CAG: ATCL imeendeshwa kwa hasara kwa miaka 5 mfululizo

CAG: ATCL imeendeshwa kwa hasara kwa miaka 5 mfululizo

5457EF55-235D-4BB2-A229-57A3C603EF3D.jpeg
 
Japokuwa si muandishi mzuri, lakini mkuu umeongea facts. Hichi ndicho wenye akili walikuwa wakishauri siku zote, wamesema sana wakaitwa majina sijui wasaliti sijui wakwamishaji sijui wamekosa uzalendo.

Hii mada imewazidi uwezo watu wengi sana hasa mataga, narudia tena mataga. Hawaelewi wanatetea nini na hawaelewi hawatetei nini na wengine wameanza kuhamisha magoli eti ni mbinu za kulifilisi na kutaka kulibinafsisha shirika.

Ni lini serikali itaelewa umuhimu wa kutokuweka mtaji 100% ambao ni pesa ya walipa kodi katika biashara na badala yake imiliki shares kadhaa na ijiondoke katika uendeshaji ila ilinde maslahi yake.
Mkuu lengo la Serikali kuwa na Airlines ni ku boost sector nyingine za Uchumi kama Utalii na Kurahisisha usafiri. Kwahiyo kifupi airlines zinakuwa na indirect effect kwenye uchumi wa Nchi. Hili lazima tulikumbuke. Japo ki ukweli biashara hii ni ngumu mno. Naona Shirika la ndege la Kenya limeomba Bail out from the Government. Mimi sipingi kuwa n Airlines kama taifa, lakini nasisitza management yake iwe juu mno. US airlines ambazo ni Private business zinatengeneza faida, japo kwa kipindi hiki cha Covid Biashara zimeyumba sana. Nchi nyingine kama South Africa, zina recession kabisaa ya Uchumi, sisi kidogo kuna unafuu kutokana kwamba hatu take stringend measures za Covid kama Wenzetu kule. Anyway niseme kwa wale ambao ni below 40 years kama mimi tujuei ipo siku tutabebeshwa majukumu ya nchi, tupambane tuipiganie nchi yetu isonge mbele. Hatuna nchi tunaiita nyumbani zaidi ya Tanzania. Hapa sizungumzii Chama nazungumzia Utaifa. Maaana nchi kwanza, halafu Vyama baadaye. Mungu ibariki Tanzania
 
Meko kaku brainwash sana
Yaani hata maoni yangu ni kuwa brainwashed ? kila mtu aliyekwenda shule maana yake kawa brainwashed na hata wewe pia huhitaji kuwa na memory kung'amua yajayo... kikwete aliwaambia, akili za kuambia .. changanyanya na zako ndugu...
 
Yaani hata maoni yangu ni kuwa brainwashed ? kila mtu aliyekwenda shule maana yake kawa brainwashed na hata wewe pia huhitaji kuwa na memory kung'amua yajayo... kikwete aliwaambia, akili za kuambia .. changanyanya na zako ndugu...
Hujawa Brainwashed Mkuu. Usiogope. Tunatofautiana experience ya ku judge mambo na uzoefu katika mambo ya kisiasa na kijamii pia.
 
Tatizo la ujinga na kushupalia kitu ilhali changamoto za kusababisha hivyo zipo wazi, hivi issue ya Corona nani asiyeijua?? pamoja na kusitishwa kwa vitu vingi ikiwemo safari za nje sababu ya ugonjwa huo uliolikumba sio taifa la Tanzania bali na Dunia nzima mlitaraji ATCL itengeneze faida??? jifunzeni hata ku reason kidogo
 
Hayo na mengi mengine yalifichwa mno angetangaza hivyo enzi za magufuli angeishia pabaya, yote yatajulikana.
Tuangalie hasara inapanda au inashuka. Mimi ningefanikiwa kusoma Financial Statements zao ningeweza jua niseme nini lakini kwa sasa sina mahesabu yao.
 
Tatizo la ujinga na kushupalia kitu ilhali changamoto za kusababisha hivyo zipo wazi, hivi issue ya Corona nani asiyeijua?? pamoja na kusitishwa kwa vitu vingi ikiwemo safari za nje sababu ya ugonjwa huo uliolikumba sio taifa la Tanzania bali na Dunia nzima mlitaraji ATCL itengeneze faida??? jifunzeni hata ku reason kidogo
Una hakika hasara zimeanza baada ya corona kuibuka?
 
Kwenye swala la ufufuaji wa ATCL mheshimiwa hayati alikurupuka sana mpk watu wa kawaida kama mimi tuliona ukurupukaji wake...Ile biashara hakuiandalia mkakati madhubuti ya kiuendeshaji alichoona yeye ni kununua ndege ili macho ya watu yaone wapate kusifia
 
Wadau naomba Msaada. Ripoti ya CAG imeonyesha hasara ya 60 Bln kwa ATCL, kulikoni? Mbona ATCL wanaongoza kwa abiria wengi, ndege zinajaa Sana, Kama Ile ya India ilijaa hadi tukamchelewesha ndugu yetu aliyekuwa mgonjwa Sana kwa kukosa nafasi. SIJAELEWA, NAOMBA MSAADA.
Kujaa so hoja. Running expenses zinaendana na revenue? Inaonyesha gharama za uendeshaji ni kubwa kuliko mapato.
 
Sekta hii tungeiachia FastJet, PrecisionAir zigo hili la hasara endelevu lisingebebwa na kodi za wananchi.
Bajeti ya kununua Madege ni zaidi ya Trilioni 1. Shilingi za Tanzania
Ndege Airbus mbili aina A220- 300 ni TSZ495.6 billion Tanzanian shillings (USD215.95 million)

Oda za Boeing 787 Dreamliner US$224.6 million Tshs 448 bilioni


Pamoja na Covid-19, gharama za manunuzi ya madege na hasara endelevu kwa kweli serikali sasa inaona maamuzi yake hayakuwa sahihi. Ilitakiwa sekta binafsi ndiyo wafanye biashara hii. Na kukutokea mkwamo ktk sekta hii serikali ingeweza kutia mkono wake kulingana na uwezo wake na siyo kujiingiza ktk hasara kubwa kiasi hiki.

Imagewww.boeing.com › customers › air-...
787 Dreamliner to become part of Air Tanzania fleet - Boeing
787-8 is first ever wide-body order for 'The Wings of Kilimanjaro' Boeing and the United Republic of Tanzania have confirmed an order for one 787-8 Dreamliner, valued at $224.6 million at list prices. The aircraft will be operated by Air Tanzania, the flag carrier of Tanzania

Air Tanzania orders two more aircraft from Airbus​

Air Tanzania Airbus A220-300Air Tanzania Airbus A220-300© Airbus
22.07.2019 - 17:32 UTC
Air Tanzania (TC, Dar es Salaam) will acquire two more aircraft from Airbus, The Office of President John Magufuli has announced.
In a statement issued last week, Magufuli said only that two more aircraft had been ordered alongside a previously disclosed Dash 8-400 from De Havilland Aircraft of Canada. The state-owned airline currently operates two A220-300s in addition to one B787-8 (to be joined by a second by year-end) and three Dash 8-400s. All aircraft are leased from TGF - Tanzania Government Flight as are one Fokker 50 and one Fokker 28-3000 that were seconded to the airline on Magufuli's direction.
In the financial year 2018/19, the Tanzanian government budgeted TSZ495.6 billion Tanzanian shillings (USD215.95 million) for aircraft purchases. Magufuli intends to use a rejuvenated Air Tanzania to drive up tourist inflows thus benefiting the fiscus.
u by year-end. Source : Air Tanzania orders two more aircraft from Airbus
 
Tulisema humu hasara ya ATCL haitaishia kwenye serikali kutumia matrillioni kununua madege, bali itaenda mbali zaidi kuikamua serikali kutoa ruzuku kila mara kuliendesha shirika hilo, kwa sababu hakuna projections zozote ambazo zinatoa matarajio ya shirika hilo kutengeneza faida hata baada ya miaka ishirini, kigezo kilichotolewa kununua hizo ndege ni kushindana na rwanda kwamba nchi ndogo inamiliki ndege, nothing else!!
 
Back
Top Bottom