Swala hapo sio kupata hasara, swala ni kwamba nchi lazima iwe na shirika lake la ndege hiyo ni lazima na sio swala la kujadili. Naona kuna watu wanafurahia hapa kuona shirika limepata hasara ni kama wanataka hizo ndege zisiwepo maana zinawanyima usingizi.
Sasa tujiulize, Kenya na Ethiopia wamekuwa na mashirika ya ndege miaka nenda rudi wanapata hasara wakati mwingine faida lakini hawaachi kwa kuwa wanajua umuhimu wa ndege. Wataalamu wetu wanaohusika na biashara ya anga ndio muda wao kutoa ushauri nini kifanyike. Hata hivyo shirika letu bado changa, na safari za nje bado chache, mathematically hapo uwezekano wa kupata hasara ni mkubwa japo huko mbelini tutapata faida na hilo ndio lilikuea lengo la kununua hizo ndege.
Usifanye biashara ya hasara kwa sababu mtu fulani anafanya. KLM aliekuwa mmbia mkubwa wa Kenya Airways, alifaidika sana na hasara zao. Kabla ya kugawa sehemu ya hisa zake kwa mabank wanayoidai Kenya Airways katika harakati za kulipa madeni.
Angalia huu mchezo 👇
Kenya Airways income statement 2019
Focus on loss for the year 127 million dollar ☝️
..............................................................
👇 Angalia sasa hiyo loss inaleta faida gani kwenye income statement ya KLM mwaka huo huo
Focus on other income and expenses ☝️utaona loss ya $127 million. Maana yake loss za Kenya Airways they can claim as loss of other trading income kwao na kupunguza profit tax wanazotakiwa kulipa huko kwao kwa kiasi cha $127 million.
Ndio maana wakati serikali ya Kenya inalia hasara, KLM kama wabia wakubwa mpaka hivi majuzi they were not bothered na loss za KA kama shirika.
........................,...............................
Walivyowajanja washatoa na asilimia kubwa ya hisa zao; shirika likienda kwenye administration either serikali ya Kenya ifanye bailout au asset stripping processes zinafuata. If it’s the latter kuna enough asset bado kwao kupata faida.
Hapo kuna long story ya kuelezea on how corporate taxation works nchi za mabeberu with oversees investments on what you pay if you make profit and what you can claim back if you make a loss.
Kenya imechezewa sana na KLM kwa manufaa yao, pengine walishaona mapema KA was loss making business na sababu ya kuinvest ni kupunguza kodi kwa hasara watakazopata Kenya. That was a tax evasion scheme in a legal way.
Hiyo ni moja ya sababu usiige kitu elewa biashara inavyofanyika, na kwa management ya ATCL sahau faida hapo miaka 800, they have to go first.
Wengine TTCL hakuna kitu pale, mtu mmoja mwenye akili timamu amkanye Ndugulile mapema. Afanye yote lakini sio kuingilia mambo ya kibiashara ukimsikiliza tu unaona he is brewing another unnecessary problem leading to hike in mobile phones charges.