CAG mstaafu Uttoh: Hakuna Shirika lolote la ndege duniani lililopata faida baada tu ya kuanzishwa, ATCL haijawahi kulipa Gawio Serikalini

Plan was 5 years ya Break Even Point.
Kutokana na corona hatuna uhakika..

 
Hapa mwamba kachemka kidogo
Tanapa ni shirika la umma
Tanesco ni shirika la umma
Dawasa ni shirika la umma
Yote hayo yanafanya biashara
Kwa akili yako faida na hasara ya TANAPA unaipimaje? Hao wanafanya makusanyo hawafanyi biashara na wanatoa matumizi yao wao kama shirika kisha pesa zote ni za serikali...ukifanya hizo hesabu za TANAPA basi jua ni asilimia 18 ya ardhi ipo tu inakaliwa na wanyama na mimea na je thamani yao ni kiasi gani kwa fedha taslimu kama kwa mfano ardhi hiyo ingetumiwa kwa namna nyingine?

Humo kuna mininga ya kutosha, kuna madini sehemu zingine etc etc hizo zote linganisha na hiyo token ya trilion 6 kwa mwaka tena pato ghafi uone kama ni faida au hasara in terms of cash...Nadhani kwanza naongea na mtu ambaye hata principles za valuation hajui...Sorry!
 
Wanaopenda kusikia wanachokipenda kukisikia hata kama siyo fact watapinga hili
Hata ninyi masikio yenu yanapenda kusikia kile tu ambacho kinaleta raharuki,uttoh angepondea government mngesikika mkisifu kuwa huyu uttoh ni jembe
 
Fact
 
Hayajawahi toa dividend, yametoa gawiwo ambalo lipo kisheria ila sheria hii ilikuwa haitekelezwi Hayati aliitekeleza...
Ndugu yangu nadhani hufahamu chochote kuhusu gawio.
Dividend=Gawio.
Gawio linatokana na faida iliyozalishwa kibiashara. Kama biashara imezalisha hasara maana yake haipaswi kutoa gawio, hasara ile inafidiwa na mtaji.
Kilichofanywa na serikali ya Magufuli ni hadaa kwa 100%.
 
Mkuu una background yoyote ya uhasibu au unalazimisha Mambo tu,kwa sababu haya ni Mambo ya kitaaluma hayataki siasa
Yes tena nalifundisha kabisa hilo somo, mbali zaidi ni expwrt wa project management na pia ni mchumi kwahiyo napoeleza situmii hisia natumia utaalamu na practical experiences
 
Hakuna shirika la umma Tanzania linalotoa gawiwo la faida...Usi kariri...gawiwo hilo linatolewa kwa mujibu wa sheria kuonyesha commitment kwa serikali kwakua mashirika ya umma hata kama yanafanya biashara bado yanakuwa highly subsidized indirectly na serikali through kodi zetu. Huwezi kulifanyia evaluation kama private company...Huo uhasibu kaanzeni upya kuusoma...Ukitaka model za jinsi ya kufanya muende Scandnavia yapo ya hivyo kama yetu mengi tu ndiyo maana mabepari wanasema serikali haitakiwi kufanya biashara...
 
Yes tena nalifundisha kabisa hilo somo, mbali zaidi ni expwrt wa project management na pia ni mchumi kwahiyo napoeleza situmii hisia natumia utaalamu na practical experiences
Kwa uchumi na project management naweza kukubali lakini uhasibu napata Shaka labda Kama ulisoma basic book keeping certificate BBC
Kwenye uhasibu divident ni maana moja tu,gawiwo kwa wanahisa
 
Ndugu yangu acha kuzunguka kwa maneno. Shirika la ATCL lilianzishwa kwa lengo la kufanya kibiashara kwa 100%, na halikuanzishwa ili kutoa huduma za kijamii ili kusaidia watu fulani fulani. Usilazimishe kuifanya ATCL kuwa taasisi ya kijamii ya kutoa huduma.
Liko kibiashara, limekuja kushindana na makampuni mengine na lazima tulipime kibiashara.

Kuhusu ATCL kusaidia sekta zingine, hilo sio lengo la msingi la kuanzishwa kwa ATCL, hilo jambo haliwezi kupimika moja kwa moja na hatuna sababu ya kulitazama kama ndio msingi uwepo wa ATCL.

Kukusaidia tu, sekta ya utalii hapa Tanzania kwa zaidi ya 90% inategemea ndege za mashirika binafsi kuliko ATCL. ATCL iwepo ama isiwepo hakuna impact yoyote ya msingi katika usafirishaji wa abiria na kukuza utalii. ATCL ipo kuleta chachu ya ushindani tu lakini hakuna kitu kipya.
 
Kwa uchumi na project management naweza kukubali lakini uhasibu napata Shaka labda Kama ulisoma basic book keeping certificate BBC
Kwenye uhasibu divident no maana moja tu,gawiwo kwa wanahisa
Kwahiyo serikali ina hisa ngapi kwa shirika lake la umma kwamfano?

Unajua msiwe mnakariri, kwakjua kuwa serikali ni custodian wa hayo mashirika kwakua yanamilikiwa na raia wa Tanzania waliweka 15% fixed ya gawiwo kwa mashirika yake pamoja na kuwa pesa zote ni za umma wa watanzania...Mashirika hayo mengine yanafanya full makusanyo, mengine yana fanya biashara, mengine yana fanya biashara na kutoa huduma na mengine yanatoa huduma pekee...Kwahiyo ukiniambia kuna frame ya kufanya accounting in international standards nakubaliana na wewe na lazima kuna assumptions za kufanya hivyo na maadamu kuna assumptions subjectivity is guaranteed...Ila kwakua umesoma tu darasani gawiwo ni kwa hisa basi usije ghafla unataka uone gawiwo kwenye faida peke...Angalia context under which you frame ypur accounting proceedures.

Ni kweli mimi siyo mhasibu by profession nimesoma uhasibu at basic na ninafundisha somo hilo kutoa basics za kufanya accounting...I can therefore see this in more than one perspective kwakua pia nilipata privillage ya kusoma project management at advance level kwakutumia both objective PERT methods na normative models zote na kwa aina mbali mbali from private, common to public...Nataka tu kukujuza ili upate amani siyo kujimwambafai, if I might sound so am sorry is not intentional!
 
Sheria inayataka mashirika ya umma kupeleka gawio serikalini kila mwaka. Sasa hilo gawio wanalitoa wapi kama sio kwenye faida waliozalisha?

Nini mantiki ya kutakiwa kutoa gawio kama hawapaswi kuzalisha faida kwanza?
 
Jamaa yupo vizuri kwenye kufosi kingi
Anakwambia uende Scandinavia ukajifunze uendeshaji wa mashirika ya umma!
 
Kwa regime ya Magufuli ndege hazikununuliwa pasipo objective, zilinunuliwa kuinua utalii na kuchochea uchumi, zipo hotuba zake kibao kwaajili hiyo...Do not try to fit a rectangular peg in a roumd hole to suit your personal desire...Kwamba hiyo objective yake haikueleweka na ninyi auditors wetu mkaenda huku mmekariri na kufanya aidits zenu kwa financial analyses pekee bila kujali nature ya hiyo business basi hilo no jambo jingine...Basi mkafanye na audits za hasara na faida kwa ma NGO yanayopokea madola toka kwa wazungu mtuambie hasara na faida zake, je hayafanyiwi audits?
 
Sheria inayataka mashirika ya umma kupeleka gawio serikalini kila mwaka. Sasa hilo gawio wanalitoa wapi kama sio kwenye faida waliozalisha?

Nini mantiki ya kutakiwa kutoa gawio kama hawapaswi kuzalisha faida kwanza?
Fuatilia maelezo yangu, kama unataka kuelewa utaelewa kama unatafuta ligi basi am out...UDSM walipata faida kiasi gani mpaka wakatoa gawiwo? Wana hisa kiasi gani za biashara ipi kwamfano?
 
Tulia nchi ijengwe scha jazba.Trillion 3 zimetumika lini?
 
Ni kweli mimi siyo mhasibu by professuin nimesoma uhasibu at basic na ninafundisha somo hilo kutoa basics za kufanya accounting..
Hapo hapo umejiondoa kwenye mjadala
Ndio Mana nilihisi kuwa wewe si muhasibu
Wewe ilmu yako ni debit na credit,ku journalize na cash book baas.
Hata preparation of final accounts huwezi,kwa hiyo haya Mambo ya dividents waulize watu waliokuzidi kidogo na pitia Sheria ya uanzishwaji wa shirika la uuma husika utapata elimu nzuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…