mgt software
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 13,778
- 7,145
Kwako kichele CAG
Nimeshangazwa na kusikitishwa na pendekezo la CAG Kichere kuwa wastaafu wanauwekea mzigo mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kuendelea kupokea huduma za mfuko huo huku wakiwa hawachangii. Nimesikitika kwa sababu Kichere na genge lake wanajua tatizo linalousibu mfuko limetokea wapi. Kufanya anavyofanya CAG ni sawa na mtu kujificha kwenye shamba la karanga.
Serikali yetu ilivyo ya ajabu inaweza kununua ushauri wake na kesho sheria ikarekebishwa na wastaafu wakaondolewa kwenye mafao. Likitokea hilo wala msishangae wabunge wetu watalipitisha kama wanavyofanya kwa sheria zote kandamizi wanazoendelea kupitisha na Rais atayawekea sahihi kesh yake.
Kichere nimemshangaa sana kwa sababu nchini Morishasi kila mzee analipwa pensheni na anayefikisha miaka 100 pensheni yake inakuwa kubwa zaidi. Iweje CAG na genge lake wapendekeze wazee kunyimwa huduma ili wafe haraka au anashrikiana na wenye kikokotoo chao wastaafu waondoke mapema 67% yao ibakie kwenye mfuko?
Natamani marekebisho haya nayo yafanyike kabla ya uchaguzi ujao labda Mapambazuko yatawafikia wadanganyika wote.