CAG: ATCL imetengeneza hasara ya Tsh. Bilioni 153.542 ndani ya miaka Mitano

CAG: ATCL imetengeneza hasara ya Tsh. Bilioni 153.542 ndani ya miaka Mitano

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Kampuni ya Ndege imekuwa ikitengeneza hasara kwa miaka 5 mfululizo na mwaka huu ilitengeneza hasara ya Sh. Bilioni 60.246. Kwa miaka mitano imetengeneza hasara ya Sh. Bilioni 153.542.

Screenshot 2021-04-08 at 21.30.06.png


====


Kampuni ya Ndege Tanzania

Nilifanya ukaguzi wa kiutendaji (Startegic and Operational Efficiency) kwenye Kampuni ya Ndege Tanzania na kubaini yafuatayo:

Hadi kufikia tarehe 30 Juni 2020, Serikali ilikuwa imenunua ndege 8 kwa gharama ya Sh. Trilioni 1.028 katika juhudi ya kuifufua Kampuni ya Ndege Tanzania.

Ndege hizo zinamilikiwa na Wakala wa Ndege za Serikali na ATCL huzikodisha.

Pamoja na kununua ndege, kwa miaka mitano yaani kuanzia 2015/16 hadi 2019/20 Serikali imeisaidia Kampuni ya Ndege kiasi cha Sh. Bilioni 153.711 kwa ajili ya shughuli za uendeshaji na maendeleo.

Kampuni ya Ndege imekuwa ikitengeneza hasara kwa miaka 5 mfululizo na mwaka huu ilitengeneza hasara ya Sh. Bilioni 60.246. Kwa miaka mitano imetengeneza hasara ya Sh. Bilioni 153.542.

Hata hivyo nilibaini changamoto zifuatazo ambazo zinatakiwa kushughulikiwa ili kuimarisha utendaji wa Kampuni ya Ndege:

Bodi ya Wakurugenzi haina mjumbe hata mmoja ambaye ana uzoefu kwenye masuala ya usafiri wa anga.

Wakati wa changamoto ya Corona (Covid 19) ndege nyingi zilikuwa zimesimama lakini ATCL ilikuwa inatozwa gharama za ukodishaji bila kujali kwamba ndege zilikuwa hazifanyi kazi kutokana na changamoto ya Covid 19. Hii inatokana na ukweli kwamba Mkataba wa ukodishaji kati ya TGFA na ATCL hauna kipengele cha Force majure. Katika kipindi kati ya Machi 2020 na Juni 2020 ATCL ilitozwa na TGFA kiasi cha Sh. Bilioni 15.464 kwa ajili ya ukodishaji wa ndege.

ATCL imerithi madeni makubwa ambayo hutozwa riba, kwa Mwaka wa Fedha 2019/20 ATCL imetozwa riba ya Sh. Bilioni 12.497.

Kutokana na madeni hayo, inakuwa vigumu kwa ndege za ATCL kusafiri kwenda nje ya nchi kwani zinaweza kukamatwa.

Kuna changamoto ya viwanja vya ndege hapa nchini kiasi kwamba ndege za ATCL haziwezi kuruka usiku na pia kuna viwanja ambavyo ndege haziwezi kutua zikiwa zimechukua abiria kwa uwezo wake.

Soma pia:

1) ATCL yatengeneza faida ya $14M, yafuatayo yanasisimua
 
IMG_20210408_210506.jpg


MATAGA bado hamjaamini kuwa bunge ni dhaifu? Bado ninaamini mwenda zake alikuwa rais wa wanyonge? Bado unaamini alipambana na ufisadi?

Mwenye takwimu za ufisadi enzi za JK na JPM tulinganishe.
Asante Mungu kwa kutupunguzia makali,sa hivi angeongeza miaka mitano ingekuaje?🤔🤔
 
Aisee kaburi la mwendazake lifukuliwe atandikwe viboko hata kama ni Marehemu shenzi taip!
Wenzangu Wote Mmewapa Miaka 10
Mimi Ndiyo Mninyime Kwani Nimewakosea Nini

😀😁😂😃😄😅😅😆

Huyu Daniel Hata Kujieleza Hajui Lakini Nasema Nileteeni Daniel Vinginevyo Mtajuta.


Huyu Livingstone Ni Darasa La Saba
Kwani Kueleza Matatizo Yenu Mpaka Degree
😥🤔😗🙂☺😚😙

Watu Wa Songwe Hamtapata Maji Msipomleta Silinde
 
Jamani nini hiii, yaani hiii nchi kila mtu ana piga dili?!!

huu sasa ndio muda wa kuchukua hatua stahiki kwa wahusika bila kuchelewa.

Fedha za watanzania zimechezewa na watu wachache,
watanzania wana hasira kwa kuibiwa fedha zao, njia pekee ni kuona hatua zinachukuliwa.
 
Hizo ndege ziuzwe tu hata kwa bei ya hasara, yaliyotokea yanatosha kuwa funzo kwetu, na kuanzia leo kila awamu itakayoingia madarakani iweke wazi mikataba yote itakayoingia wananchi waisome, waichambue wajue hasara na faida zake, isiwe siri tena, kuwaachia hawa CCM waendelee kufikiria kwa niaba yetu kuna siku tutauzwa kwa wawekezaji.

Hizi ripoti za CAG kila awamu zinakuja na madudu tu, tutaendelea kushangaa mpaka lini? wenye nchi tuamke sasa, hiyo mikataba watakayoingia mbele ya safari itangazwe hata kwenye magazeti ya serikali tuijue.
 
Back
Top Bottom