CAG: Mradi wa Umeme wa Bwawa la Nyerere unatumia upembuzi wa mwaka 1970

CAG: Mradi wa Umeme wa Bwawa la Nyerere unatumia upembuzi wa mwaka 1970

Hili ndio swali ninalojiuliza baada ya ripoti ya CAG kubainiasha jambo hili na kuripotiwa na gazeti la The Citizen.

Habari husika utaipata kupitia link hii hapa chini:

Wanatafuta sababu za kusimamisha mradi maana wanaona hawatakua na uwezo wa kugharamia
 
Nchi ipo hivyo hivyo tu, ni nyie tu na mihemko yenu kwani kwa JK mlisemaje?.. watu wenye upeo mdogo sana wa kufikiri(Low thinking capacity) ndo wanaongeaga huo uk.uma. hakuna Raisi aliyeharibu wala kuipaisha nchi. Nchi ipo hivyo hivyo na CCM ni ileile tu. Nyie mnaofuata upepo na akili finyu ndo mnakuja na hivi vioja.
Mkuu wewe mwenye HIGH THINKING CAPACITY umeshagundua nini kipya katika dunia hii????
 
So what!!?
nyuzi za upondaji na watu wenye wivu zipo nyingi sana humu....nyuzi mojawapo hii hapa.
kazi nzuri za JPM zimeonekana.
Hili ndio kosa tunalofanya kama Jamii...., Issue sio kazi nzuri anayofanya au aliyofanya au watakaofanya kina nani..., Issue ni mambo ya kitaifa kwenda kwa misingi na utaratibu wa kuangalia yote hasi na chanya ili pasiwe na uwezekano wa hasara au kulauminiana

Huu mradi ni mzuri na unafaa kwa Taifa ila kufanya due dilligence huenda badala ya kutumia pesa nyingi tukatumia ndogo au badala ya kutumia mzabuni huyu tukatumia yule...

Hii nchi sio yetu tu bali mpaka vizazi vijavyo ambayo tukifanya makosa huenda makaburi yetu yakawa yanapondwa mawe...
 
Mi ninachojua vipimo vya sayansi havibadiliki.sasa hata kama ni vya miaka hiyo vipimo vipo vile vile
 
Project zote za JPM lazima wazipondeponde kwanza kabla ya kuzifutilia mbali ili waendeleze zao za upigaji kama bandari ya bagamoyo. Tusahau kuhusu sgr, bwawa la nyerere sijui kupeleka umeme kila kijiji by 2023 na mingineyo. Sasa hivi tupo kwenye kipindi cha kutengeneza ulaji hadi tushibe ndio hayo maproject yenu yaendelee

Umeme kupelekwa kila kijiji ni fedha za REA wala sio ubunifu wa Magufuli. Bwawa la SG ni la 6.5t ili kupata 2,115mg, kwanini tusiweke 3t, kupata zaidi ya 2,115mg kwenye gas ambayo tayari bomba la gas liko hapa Dar? Hiyo SGR, tayari JK alikuwa ameshafikia makubaliano ya mkopo wa exim bank ya China kutoa $7. Leo hii tumeshakopa zaidi ya $3.1b na bado hiyo reli haijafika hata nusu ya malengo.
 
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limeshindwa kuhuisha vipengele vyote vya upembuzi yakinifu uliofanyika awali katika ujenzi wa mradi wa umeme wa bwawa la Mwalimu Nyerere (JNHPP), imeeleza ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG).

Badala yake ripoti hiyo ya mwaka wa fedha unaoishia Juni 2020 imesema Tanesco lilitegemea upembuzi yakinifu ambao ulifanywa katika miaka ya 1970 na 1972 na kampuni ya M/S Norconsult ya Norway.

Pia shirika hilo linatumia mpango mtambuka wa mradi na ripoti ya uchunguzi wa kiufundi uliofanywa na kampuni ya M/S Hafslund na M/s Norplan pia kutoka Norway ambayo ilihuisha vipengele vya taarifa ya upembuzi yakinifu miaka ya 1980.

“Vipengele ambavyo havikufanyiwa mapitio na kuhuishwa ni pamoja na utafiti wa kiuchumi na kifedha wa mradi, tafiti za kuwepo kwa maji na uendeshaji endelevu wa mradi,” imesema ripoti hiyo.

Ripoti hiyo imesema maofisa waandamizi wa Tanesco waliozungumza na CAG walieleza kwamba, upembuzi yakinifu uliofanyika katika miaka ya 1970 ulionesha kwamba mradi unawezekana kitaalamu, kiuchumi na kifedha.

“Maofisa waliongeza kuwa kutokana na uharaka wa kuanza utekelezaji wa mradi, taarifa za upembuzi za awali hazikuweza kupitiwa upya zote ili kuzihuisha,” inaeleza.

Ripoti hiyo imesema kuhuishwa huko kwa upembuzi kunatakiwa kwa mujibu wa Sheria ya Umeme ya mwaka 2008, Sheria ya Umwagiliaji ya Kitaifa ya mwaka 2013, Sheria za Usimamizi ya Vyanzo vya Maji ya mwaka 2009 na Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya 2004.

Mwananchi
Aisee duniani kuna mijizi hakuna mfano!
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Tunarekebisha kuanzia na bandari ya Bagamoyo....

Usichoke kuandika uchochezi ila hakikisha kuwa nawewe ni mkwele...

Nchi ilikuwa inaendeshwa kwa utashi was MTU sheria zooote ziliwekwa pending!!
Kwa taratibu za kifedha karibu miradi yooote ya stoni itakuwa nje ya utaratibu!!
Kunahaja serikali yooote ijiuzulu tufanye uchaguzi upyaaa!! Stone hakushauriwa vyema na makamu wake,waziri mkuu,spika,bunge,chama nk.
Kama walijua hashauriki kwanini walituletea kama mgombea na wakawa wanamsifu kila dakika??
Kistaarabu serikali yooote ijiuzulu tuchague upya asisingiziwe MTU mmoja asiyeweza kurudi kuitetea!!!
  • bandari hovyo
  • atcl hovyo
  • utalii hovyo
  • mawasiliano hovyo
  • elimu hovyo
  • afya hovyo
  • demokrasia hovyo
Embu serikali istep down kidogo turudie uchaguzi maana Samoa alisema stone alikuwa mwalimu wake sasa kama mwalimu kaharibu hivi mwanafunzi wake je??
 
Ripoti imepikwa ndo inasomwa, kila kitu hasara, hakifai, acheni usenge wenu Nyinyi majizi, manyanganyi.
Mtaifuta kazi yake Magufuli miaka kenda na kenda Yumo tu.
 
Umeme kupelekwa kila kijiji ni fedha za REA wala sio ubunifu wa Magufuli. Bwawa la SG ni la 6.5t ili kupata 2,115mg, kwanini tusiweke 3t, kupata zaidi ya 2,115mg kwenye gas ambayo tayari bomba la gas liko hapa Dar? Hiyo SGR, tayari JK alikuwa ameshafikia makubaliano ya mkopo wa exim bank ya China kutoa $7. Leo hii tumeshakopa zaidi ya $3.1b na bado hiyo reli haijafika hata nusu ya malengo.
Nipe takwimu kabla ya JPM vijiji vingapi vilikuwa na umeme na hadi anaondoka vilikuwa vingapi ? Kwenye sgr unampa crédit aliyeota kufanya kuliko aliyefanya ?jamani hivi hivi tunaishi nchi tofauti au hii hii Tanzania ? Hospitali huduma ziliboreshwa na tumeona vituo vingi zaidi vya afya vikijengwa pamoja na project nyingine nyingi tu !!! Sasa hivi naona mnapambana kutuaminisha kuwa miradi yetu wenyewe kama sgr na bwawa la Nyerere ni ya hovyo bora ya huo watakaomiliki wachina kwa miaka mia. Yaani dunia ya leo unaingia mikataba ya akina mangungo unakata kipande cha nchi yako unawapa wakoloni watawale halafu unabaki unashangilia tu kama zuzu !!! Kweli nyie ni wazalendo wa kutupwa
 
Kwa taarifa yako umeme umekuwa ukisambazwa hapa nchini hatua kwa hatua, na hiyo ni toka enzi za ukoloni. Ni kweli inawezekana kiwango cha kuongezeka mtandao wa umeme nchini imekuwa juu kidogo chini ya watangulizi wake, lakini yeye pia aliminya sekta nyingine ambazo watangulizi wake waliwekeza nguvu huko. Upande wa hospitali, huduma hazijaboreshwa kwa kiwango kikubwa, lakini ni kweli majengo yameongezeka, lakini ubora wa huduma kwenye hospital, haukuwa na ubora unaotaka kutuongopea.

Halafu unapojenga utetezi wako, acha kuweka upotoshaji usio na tija ili kubeba hoja zako dhaifu. Hakuna anayesema miradi ya Magufuli ni ya hovyo, bali approach yake ya utekelezaji, na uchaguzi sahihi wa kipi afanye. Mradi wa SGR wakati anaingia madarakani alikuta kila kitu JK kashakamilisha ikiwa mkopo wa exim Bank ya China kwa kiwango cha $7b, akaingia yeye akabadili kwa maelezo ya kuwa anatumia fedha za ndani. Lakini hadi sasa ameshakopa $3.1, na bado huo mradi haujafika hata nusu. Cha ajabu alirudi huko huko China kukopa kwenye bank ya Standard Chartered, ili kuendelea na huo mradi wa SGR. Kama si wendawazimu ni nini?

Huo umeme wa SG, ukiacha mizengwe ambayo CAG kaanza kuonyesha, anasema ni mradi wa 6.5t, ili azalishe umeme wa 2,115m, wakati gas ambayo tayari bomba liko Dar, na tulikopa $1.2b, na matarajio ilikuwa ni kupata 5,000mg. Kwanini asiweke 3t tupate hizo 2,115mg, kisha hela inayobakia aingize pengine?
Kuhusu mradi wa Bagamoyo, kama kuna masharti mabaya ni kuyafanyia kazi, kisha kupima faida na hasara ya mradi huo. Hata hivyo ni wendawazimu mtu kujifanya mzalendo wa kuzuia mradi wa hivyo bila kuweka wazi mapungufu ya mradi, halafu akajenge uwanja wa ndege kijijini kwao wa 39b, ambao abiria kwa wiki hawafiki 20.
 
Watu hawajaiba sikubyingi, Magu aliwabana sana sasa wanatafuta njia fasafasta wajilipe.
 
Tunarekebisha kuanzia na bandari ya Bagamoyo....

Usichoke kuandika uchochezi ila hakikisha kuwa nawewe ni mkwele...
Mmezoea kutishia watu na kesi za uchochezi na uhujumu uchumi eeh!! Zama za udikteta uchwa... zimekwisha! zama zakutisha watu ili maovu yasisemwe,zama za kupiga watu risasi,kuteka na kutesa,zama za kutukana wanaoshauri,zama za kishamba MTU mmoja kujiona nchi yake,zama za kugawa hela barabarani na kumtaja Mungu kilasaa kumbe chini ya kapeti kuna uovu,zama za chuki kwa wanaokukosoa,zama za chama kimoja,zama za kilamtu mpumbavu isipokuwa yeye...
Tumejionea uongozi wa ajabu haijawahi tokea!! alivyosema Lissu. Angekuwepo hata "SIEIGII" angeogopa kusema haya
Jina limechafuka watu wakiliona wanajiskia hata kupu... endelea na uchawi sore uchawa labda itakusaidia!!
 
Kuna watu hawataki kuamini ripoti ya CAG kwa kuwa imekuja kipindi tuna msiba? Watafute ripoti ya assad ya mwaka jana walinganishe ipi ina mapungufu zaidi..ya upigaji
 
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limeshindwa kuhuisha vipengele vyote vya upembuzi yakinifu uliofanyika awali katika ujenzi wa mradi wa umeme wa bwawa la Mwalimu Nyerere (JNHPP), imeeleza ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG).

Badala yake ripoti hiyo ya mwaka wa fedha unaoishia Juni 2020 imesema Tanesco lilitegemea upembuzi yakinifu ambao ulifanywa katika miaka ya 1970 na 1972 na kampuni ya M/S Norconsult ya Norway.

Pia shirika hilo linatumia mpango mtambuka wa mradi na ripoti ya uchunguzi wa kiufundi uliofanywa na kampuni ya M/S Hafslund na M/s Norplan pia kutoka Norway ambayo ilihuisha vipengele vya taarifa ya upembuzi yakinifu miaka ya 1980.

“Vipengele ambavyo havikufanyiwa mapitio na kuhuishwa ni pamoja na utafiti wa kiuchumi na kifedha wa mradi, tafiti za kuwepo kwa maji na uendeshaji endelevu wa mradi,” imesema ripoti hiyo.

Ripoti hiyo imesema maofisa waandamizi wa Tanesco waliozungumza na CAG walieleza kwamba, upembuzi yakinifu uliofanyika katika miaka ya 1970 ulionesha kwamba mradi unawezekana kitaalamu, kiuchumi na kifedha.

“Maofisa waliongeza kuwa kutokana na uharaka wa kuanza utekelezaji wa mradi, taarifa za upembuzi za awali hazikuweza kupitiwa upya zote ili kuzihuisha,” inaeleza.

Ripoti hiyo imesema kuhuishwa huko kwa upembuzi kunatakiwa kwa mujibu wa Sheria ya Umeme ya mwaka 2008, Sheria ya Umwagiliaji ya Kitaifa ya mwaka 2013, Sheria za Usimamizi ya Vyanzo vya Maji ya mwaka 2009 na Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya 2004.

Mwananchi
Kama ni dosari,basi ni dosari na imeelezwa kwa nia ya kuzuia siku zijazo kosa la hivi lisirudiwe
 
Back
Top Bottom