Hazijatumika siyo kwa sababu ya sheria ni kwa sababu aliyezitaka kaondoka angekuwepo wala asingehitaji sheria yangekuwa maelekezo tu, Nampongeza sana tena kwa dhati ya moyo wangu DPP, amefanya kazi nzuri sana (wasikilizaji wanapiga makofi, DPP ananyanyuka na kuinama) kaa tu DPP, amekusanya ndani ya miezi 4, 60B hizi ni fedha za watanzani maskini zilichukuliwa na wachache ila kwa sheria tuliyoipitisha bungeni na kwa hili nimpongeze Spika mtani wangu kwa kuhakikisha sheria inakamilika na tumeifanyizia kazi na haya leo ndiyo matunda yake
Sasa naelekeza hizo bilioni 60 zipelekwe Tanroads zikajenge mabarabara na madaraja na miundombinu mingine watu wa hazina mlisimamie hili kikamilifu(makofi), au nimefanya vibaya ndugu zangu, Asanteni sana