CAG Assad alisema ni mtu mjinga pekee ndo anaweza kufanya manunuzi cash: Anajifunza nini Entebbe Airport?

Lakini na sisi si tulienda Hong Kong kukopa ili tukanunue ndege cash huko ulaya?
 
Kukopa kwa serikali ni hasara zaidi maana deni linakuwa kubwa siku hadi siku kwa biashara ya ndege sio kama ya dala dala usilnganishe na you tone ambazo ni pure private
ndugu yangu serikali kununua kwa cash madege ya boeing ndiyo hasara kubwa zaidi na zaidi maana pesa ambazo zingezunguka hapa ndani na wewe ukazigusa zinaenda canada zote at a go, msukuma aliyeko gulumungu ambaye hata helicopter haijui angeweza kupata mbolea kwa bei rahisi kwa sababu pesa za serikali zingeweza kusubsidise hapo.
 
Stori uliyoweka hapa wala haina uhusiano na kichwa cha habari. Uganda walikopa fedha za kuendeleza miundombinu ya uwanja wa ndege. Kinachosumbua ni wao kushindwa kuendana na payment schedule. Nothing to do with cash purchase
 
Unaongea kitaalam mno, sijui kama atakuelewa.
 
Ninachojiuliza mimi kwan kununua Cash kuna shida gani? Kama mkopo si ingekuwa hela mengi? Na mkopo unaweza kopa kiwandani kweli? Kama ndiyo kwa mda gan? Na si itakuwa mara 2 ya cash?

Sent using Jamii Forums mobile app
Acheni kukurupuka kwa vitu ambavyo hamvijui au kudhani Assad alikuwa hajui anaongea nini. Alimaanisha kuwa uchumi wetu ni mdogo sana kuweza kuchota hela zote zile kwa mkupuo mmoja.

Pili ndege kote duniani, unakopa halafu shirika linajiendesha na kulipa kidogo kidogo.

Tatu, sheria ya manunuzi ya umma inasemaje, PPRA
 
Mleta post usipende kulinganisha vitu irrelevant.

Mikopo ya mchina ni tofauti na ya mzungu.

Mchina ukikopa kujenga Reli dhamana ya mkopo ni reli yenyewe. Ukishindwa kulipa anachukua reli anaendesha anajilipa hadi deni litakapoisha.

Mikopo ya wazungu haiko hivyo, ndiyo maana tunaambiwa itafika siku Mchina ataimiliki Afrika yote.

Tatu, kauli ya Assad ilikuwa sahihi kwamba uchumi wetu Ni mdogo sana kununua vitu kwa mkupuo mmoja kwa cash. Kote duniani hakuna mtu ananunua ndege cash. Unakopa unalipa kidogo nyingine ndege zitafanya kazi zitajilipia zenyewe.

Kwani pia PPRA inasemajey kuhusu manunuziy ya umma?
 

na wewe ndo wale wale, mkopo wa mzungu huezi lipa pole pole kwa sababu wenyewe wanafidia mpaka inflation, unavolipa na ndo deni linaongezeka! 10,000 ya leo sio sawa na ya miaka mitano ijayo kwa sababu itakua imeshapungua thamani: ili kufidia hilo pengo linakuja neno riba, umekopa 100K lakini lazima ulipa 800K, yupi afadhali aliejibana akanunua kwa 100K cash ama alienunua kwa ushauri wa asaad saaahv anatakiwa kulipa 800K?
 
Stori uliyoweka hapa wala haina uhusiano na kichwa cha habari. Uganda walikopa fedha za kuendeleza miundombinu ya uwanja wa ndege. Kinachosumbua ni wao kushindwa kuendana na payment schedule. Nothing to do with cash purchase

kama story nzima hujaielewa we kaa pemben! kna watu na hizo hints chache washaelewa nazungumzia nn
 
Hivi unajua kuwa marehemu alikopa Exim Bank China ma Barclays Bank, tena mkopo wa kibiashara?

Usiwaone waganda ni wajinga zaidi yetu. Sisi mikopo tuliyouchukua Exim China na Barclays huenda ina masharti ya ovyo zaidi.
Ukikopa ndan ni sawa na hauna deni! Mikopo kichefu chefu ni ile ya mikataba miongoni mwa nchi mbili tafauti ama mashirika ya kimataifa mfano (IMF na WORLD BANK), serikali ya tanzania ikiamua kulipa madeni yote ya ndan inaweza kufanya ivo kwa mda mfupi sana, ili kustabilize tsh hua inalipwa pole pole kuhakikisha Tsh haiflactuate katika kipimo cha kushangaza
 
Hakuna tajiri ambae hakopi, wewe weka savings zako bank kuna mtu ana chukua ana zungusha ndani ya wiki ana rudisha na riba
 
Itachukua miaka mingi sn kumuelewa jamaa

kumwelewa kwa lipi na hana background ya biashara! ufipa najua mnamuelewa kwa sababu elimu yenu wote ya biashara imeishia kupangisha kwenye kile kibanda pale ufipa
 
Hakuna tajiri ambae hakopi, wewe weka savings zako bank kuna mtu ana chukua ana zungusha ndani ya wiki ana rudisha na riba

ukikopa world bank kiuhalisia unakopa katika mataifa ya G7, unakopa USD , but mfanyabiashara anakopa Tsh, whether ataweza kulipa ama atashindwa kukopa no effects will happen katika mzunguko halisi wa Tsh, sasa ushindwe kulipa china ela yao
 
kumwelewa kwa lipi na hana background ya biashara! ufipa najua mnamuelewa kwa sababu elimu yenu wote ya biashara imeishia kupangisha kwenye kile kibanda pale ufipa
Wewe naPolepole akili yenu ni sawa kamuulize Mavieitee alinunua cash.
 
ukikopa world bank kiuhalisia unakopa katika mataifa ya G7, unakopa USD , but mfanyabiashara anakopa Tsh, whether ataweza kulipa ama atashindwa kukopa no effects will happen katika mzunguko halisi wa Tsh, sasa ushindwe kulipa china ela yao
Sijui kama ume nielewa, swali ni kwamba una kopa kufanya nini? Kopa kutumia tsh, dola, au beti ila kama una uhakika na unacho fanya. Biashara zina insurance kata wekeza pata matokeo
 
Sijui kama ume nielewa, swali ni kwamba una kopa kufanya nini? Kopa kutumia tsh, dola, au beti ila kama una uhakika na unacho fanya. Biashara zina insurance kata wekeza pata matokeo

naomba kujua fani yako maaana ni kama likichwa lako halielewi, Ukikopa nje ya bongo maaana yake unakopa kwa kufidia inflation rates maaana yake ukija kulipa unamfidia mzungu factors za inflation then jumlisha na faida yake!

2) Mpaka umefika kipimo cha kukopa maaana yake umekosa fedha kutoka kwenye biashara yako, kwahio unatia mzigo wa lawama mwingine kwenye biashara ambayo mapato ya biashara yako yameshindwa kukusogeza! ukiwa na imani kimiujiza yatajilipa nadhan utakua uchawi na matajiri wangekua washalipa madeni yao yote

3) unapokopa nje unarudisha $$ sio Tsh, mfano wakati nyerere anakopa unaweza kuta dola moja ilikua sawa na 500, leo hii tupo 2400, sasa jumlisha inflation cost + faida yake + tsh kuporomoka! unapata nn? Mlundiko wa madeni ya toka miaka ya 70 ambayo hayawezi kulipika kutokana na ahadi

4) Mpaka saaahv bado tuna madeni + jumlisha mapya tunaochukua kwa masharti yale yale lazima kila mwaka wa fedha BOT ipitie EX-CHECKERS, IOU zote kujua deni la taifa limefikia wap, hata kama hamkukopa mwaka huo kuna cost za kufidia + dola imepanda thamani kiasi gan mpaka mmefikia,

5) Serikali ikikopa ndan ni kwa ajili ya matumizi ya ndan huezi kopa CRDB ukaenda kununua ndege hamna mtu ana imani na ela yako, Deni la ndan serikali inaweza kulilipa lote ndan ya sekunde kadhaa lakini kuepuka kufa kwa Tsh inabidi ilipe kidogo kidogo kuepuka kujaza pesa nyingi kwenye mzunguko! mfanyabiashara yoyote wa tanzania akikopa hakuna effect yoyote kwenye uchumi kwa sababu amesaidia tu kusambaza ela , akishindwa kulipa maaana yake asset zake znatumika ila kunakua na fresh supply mpya ya pesa!

5) Unapokopa kimataifa maaana yake unatia umaskini nchini kwako, tuseme leo serikali ikaaamua kulipa $bil 60 inazodaiwa maaana yake pesa zote kwenye mzunguko ztaisha na bado utakua unadaiwa zingine kwa sababu ya zile additional cost! wakati nyerere anakopa dola moja ilikua noti ya 500 tu, leo inakubidi mwananchi atoe noti za 500 zikiwa nne kulipa deni hilo? umetoka kwenye noti moja sasa unalipa noti 4 deni ilo ilo moja apo bado hujajumlisha faida yao, kila mwaka kuliongezeka kiasi gan

kama hujaelewa mpaka apo imekula kwako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…