Kuna msiba, subiri kwanza mazishi yafanyike.Upangaji wa makundi ya CAFCL umekamilika kwa Yanga kupangwa kundi moja ya Al Ahly wakati Simba itakuwa kundi moja na Esperance
View attachment 3496685
Tunaisubiri kwa hamu,wewe shabikia kunguniNitashangaa nikiona Watanzania wenzangu wakienda uwanjani kushabikia machawa
Ukiachana na al ahly hizo timu nyingine mbili hazina chochote cha kuogopesha kwenye historia ya haya mashindanoNi kundi la Yanga ni gumu, ila uwezo wa kuvuka upo kama timu ikibadilika.
Sio kuhusu historia bali ubora wa sasa wa timu. Yanga imeonekana kupoteza ubora uliokuwa kipindi cha Gamondi na Nabi. Kaja Miloud kaifanya Yanga iwe timu unayoweza kuweka hata nyumba ya urithi kwa kuwa na uhakika wa ushindi kwa kila mechi ila akaondoka na kuja kocha aliyeshusha viwango vya wachezaji na ubora wa timu kwa ujumla. Kaja kocha mpya ambaye anatakiwa kufukia mapungufu ya timu jambo ambalo linahitaji muda kufanikiwa au kutofanikiwa. Bado tuna struggle kujipata, tunacheza na timu zilizojipata na zipo kwenye ubora wao, na zikiwa zinatoka kwenye ligi kubwa Africa.Ukiachana na al ahly hizo timu nyingine mbili hazina chochote cha kuogopesha kwenye historia ya haya mashindano
Hatupo mbali sana kiubora ukilinganisha na hiyo misimu ya nyuma, almost 97% ya wachezaji bado wapo. Msimu huu tumepuyanga kwenye kusajiri kocha, hata wachezaji wapya pia sijaona hata mmoja wa kusema anaweza kuingia moja kwa moja kwenye first eleven. Bado wachezaji wengi wa zamani wapo mambo yatakaa vizuri tu. Wale asfar na kabliye tunawamudu kabisaSio kuhusu historia bali ubora wa sasa wa timu. Yanga imeonekana kupoteza ubora uliokuwa kipindi cha Gamondi na Nabi. Kaja Miloud kaifanya Yanga iwe timu unayoweza kuweka hata nyumba ya urithi kwa kuwa na uhakika wa ushindi kwa kila mechi ila akaondoka na kuja kocha aliyeshusha viwango vya wachezaji na ubora wa timu kwa ujumla. Kaja kocha mpya ambaye anatakiwa kufukia mapungufu ya timu jambo ambalo linahitaji muda kufanikiwa au kutofanikiwa. Bado tuna struggle kujipata, tunacheza na timu zilizojipata na zipo kwenye ubora wao, na zikiwa zinatoka kwenye ligi kubwa Africa.
Kwa sababu ni timu ndogo.Simba ana urahisi wa kupita ila Yanga ana wakati mgumu sana. Sijui kwa nini kila mwaka Yanga huangukia kundi gumu tu.
Game ya kwanza ni home kama sijakosea dhidi ya Far Rabat kisha tunaenda Algeria kucheza na Kabylie. Inatakiwa kuhakikisha point sita zipatikane hapo maana baada ya hapo ni mapumziko hadi 2026 January 23 kipindi ambacho tayari timu imeshafanya maboresho kupitia dirisha dogoHatupo mbali sana kiubora ukilinganisha na hiyo misimu ya nyuma, almost 97% ya wachezaji bado wapo. Msimu huu tumepuyanga kwenye kusajiri kocha, hata wachezaji wapya pia sijaona hata mmoja wa kusema anaweza kuingia moja kwa moja kwenye first eleven. Bado wachezaji wengi wa zamani wapo mambo yatakaa vizuri tu. Wale asfar na kabliye tunawamudu kabisa
Ni kweli tumalize hesabu game za mapema, maana tuna kawaida ya kuzembea game 2 za mwanzo halafu tunaenda kujipa kazi kubwa game zinazobaki.Game ya kwanza ni home kama sijakosea dhidi ya Far Rabat kisha tunaenda Algeria kucheza na Kabylie. Inatakiwa kuhakikisha point sita zipatikane hapo maana baada ya hapo ni mapumziko hadi 2026 January 23 kipindi ambacho tayari timu imeshafanya maboresho kupitia dirisha dogo