CAG: Mradi wa Umeme wa Bwawa la Nyerere unatumia upembuzi wa mwaka 1970

Kila mwenye akili timamu na uwezo wa kufikiria alikuwa anajua kabisa hii Nchi ilikuwa inapigwa sana kipindi cha JPM, na kwa vile alikuwa anajiona yeye bora hakuwa radhi watu waseme madhaifu ya watu wake, hapo ndipo tatizo lilipokolea, angeshika hii Nchi kwa miaka 10 tungekuwa na hali mbaya sana.
 
Wapi imeonekana kuna wizi au ufisadi kwenye huu mradi?
 
Sasa wewe ulitaka uendelee kufanya kazi serikalini na cheti cha kufoji? Punguza jazba brother kaka ndio imeshakula kwako hvyo!

Nimeanza sasa PhD yangu hivyo kama Cbuo Kikuu huwa wanapokea Vyeti Feki ( vya Kufoji ) wakati Vyeti vyangu vya Vyuo Vikuu vyote Viwili ( vinavyotambuliwa na Serikali ) nilivyosoma Kihalali vipo na Kumaliza vyema kabisa basi sawa.
 
ufisadi sio kuiba pesa za umma tu. hata kutumia vibaya Kodi na rasilimali za umma ni ufisadi, kwa akili ndogo tu unaweza kujenga ikulu nyingine ya bilioni 500 na ushehe huku wanafunzi wanakosa vyoo na madarasa?
 
Elewa kuwa nilikuwa na budget ya upembuzi mpya, ilitumikaje? Au unawaza maandishi tu kuwa ni ya mwaka 40 au current?
 
Kwani kuna mtu anamsumbua hadi utake aachwe apumzike??
Sasa kama miradi haifai si mbomoe ili msikie vizuri.bomoeni kila kitu anzisheni vyenu.
Acheni Magu apumzike,enough is enough.
 
Tena ukileta independent auditing firm ndiyo kutakuwa na hatari zaidi
 
Huu mradi utatulipukia. Tofauti na walivyosema hao maofisa waandamizi, washauri waliona huu mradi hautalipa kutokana na uharibifu wa mazingira ( kukata miti, athari katika Rufiji Delta). Aidha, bwawa litajaa matope mapema sana. Ndio maana miaka yote hii hakujitokeza mtu kuufadhili au kuwekeza. Ni tembo mweupe.

Amandla...
 
Hiyo ya Chadema unawasingizia. CAG kapitia na kupitisha mahesabu yao. Baada ya wale wakina mama na Lijualikali kumwaga sumu bungeni, Takukuru nae akasema atapitia na mpaka leo yuko kimya. Hao wabunge walihama kwa maslahi yao binafsi na sio ufisadi wa michango yao.

Amandla...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…