CAG: ATCL imetengeneza hasara ya Tsh. Bilioni 153.542 ndani ya miaka Mitano

CAG: ATCL imetengeneza hasara ya Tsh. Bilioni 153.542 ndani ya miaka Mitano

Niliwahi kuwaonya watu Fulani wale wasiotaka kufikiri kwani huongozwa na mihemko zaidi ya kuwa serikali ya magu haikuwa serikali Bali genge la waporaji wakanizomea na kuniita majina yao Yale ya wewe sio mzalendo! Leo hii hawaamini walichoambiwa na cag Hadi mmojawao Malia kwa uchungu mkubwa!

Vyombo vya ulinzi na usalama, mahakama na wengine kwenye nafasi za maamuzi lilindeni taifa lisije kuingia kwenye machafuko ambayo chanzo chake ni hiki Cha ulaji wa fedha za umma uliopitiliza!

Wananchi kwa jinsi walivyotaabika na kuaminishwa kuwa wanajenga miradi ya kimkakati wavumilie wakipata mchomeka utambi nchi itawaka kwa jinsi walivyojaa upepo vifuani! Washitakini wahusika wote bila kuacha hata mmoja!
 
Kwa jinsi huyu mwendazake alivyoweka pause mishahara ya watumishi na kubana watu mikanda tukiamini nchi inasonga kumbe wanagawana noti yeye na genge lake,natamani nisikie hata anatandikwa viboko huko alipo tuvisikie hadi huku duniani
 
DAAH jamani si amesacrifice maisha yake kwa wanyonge
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji125][emoji125][emoji125]
 
Sasa kama mambo ndivyo yako hivi since the beginning of this project, hilo gawio la faida ya Tshs. 25bn ambazo ATCL walitoa kwa serikali mwaka 2019 zilitoka wapi..?

Hivi ndiyo tuseme Hayati John P. Magufuli akishirikiana na hawa ATCL walikuwa wanacheza mchezo hatari na wa kijinga kiasi hiki dhidi ya Watanzania..?

I am completely speechless and puzzled na Urais wa John Pombe Magufuli maana mtu akisoma haya hataelewa maana ya haya mambo ilikuwa ni nini hasa..

Ni kana kwamba nchi ilikuwa inaongozwa na mwizi tu 100%...
 
View attachment 1746920

MATAGA bado hamjaamini kuwa bunge ni dhaifu? Bado ninaamini mwenda zake alikuwa rais wa wanyonge? Bado unaamini alipambana na ufisadi?

Mwenye takwimu za ufisadi enzi za JK na JPM tulinganishe.
Asante Mungu kwa kutupunguzia makali,sa hivi angeongeza miaka mitano ingekuaje?🤔🤔
Alishatangulia mbele za haki mpumzisheni, na nyinyi pambaneni kufanya yenu. Tunajua kwamba now mtakuwa bize kututhibitishia kuwa JPM alikuwa lijizi ili kujijustfy nyie 'vijizi', ili tukija wauliza mbona mwaiba mjiteteee kwa kujilinganisha nae.

Ndugai kashatuandaa kisaikolojia tusahau kuhusu reli that watu wanahamia kwenye bandari now, tunajua project nyingi za JPM kuwa kaenda nazo kaburini ! Yetu macho
 
Hivi ndugu zangu huyu Magufuli alikuwa anatupeleka wapi?Yaani uchafu wote huu huku akituambia tutembee kifua mbele kweli?
 
Ni kwa sababu hataweza tena kufungua kinywa chake,madhaifu yote yatakayoonekana nilazima mmtupie yeye.
Nawambieni hata iwe nini yeye alifanya alichokiamini na amewaachieni ninyi kila mlichokitaka
Sasa kila mmoja ahangaikie maisha yake mapya yeye hamtamuona tenaa
 
Ni shirika la umma, kazi yake ni huduma sio biashara.

Hujui chochote!! Nia ya ulichosema huwa ni kutotoa huduma kwa faida. Sio kujiendesha kwa hasara. Hata sijui kama una uwezo wa kutambua tofauti!

Ujinga wa namna hii ndio shida ya nchi. Hizi ndege zinafanya safari za ndani, vipi kama zingekuwa zinafanya safari za kimataifa - ungesema zinatoa huduma???

Mawazo yenu ya “ujamaa na kujitegemea ndio njia PEKEE ya kujiletea maendeleo” ndio yametifikisha hapa. Ingekuwa hivo miaka yote hii ya uhuru si tungekuwa tunazizidi nchi za kibapari?? Ujinga from right, left and center!!
 
Back
Top Bottom