CAFCL Group Stage: Yanga yawekwa kundi moja na Al Ahly, Simba wapewa Esperance

Ni kundi la Yanga ni gumu, ila uwezo wa kuvuka upo kama timu ikibadilika.
 
Simba ana urahisi wa kupita ila Yanga ana wakati mgumu sana. Sijui kwa nini kila mwaka Yanga huangukia kundi gumu tu.
 
Nitashangaa nikiona Watanzania wenzangu wakienda uwanjani kushabikia machawa
 
Ni kundi la Yanga ni gumu, ila uwezo wa kuvuka upo kama timu ikibadilika.
Ukiachana na al ahly hizo timu nyingine mbili hazina chochote cha kuogopesha kwenye historia ya haya mashindano
 
Ukiachana na al ahly hizo timu nyingine mbili hazina chochote cha kuogopesha kwenye historia ya haya mashindano
Sio kuhusu historia bali ubora wa sasa wa timu. Yanga imeonekana kupoteza ubora uliokuwa kipindi cha Gamondi na Nabi. Kaja Miloud kaifanya Yanga iwe timu unayoweza kuweka hata nyumba ya urithi kwa kuwa na uhakika wa ushindi kwa kila mechi ila akaondoka na kuja kocha aliyeshusha viwango vya wachezaji na ubora wa timu kwa ujumla. Kaja kocha mpya ambaye anatakiwa kufukia mapungufu ya timu jambo ambalo linahitaji muda kufanikiwa au kutofanikiwa. Bado tuna struggle kujipata, tunacheza na timu zilizojipata na zipo kwenye ubora wao, na zikiwa zinatoka kwenye ligi kubwa Africa.
 
Hatupo mbali sana kiubora ukilinganisha na hiyo misimu ya nyuma, almost 97% ya wachezaji bado wapo. Msimu huu tumepuyanga kwenye kusajiri kocha, hata wachezaji wapya pia sijaona hata mmoja wa kusema anaweza kuingia moja kwa moja kwenye first eleven. Bado wachezaji wengi wa zamani wapo mambo yatakaa vizuri tu. Wale asfar na kabliye tunawamudu kabisa
 
Yanga labda watoboe sikio au pua.Safari hii hawaendi kokote
 
Game ya kwanza ni home kama sijakosea dhidi ya Far Rabat kisha tunaenda Algeria kucheza na Kabylie. Inatakiwa kuhakikisha point sita zipatikane hapo maana baada ya hapo ni mapumziko hadi 2026 January 23 kipindi ambacho tayari timu imeshafanya maboresho kupitia dirisha dogo
 
Ni kweli tumalize hesabu game za mapema, maana tuna kawaida ya kuzembea game 2 za mwanzo halafu tunaenda kujipa kazi kubwa game zinazobaki.

Msimu jana game mbili za mwanzo tuliwamudu wapinzani wetu lakini tukashindwa kupata ushindi. Matokeo yake tukalazimika kucheza kufa na kupona game za mwisho lakini ndio bahati haikua upande wetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…