CAG: ATCL imetengeneza hasara ya Tsh. Bilioni 153.542 ndani ya miaka Mitano

CAG: ATCL imetengeneza hasara ya Tsh. Bilioni 153.542 ndani ya miaka Mitano

Duh bodi haina mjumbe hata mmoja mwenye uzoefu wa masuala ya ndege...CAG kichere

Nchi ina wataalam wazoefu wa masuala ya ndege wengine wame staafuu kwanini watu kama hao wasingekuwa wanawaweka kwenye bodi waache kuwaingiza wanasiasa.

Na wajanjajanja wengine.

Ova
 
Duuh basi wajameni haya maumivu niliyopitia ya mdororo wa kiuchumi binafsi, nikisikia mahasara ya mabilioni, na huku mitaani mamlaka zilikuwa zinatukaba mpaka tumeacha kufanya biashara, najihisi hasira kali!

Ngoja nipoe na SAFARI lager bariidii!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Kampuni ya Ndege imekuwa ikitengeneza hasara kwa miaka 5 mfululizo na mwaka huu ilitengeneza hasara ya Sh. Bilioni 60.246. Kwa miaka mitano imetengeneza hasara ya Sh. Bilioni 153.542
Halafu Kuna watu bado wapo ofisini na mishahara mikubwa na marupurupu manono yanaendelea kumiminika kwenye account zao! Huu ni ujinga uliopitiliza! Dpp yupo tu naye anashangaa badala ya kuchukua hatua!

Nao takukuru wapo tu mitaa wakikimbizana na rushwa za elfu kumi na kujionyesha kwenye linings kuwa wapo makini na Wala rushwa huku hazina ya taifa ikiishia kwa watu wasizidi 100!

Mama Samia, haya madudu yafike mwisho Sasa na yasisikike Tena kipindi chako! Komesha huu wizi na wahusika warejeshe pesa zetu!
 
Mataga wana kazi sana

Screenshot_20210328-145853.jpg
 
Chini ya serikali ya CCM haya mambo mbona ni ya kawaida sana. kwani ni lini ccm wakawa wakweli?
 
Hii nchi tulichezewa saaana..! Kumbe ye ndio anatuchezea anatuangalia tu halafu anasema hiiiiiiiiiiiiii!!!
Avator yako inafanana na ya ELWATEGE nikashangaa kapata wapi nguvu za kuandika.
 
Kampuni ya Ndege imekuwa ikitengeneza hasara kwa miaka 5 mfululizo na mwaka huu ilitengeneza hasara ya Sh. Bilioni 60.246. Kwa miaka mitano imetengeneza hasara ya Sh. Bilioni 153.542
Mgonja kwanza ,nafikili ifike muda wenye nchi ambao ni wanachi tuwe na maamuzi ya busara tu kwamba JPM KWA ufisadi huu uliofanyika chini yake chini ya wapambe njaa ,ni mda wa kutafuta namna ya kumfuta Kama Rais alie wahi kiongozi wa taifa Hili haiwezekani watumishi hawakuwai pandishiwa mishahara,wananchi wa kila namna wamefunga mikanda, katangulia mbele but mchakato vyema kuanza kumfuta katika record za viongozi ambao wamewahi kua marais wa inchi hii full stop so.

Tutabaki na awam ya kwanza,pili,tatu,nne ,tano inabaki KWA historia ikiwa wazi,then sita,hivi inawezekanaje kigwangala akawa anakula pesa hivi Kama waziri bila bosi wake kujua ,wenda alimpiga chini tokana na sehem flani ambayo kigwangala alikula Sana akazidi chakula Cha bosi ,mungu akawape stahiki zao KWA walio hai na ambao amewaita, KWA kutesa watanzania angali wao na familia zao zashiba
 
Kazi yao ilikuwa kusifia tu kumbe hasara kwa taifa
 
Wasipoziuza wakiendelea kuzinga'ang'ania zitaendelew kuwa jini mnyonya kodi.
Hizo ndege ziuzwe tu hata kwa bei ya hasara, yaliyotokea yanatosha kuwa funzo kwetu, na kuanzia leo kila awamu itakayoingia madarakani iweke wazi mikataba yote itakayoingia wananchi waisome, waichambue wajue hasara na faida zake, isiwe siri tena, kuwaachia hawa CCM waendelee kufikiria kwa niaba yetu kuna siku tutauzwa kwa wawekezaji.

Hzi ripoti za CAG kila awamu zinakuja na madudu tu, tutaendelea kushangaa mpaka lini, wenye nchi tuamke sasa, hiyo mikataba watakayoingia mbele ya safari itangazwe hata kwenye magazeti ya serikali.
 
Hii haindoi ukweli kuwa hasara imeenda ikipungua mwaka hata mwaka. ATCL wanayo business plan ya long term project. Watuambie BEP yao ilitakiwa ifikiwe lini?

Kwa nature ya biashara hii tulinganishe na mashirika mengine yenyewe yamefanya vipi kwa kipindi hicho?

Tuangalie faida zitokanazo na tija zake maana wajanja ni kama wameshaona mpenyo hapa wa kutengeneza mazingira ndege zilizopo zinaweza kuuzwa kama reject na zile zinazoendelea kujengwa kiwandani kama chuma chakafu.
 
Hu yu mwendazake alikua anatuchora alikua anapokea gawio la aina gan....au walikua wanagawana hasara?
 
Back
Top Bottom