attempts in assisting the Benjamin Mkapa Stadium to comply with the CAF Regulations and standards.

Unfortunately, due to time constraints, the Report of the internationally respected, independent stadium assessment company, concluded that the necessary repairs and upgrading at the Benjamin Mkapa Stadium could not be completed in time for the hosting of the Second Leg of the TotalEnergies CAF Confederation Cup 2024/25 Final which is scheduled for 25 May 2025. As stated in an earlier Media Statement by CAF, the Second Leg will therefore take place at the Amaan Stadium in Zanzibar.

CAF is committed to continue working together with the Tanzania Football Federation (“TFF”), the Government of Tanzania and all other Stakeholders to ensure that the Benjamin Mkapa Stadium and all other stadiums, infrastructure and facilities that are essential for the hosting of the TotalEnergies African Nations Championship Kenya, Tanzania, Uganda 2024, are in compliance with the CAF Regulations and Standards. This Competition will start on 2 August 2025 and CAF is confident that it will be very successful.
 
Good!! Huko huko amani tutawapiga goal nyingi tu.
 
Wahusika wote wawajibike kuanzia Msemaji Msigwa aliyesema hata kabla ya mechi ya Al Masry kwamba "CAF waje hata leo kukagua uwanja upo tayari", Naibu Waziri Mwinjuma aliyekuwa anatoa kila siku kauli za kutuhadaa hadi Waziri Mkuu Majaliwa aliyesema "tunavyojua sisi uwanja upo tayari ila hatuwezi kuwaingilia CAF majukumu yao".

Mmekaa mnazurura na timu utadhani nyie ni sehemu ya benchi la ufundi halafu majukumu yenu ya msingi yanawashinda. Shame on you!

Embu tujenge utamaduni wa kuwajibika tuache utapeli wa kisiasa.

Na viongozi wa Simba wanaohusika kufichaficha uchafu huu wajue tunawazoom.
 
Sasa jamani haya mambo nao caf wanaleta uhuni pia.
Rais wa caf sii alikujaga kukagua uwanja kwa ajiri ya chan wakasema uwanja mukide inakuwaje tena uwanja sio mukide kwa final?
Africa bwana somjo tupu
 
Sawa tunatarajia hata derby yoyote pia, iwe ya ligi au fainali ya crdb nayo haitapigwa kwa mkapa, bali itatafutiwa uwanja mwingine
 
Kwani Simba mkichezee mechi yenu Zanzibar miguu inakuwa mizito amaa ? Embu acheni utoto banaa .
Nenda mkacheze hapo Zanzibar na mlete kombe . Unless otherwise mseme nini kitachowakwamisha msiweze kucheza na mkashindwa kule kwa mama kizimkazi.
 
Sawa tunatarajia hata derby yoyote pia, iwe ya ligi au fainali ya crdb nayo haitapigwa kwa mkapa, bali itatafutiwa uwanja mwingine

Usilinganishe international matches na hizi local . Fainali za crdb zitachezwa hapo taifa bila shida . Ila za kimataifa kwakweli hatutaziruhusu kamwe hadi uwanja ukamilike na wakaguzi wakimataifa wakague kama standard inayotakiwa kama imefikiwa.
 
KIKO WAP!
 
Nikisema CCM n matapeli eti waziri anashinda saiti ucku na mchana. Kumbe ni upigaji w PESA zangu kwenye kodi zangu.

KAZI ni kipimo cha utu
Ukiwaona n km watu kumbe wamejaa vituko TU,mambo haya yamewaumbua wizara na upigaji
 
Serikali imelala na maksudi kwa kuwa aliye juu anatokea kule kafanya hujuma za wazi, mcheza kwao utunzwa
 
Usilinganishe international matches na hizi local . Fainali za crdb zitachezwa hapo taifa bila shida . Ila za kimataifa kwakweli hatutaziruhusu kamwe hadi uwanja ukamilike na wakaguzi wakimataifa wakague kama standard inayotakiwa kama imefikiwa.
Umeelewa lakini lengo la caf kuzuia uwanja wa mkapa kutumika kwenye fainali au umekurupuka tu kujibu, uwanja wa mkapa siyo kwamba hauko tayari kuchezewa hii fainali ila wameona wauache kwanza uendelee kufanyiwa marekebisho bora zaidi kwa ajili ya michuano ya chan inayoanza mwezi wa nane, sasa international matches zina tofauti gani na local matches kama lengo ni kuutunza uwanja kwa ajili ya chan kwanini hizo local matches ziingilie kati kwenye hayo matunzo ya uwanja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…