CAG kama umo humu naomba unijibu haya maswali

Magufuli alikopa trilioni 29 kwa miaka 5 tu...Huu ni mkopo mkubwa zaidi kuchukuliwa na Rais wa Tanzania

Na huyu CAG alichaguliwa na Magufuli baada ya kumuona Assad hafai

Swali ni je kwa nini utawala wa Magufuli unagombana na kila CAG?
The best answer ever[emoji1317][emoji1317][emoji1317][emoji1317]
 
Haya yote yanahalslisha ufisadi? Pia kumbuka kilichojengwa ni kwa kodi zetu, yeye alikuwa msimamizi, ok na tulimlipa. Pesa iliyofisadiwa ni kodi zetu, tunapaswa kumuuliza na tuna haki ya kupewa majibu na wezi wawajibishwe.
 
CAG wa zamani alitumika na genge la wale jamaa kutaka kumchafua Dkt Magufuli na serikali, nasema Prof ni mdini mno na hana weledi wa utumishi wa umma.
Vp kuhusu huyu wa sasa ambaye alimchagua mwenyewe? Jiwe kifupi hakupenda kufanya kazi na watu wenye ueledi ndiyo maana alikuwa anajificha kwa watu wanyonge.
 
Unaharibu na kushusha hadhi ya Neno hayati. Nisawa na kusema Hayati Idd Amin
 
Unaweza kuweka ushahid hapa? Hakuna utawala uliokuwa haupendi kukaguliwa kama ule wa jiwe. Kumbuka mpaka shirika la ndege alilirudisha chini yake ili kukwepa kukaguliwa. Ila wanyonge na mazuzu ni kushangilia tu
 
JPM will remain as the best president Tanzania have had. Ukiwa na akili za kijinga na malaya wa rushwa, ufisadi na wizi wa mali ya umma ndio utasimama na kumtukana Late JPM.

Kimantiki unashangilia upandaji madaraja na nyongeza ya 5000 ya mshahara wakati... ulipopanda hapajaboreshwa na unaendelea kutekeleza majukumu yaleyale..kwa usimamizi uleule refer maafisa magereza wanaorudi kushinda na wafungwa wakiwa na nyota mabegani... unashangilia ongezeko la mishahara wakati gharama za bidhaa bei juu zaidi ya 45% ya bei za kawaida... mfano karanga kilo ilikuwa 1800 leo 2800 mpya 3000 za last year... sijaongelea karatasi ...Rim toka 8000 mpaka 20,000 bado kuna mijitu mijinga na mifisadi kama Zitto, Bi tozo na genge lao la msoga aka anaupigwa mwingi wanamtukana JPM... mbwa kabisa.

Na huyu mama yenu muuongaza vikoba mwisho hii mitano ya marehemu baada ya hapo tutajua cha kufanya.
 

Best president kwa vigezo gani?. Tatizo mnataka tuamini Tanzania ilianza mwaka 2016. Mnadharau Sana. Watu wameihangaikia hii nchi Sana mpaka Magufuli kukuta Mambo yamenyooka. Hivi mwalimu Nyerere angekuwa ana ukabila na upendeleo Kama wa Magufuli leo Tanzania ingekuwa wapi.

To me Magufuli alikuwa worst president ever. Nashukuru maombi yangu yalitimia aliondolewa kwenye uso wa dunia.
 
JPM alikuwa mtu mzito sana, yaani amemaliza mwaka bado ni mada mitandaoni kila leo.
Leo nilikuwa naongea na mama , anashangaa hawa mateja walijificha wapi maana wizi umerejea hatari mtaani.
Jana gari la tanesco wanaomba ulinzi shirikishi kudhibiti wezi wa mafuta ya transforma.
Nikiangalia jitihada za nape na hii mitaaa naona tunawawekea vyuma mateja mitaani, ni bora tujengee nguzo za zege hazitokatwa na mateja.
Back to topic, JPM bado anaishi mioyoni mwa watu mpaka leo.
 
jibu ni moja tu, yule alikuwa Chuma kweli ni kosa kubwa kumfananisha na boflo au kitu kingine chochote kile
 
CAG natumika ili wananchi wawe wapumbavu waendelee kuibiwa kupitia viongozi wezi. Ila bahati mbaya watanzania wapo machi. Mabeberu wanafurahi sana wakipata kiongozi mpenda rushwa. Hakika Zitto na genge lake bado wanashangilia kifo cha Dkt Magufuli.
 
Tena mpaka huko maporini Dkt Magufuli yupo live. Nilienda vijiji vya mbali sana ndani ndani wanamlaani sana Mama Samia, yaani wanasema hivi hili limetoka wapi. Yaani Mama Samia mwanzoni watu walimpenda sana na walikuwa na huruma ya yeye kufiwa na bosi wake, ila alipoanza kejeli hasa kwa machinga, bei za mbolea etc na mwisho kabisa kuutangazia umma kila kitu kitapanda bei na mara amekuwa rais kwa kudra za mwenyezi mungu yaani mioyoni mwa watanzania hayupo kabisa. Ingawa hajachelewa kujirekebisha, aombe msamaha kwa kauli tata, atengue teuzi zote tata, arejee kujali maslahi mapana ya nchi, watanzania watamsamehe Mama yetu
 
Ukweli Ni kwamba mwamba Ni the best mpaka sasa na atazidi kuwatokea vyumbani wanapolala mpaka wauseme ukweli.

TIME HEALS ALL WOUNDS
 
Na mm naomba unijibu haya kuhusu serikali adilifu isiyona mdhaha na wizi
1.kwa nn ilikopa kushinda serikali yeyote tangu uhuru (ilivunja record)
2.Nani mmiliki halisi wa mayanga construction ?na kwanini ilichukua tenda zote kubwa?
3.kwa nn alichukua pesa bodi zote za mazao ,na korosho tu alichukua bil 300 wakapinga akasema atapiga viboko shangazi zao (haikuwa hela ya serikali ni ya wakulima)
4.tamisemi inaongoza kwa bajet kwa nn aliihamishia ikulu ili isikaguliwe shujaa anaogopa ukaguzi?
5.kwann aliweka kinga kwa spika jaji etc kuwa wasishitakiwe wakitoka madarakani alikuwa anaogopa nn juu ya matendo yake ya uadilifu?
 
aliwezaje kujenga daraja la tanzanite ? aliwezaje kujenga daraja la busisi ? aliwezaje kuhamisha makao makuu dodoma wakati marais wote walishidwa kwa ukosefu wa pesa?
Aliweza kupitia haya hapa
πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
Mikopo yenye riba kubwa za kibenki.
Kupora pesa za watu binafsi.
Kuiba pesa zote kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.
Kudhulumu wafanyakazi stahiki zao
Kuzuia ajira mpya kwenye serikali kwa miaka mitano.
Kupora wakulima wa korosho.
 
Pumba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…