CAG: ATCL imeendeshwa kwa hasara kwa miaka 5 mfululizo

CAG: ATCL imeendeshwa kwa hasara kwa miaka 5 mfululizo

Itafika sehemu tutaenda chato kutia pingu kaburi we subiri, CHADEMA walichelewesha sana maendeleo
 
Kuna uzushi mkubwa uliletwa na Zitto kuwa kasma ya Atcl imehamishiwa ikulu ili watu waibe pesa sababu pesa za ikulu hazikaguliwi. Jambo ambalo lilikuwa sio kweli na wafuasi wa Chadema walikomaa sana juu ya ishu. Leo wameumbuka.
View attachment 1736519

Hiyo sio hoja kwa sasa maana huko nyuma serikali ilikuwa inadanganya kuwa inapata faida wakati haikuwa kweli. Sasa ukweli tuliokuwa tunaufahamu unaanza kuwekwa wazi.
 
Payback Period ya mashirika ya ndege huwa ipoje mkuu
Nadhani hapo inachowekwa kwenye income statement ni ile interest rate tu.

Otherwise haiwezi rekodiwa deni lote kwa mkupuo.... Kma deni ni billion 100 then kwa amortization una igawanywa kwa miaka yote iliyobaki ya maisha ya ndege. Kma ni miaka 10 then utarekodi billion 10 kwa kila ripoti ya mwaka.

Wahasibu watusaidie hapa
 
kuna kundi fulani liliqah kutaka kumshauri. akawa blinded na political view. even though alijua hili shirika lina run on hasara.
Kuna kitu unatakiwa kujua kihasibu. Uwekezaji mkubwa mara nyingi unachukua miaka kadhaa kuanza kuleta faida. Faida maana yake hela inayoingia ni kubwa kuliko inayotoka. Hasara ni kinyume chake. Kuna ndege zimenunuliwa tu juzi unatakaje zipate faida ndani ya siku mbili? Haiwezekani kabisaa duniani kote. Baada ya muda shirika litatulia. Ukianza biashara ya kupanda mitiki leo, mwakani si rahisi ukapata faida.
 
Kuna Kenya airways, Ethiopia airways, Rwanda airways. Ili la kwetu ni uongozi mbovu na kukosa ubunifu!
Biashara ya ndege si mchezo, hata kwa nchi zenye uzoefu na mashirika makubwa , bado wanaendelea kuyaendesha kwa hasara. Tena baada ya corona kuingia basi ni taabu sana. Umeona mashirika kama Ethiopian Airlines na mengine ikabidi kuchangamkia haraka cargo ili kuweza kusurvive... mashirika mengine huku southern Afrika mpaka serikali zao zinanawa sasa mikono kuacha tu yafilisiwe i.e. kama SAA ambayo serikali imekuwa kuwa inabail out pesa mfululizo kila mwaka since 2010...Na vilevile Namibia Airways nayo imekuwa liquidated hivi karibuni for similar reasons.. Kwa hiyo biashara ya ndege si rahisi kama wengi wetu tunavyofikiri inahitaji bussines plan iliyosheni na mambo mengi, na bila kuingiza sana ' politics' ktk uendeshaji wake. Hata wenzetu Kenya Airways currently, wamekuwa wanaoperate kwa losses .. Mie ningeshauri Mh. Samia Suluhu na serikali yake, kwa issue ya ATC na kwa vile hayati Mzee wetu aliiweka chini ya ikulu moja kwa moja, na ikimaanisha kwamba kwa yeye Rais kwa sasa ndo itabidi awajibike vilevile kwa masaibu ya ATC, hivyo kwake labda akiwa na washauri wake na ikimpendeza kulingana na all options, vilevile kufikiria kuipatia ATC, deadline period ya ku break-even ambapo wakishindwa, itabidi market forces ziongeee ili kuepusha further losses. Serikali ijitahidi kutojiingiza kuimiliki 100 percent kwenye biashara na labda mostly, wanakuwa na shares tu na other entities kuepuka hasara kubwa kwa taxpayers money.
Nawatakia heri Rais Mama Samia Suluhu na serikali ya Tz mafanikio mema.
 
Mradi kama stendi ya mabasi pale Mbezi Luis umeghalimu Tsh Billion 50..!!!! Mpaka mradi ujiendeshe kwa faida tunaitaji miaka mingapi? Hapa watu wanaodili na biashara wanaweza kutushauri zaidi.
Nadhani hapa tunachanganya mambo mawili.

Hasara inakuja pale ambapo gharama za uendeshaji inazidi mapato.

Hata makampuni makubwa yana madeni yanayofika mpaka billion 200 na zaidi ila hawasemi yanaendeshwa kwa hasara kwa sababu mapato huwa yanazidi gharama za matumizi.
 
Mitano tena walisikika wabunge wa chama kileeee wakipaza sauti zao,na kukodoa macho mithili ya Chura aliyekabwa na mlo mkubwa kuzidi kiasi chake.
 
Kuna kitu unatakiwa kujua kihasibu. Uwekezaji mkubwa mara nyingi unachukua miaka kadhaa kuanza kuleta faida. Faida maana yake hela inayoingia ni kubwa kuliko inayotoka. Hasara ni kinyume chake. Kuna ndege zimenunuliwa tu juzi unatakaje zipate faida ndani ya siku mbili? Haiwezekani kabisaa duniani kote. Baada ya muda shirika litatulia. Ukianza biashara ya kupanda mitiki leo, mwakani si rahisi ukapata faida.
Mwambie Samia sasa. Hizo enzi zimepita.
 
Tukishajua Hasara Bil.60 tujue na Faida ni Bil.ngapi,usikute Faida ni Bil.90,sasa tukitoa 90 - 60 tunapata 30.bil hii ndio faida yetu japo ni kidogo ila si mbaya,hebu tuache jadili Hasara tuulize na Faida iliyopatikana kwa miaka hiyo mi 5 ni kiasi gani.
Aiseeee, Hadi huruma.! Kuna siku utaelewa kweli kama huelewi report ya CAG?
 
Daaah yaani sa hv ningekuwa na nyumba yangu nzuri kabisa maeneo ya mbweni , mweshimiwa Alibana ajira ili anunue ndege ...daaah yote mema Tu lakn
Huyu mother inatakiwa awe makini sana na suala la ajira.
Sisi hatutanii,tunataka ajira.
 
Back
Top Bottom